Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Magharibi Yaangazia Uhalifu wa India

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri Mkuu wa Canada Justin Bwana Trudeau alisema mapema wiki hii kwamba kulikuwa na ushahidi wa kuaminika serikali ya India ilishiriki katika mauaji ya kinyume cha sheria ya raia mmoja wa Canada kwenye ardhi ya Canada, mwanaharakati wa Kikalasinga ambaye India amemtuhumu kwa ugaidi.

Jijini New York maripota kadhaa waliuliza, je ni washirika wa Canada? "Hadi sasa," mwandishi wa habari mmoja alimwambia Bw Trudeau, "unaonekana kana kwamba uko peke yako".

Waziri wa Mambo ya nje wa Uingereza James Cleverly alisema nchi yake imeyachukulia "kwa umakini sana mambo yanayosemwa na Canada". Kwa kutumia lugha karibu sawa, Australia ilisema "ina wasiwasi sana" na tuhma hizo.

Lakini labda kimya kikubwa zaidi kilitoka kwa jirani wa kusini mwa Canada, Marekani. Nchi hizo mbili ni washirika wa karibu, lakini Marekani haikuongea kwa hasira kwa niaba ya Canada.

Wakati Rais Joe Biden alipoinyanyua hadharani India wiki hii, wakati akizungumza katika UN, haikuwa kulaani, bali kuisifu nchi kwa kusaidia kuanzisha njia mpya ya kiuchumi.

"Marekani, Uingereza, na washirika hawa wote wa Magharibi na Indo-Pasifiki wameunda mkakati ambao unazingatia sana India, kuwa ngome na uzani kwa China. Hicho ni kitu ambacho hawawezi kukimudu nje dirishani," Alisema Xavier Delgado, mtafiti katika Taasisi ya Canada ya Kituo cha Wilson. (Chanzo: BBC)

Maoni:

Canada leo inakabiliwa na uhalisia wa Machiavelli wa mahusiano ya kimataifa katika mfumo wa kilimwengu wa kirasilimali. Kama Waziri Mkuu wa Uingereza Henry Palmerstone alivyosema kwa Bunge la House of Commons mnamo 1848 "Hatuna washirika wa milele, na hatuna maadui wa kuendelea. Maslahi yetu ndiyo ya milele na ya kudumu, na maslahi hayo ni jukumu letu kuyafuata."

Licha ya majigambo yao yote juu ya haki za binadamu, hadhi na utaratibu wa msingi wa sheria, Magharibi ya kirasilimali hutathmini kila uamuzi juu ya maslahi yao ya kichoyo, sio kulingana na kanuni zozote za usahihi na makosa. Ikiwa maslahi yao kwa siku fulani yatatokea sanjari na kauli mbiu maarufu ya maadili, basi watatangaza kwa sauti kubwa kuwa ndio msingi. Uongo huu umethibitishwa kupitia unafiki na undumakuwili wao unaojikariri kote ulimwenguni.

Mauaji kinyume cha sheria ni makosa, isipokuwa ikiwa ni kwa adui wao wenyewe waliyemtangaza. Uhuru wa kuzungumza lazima ukuuzwe isipokuwa ikiwa ni mazungumzo dhidi ya maslahi yao wenyewe. Tawala za kidikteta ni mbaya, isipokuwa zile zinazo tumikia maslahi yetu nje ya nchi. Chaguo huru la dini ni kwa wote, isipokuwa wale wanaochagua Uislamu.

Sasa kwa kuwa Marekani inaitegemea India kudhibiti ukuaji wa China kama dola, serikali ya Modi inahisi kuwa na nguvu ya kuzitesa jamii zake za wachache, kwani hawaogopi kuadhibiwa na Marekani au washirika wake.

Uislamu ni mwongozo kwa wanadamu wote kuwaonyesha nuru baada ya giza. Sera kama hizo za mbwa kumla mbwa hazina thamani kwa Waislamu, ambao lazima washikamane na sheria za Mwenyezi Mungu kwa mahusiano ya ndani pamoja na ya kimataifa.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yahya Nisbet
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Uingereza

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu