Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Viziwi, Mabubu, Vipofu; kwa hivyo hawataregea [kwenye njia ya haki]

(Imetafsiriwa)

Habari:

ISLAMABAD: Onyo la wazi lilikuja kutoka Benki ya Dunia kabla ya mzunguko mpya wa uchaguzi nchini Pakistan, likisema kwamba Pakistan iko katika mgogoro wake wa hatua ambapo asilimia 40 ya idadi ya watu wanaishi chini ya umaskini. Kulifanya liwe wazi kuwa wakopeshaji wa kimataifa na washirika wa maendeleo wanaweza kushauri tu juu ya uzoefu wa kimataifa wa mafanikio na baadhi ya ufadhili, lakini machaguo mgumu na maamuzi ya kusahihisha mwenendo yanaweza kuchukuliwa tu ndani ya nchi. (Chanzo: Dawn)

Maoni:

Umasikini nchini Pakistan sio kwa sababu ya kukosekana uwezo katika watu wake au rasilimali za ardhi yake lakini kwa sababu ya matokeo yaliyoshauriwa na kutekelezwa kikatili na uongozi kwa jina la 'maamuzi ya kurekebisha mwenendo'. Hili linahimiliwa na watu wa Pakistan na linathibitisha kutokuwa na uwezo na ulafi wa watawala wake na mabwana wanaowategemea. Watu tayari wanakabiliwa na kuongezeka kwa bei ya kila siku huku serikali ikishughulishwa na kuchukua hatua za Mfuko wa Fedha wa Kimataifa (IMF) za kupokea bahashishi iliyokubaliwa hapo awali ya bilioni 1.1 kutoka mkopo wa mwaka 2019. IMF, tangu kuanzishwa kwake baada ya WWII kwa jina la kuleta utulivu wa uchumi wa dunia, inasalia sababu kuu ya kuuharibu. Pakistan pamoja na nchi zengine nyingi wahasiriwa ni tajiri katika rasilimali na ustadi, ambayo kwa kweli ni tishio kwa wakiritimba hawa wa kimataifa.

Utelekezaji wa kisiasa nchini Pakistan umesababisha utelekezaji wa kijamii na mipango kama vile IMF inavyoathiri watu kwani kuna ongezeko la ushuru na bei ya bidhaa msingi zinaendelea kuongezeka. Watawala wetu huchaguliwa, na kuteuliwa kwetu kwa maelezo ya kazi ya kwanza kutumikia maslahi ya Magharibi, kuwanyamazisha watu, na kisha wako huru kujihudumia wenyewe pia. Kipote hiki cha watawala wana hatia ya uzembe na mapendeleo. Kipote cha mabepari wa Pakistan kilifanikiwa sana wakati wa Raj wa Kiingereza kupitia uporaji na ufujaji wa rasilimali za umma, na uteuzi katika utawala wa kikoloni na hawakuchukua muda mwingi kujimakinisha kama wasuluhishi pekee wa usambazaji wa utajiri wa kitaifa. Kutoona mbali kwa taasisi zetu ni kwa Kiitikadi kwani wamechagua kuishi katika wakati huu na kufurahiya. بُكْمٌ عُمْيٌ فَهُمْ لَا يَرْجِعُونَ] “Viziwi, mabubu, vipofu; kwa hivyo hawatarejea.” [Al-Baqara: 18].

Shamshad Ahmed, waziri wa zamani wa mambo ya nje wa Pakistan na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa, katika mahojiano moja, alisema "Natamani watawala wangejue misingi ya uchumi: mkopo sio mtaji, lakini ni dhima. Na mkopo ambao IMF inatoa kwa nchi kama zetu imeundwa kutia mtegoni kwa deni lisilo na mwisho kwa agizo la Marekani,"

Watawala hawa sio wapumbavu, na wanajua vizuri jinsi ya kulinda na kusimamia fedha zao wenyewe. Kamwe hawaziweki mali zao za kidunia hatarini, hata wakijua kuwa watangulizi wao wasaliti wote wameacha kila kitu nyuma.

[وَيْلٌۭ لِّكُلِّ هُمَزَةٍۢ لُّمَزَةٍ * ٱلَّذِى جَمَعَ مَالًۭا وَعَدَّدَهُۥ * يَحْسَبُ أَنَّ مَالَهُۥٓ أَخْلَدَهُۥ * كَلَّا ۖ لَيُنۢبَذَنَّ فِى ٱلْحُطَمَةِ]

“Ole wake kila safihi, msengenyaji! Aliye kusanya mali na kuyahisabu. Anadhani ya kuwa mali yake yatambakisha milele! Hasha! Atavurumishwa katika H'ut'ama.” [Al-Humaza: 1-4]

Ulimwengu mzima unahitaji mno Khilafah Rashida kwa njia ya Utume kwani huu ndio mfumo pekee uliopeanwa na Mwenyezi Mungu (swt) unaoelewa mahitaji na mapungufu ya wanadamu. Mfumo wetu wa sasa wa kiuchumi unatuumiza kwa viwango vingi, kuanzia kwa utumizi mbaya wa vifungu vya Mwenyezi Mungu (swt) na kuharibu vizazi vijavyo na maisha yetu ya akhera. Ummah wa Kiislamu hauhitaji ushauri wowote kutoka kwa maadui wa Mwenyezi Mungu na unajua kuwa uchumi uliojengwa juu ya riba ni haramu, na kuukumbatia imetuletea udhalilifu na matusi katika ulimwengu huu huku tukiwa tumeharibu maisha yetu yajayo vilevile. Kukataa Riba kwa mustawa wa mtu binafsi, ambako Waislamu wengi hufanya, hakuwezi kutatua ugonjwa huu wa jamii. Inahitaji kusimamishwa kwa dola ya Khilafah ambayo itaondoa riba, kukataa riba yote na kuwahisabu watawala mafisadi ambao wameleta mateso haya na udhalilifu kwa Ummah wa Mtume Mtukufu (saw).

[يَمْحَقُ ٱللَّهُ ٱلرِّبَوٰا۟ وَيُرْبِى ٱلصَّدَقَـٰتِ ۗ وَٱللَّهُ لَا يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ]

“Mwenyezi Mungu huiondolea baraka riba, na huzibariki sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukanya na afanyae dhambi.” [Al-Baqara: 276]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ikhlaq Jehan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu