Jumanne, 05 Rabi' al-thani 1446 | 2024/10/08
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Utenganishaji Mamlaka? Kweli?

(Imetafsiriwa)

Habari:

Hivi karibuni, suala linalohusisha na mfumo wa sheria wa nchi liligonga vichwa vya habari kwenye vyombo vya habari. Mahakama Kuu ya Malaysia ilitoa ombi kutoka kwa waendesha mashtaka kuondoa mashtaka yote ya ufisadi dhidi ya Naibu Waziri Mkuu wa nchi hiyo Ahmad Zahid Hamidi katika kesi yake ya ufisadi wa Wakfu wa Charity. Mahakama ilimpa Ahmad Zahid, ambaye alikuwa akikabiliwa na mashtaka 47 ya uvunjaji wa kijinai (CBT), hongo na utapeli wa pesa, uondolewaji mashtaka pasi na kutokosekana hati (DNAA). Uamuzi huu umesababisha mihemko mbali mbali. Kwa wafuasi sugu wa chama tawala, hili lilionekana kuwa uamuzi sahihi na vyama vyote vinatarajiwa kuuheshimu. Kwa upinzani, hii ni aina fulani ya uingiliaji wa kisiasa katika mfumo wa sheria wa nchi. Ama kwa watu wa kawaida, wanashauriwa kukubali uamuzi wa Mahakama na kuheshimu utawala wa sheria iliyorithiwa kutoka kwa wakoloni ingawa heshima hii imekiukwa wazi kwa madai ya 'mikono isiyoonekana' ili kuokoa viongozi wa juu wa vyama tawala.

Maoni:

Licha ya kushinikizwa na upinzani katika suala hili la DNAA, Waziri Mkuu, Anwar Ibrahim, amesisitiza mara kwa mara kwamba hakuingilia kesi ya mahakama. Licha ya hayo, dhana kwamba kuna uingiliaji kati wa baraza la mawaziri katika suala hili linalohusiana na DNAA tayari imepenya katika ngazi ya umma. Matokeo yake kumekuwa na sauti ambazo zinapendekeza kwamba utenganishaji mamlaka kati ya baraza la  mawaziri na mahakama unapaswa kutekelezwa kwa umakini.

Nchini Malaysia, mfumo wa serikali unafuata mtindo wa nadharia ya utenganishaji mamlaka. Kwa mujibu wa nadharia hii, mfumo wa serikali umegawanywa katika baraza la mawaziri, bunge na mahakama. Katika muundo huu, Bunge ndio chombo kinachowajibika kutunga kanuni na sheria. Mamlaka ya Baraza la Mawaziri (Serikali) ni kutekeleza sheria zilizotengezwa na Bunge huku idara ya mahakama inasimamia na kufuatilia utekelezaji wa sheria hizi. Hata hivyo, matatizo huanza kujitokeza wakati wanachama wa serikali wanateuliwa kutoka miongoni mwa wabunge. Kunawezaje basi, kuwa na mtengano wa mamlaka ikiwa Bunge na baraza la mawaziri ni kundi moja la watu na baya zaidi, maafisa wa mahakama wao wenyewe wameteuliwa na baraza la mawaziri!

Katika Uislamu, mfumo wa sheria unatabikishwa na idara ya mahakama inayojumuisha Mahakama ya Madhalim, Mahaka ya Utesi (Khusumat) na Mahakama ya Hisbah. Zote tatu zimeasisiwa kwa msingi wa Aqidah na chimbiko lake ni kutoka kwa wahyi wa Mwenyezi Mungu (swt). Mkuu wa kila mahakama atahakikisha kwamba michakato yote ya korti inaenda kulingana na hukmu za sheria za Kiislamu. Uteuzi wa mkuu wa kila mahakama hufanywa na Khalifa. Watachaguliwa kutoka miongoni mwa watu wanaostahili zaidi. Ingawa kihistoria kumekuwa na udhaifu na dosari katika utekelezaji wake, hii ilitokana na sababu za kibinadamu. Katika hali ambayo mfumo wa sheria wa Kiislamu 'unatumiwa vibaya' na muundo wowote ndani ya mfumo wa Khilafah, hapo suala hilo litashughulikiwa na Mahakama ya Madhalim, ambayo ni korti ambayo dori yake ni kushughulikia mizozo inayoibuka kati ya watu na serikali. Mahakama ya Madhalim ina haki ya kuwahukumu watu walioshtakiwa, bila kujali kama yeye ni Khalifa, wasaidizi wake au maafisa wowote wa dola. Katika Khilafah, ni Khalifa pekee ndiye aliyeidhinishwa kutabikisha sheria nzima ya Kiislamu juu ya watu. Kwa kuwa utabikishaji wa Sharia ni amri kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) hakuna vyama vya upinzani katika kujadili utabikishaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu (swt). Ndani ya muundo wa Khilafah, kuna Majlis ya Ummah ingawa kazi yake sio kupinga, lakini kuhakikisha kuwa utabikishaji wa Sharia unafanywa kwa uadilifu na kwa uhakika na taasisi ya Khilafah.

​Suala la kisheria ambalo linaumiza nchi kwa sasa sio jambo jipya. Nadharia ya utenganishaji mamlaka wanayojivunia wafuasi wa serikali ya sasa 'inaonekana kuwa nzuri' ndani ya vitabu vya vilivypitwa na wakari vya falsafa ya Kimagharibi. Lakini, linapotekelezwa, kuna nafasi kubwa ya udanganyifu wa vyama visivyo na ukweli. Huu sio mfumo wa kisheria ulioteremshwa na Mwenyezi Mungu (swt). Muundo pekee wa serikali ya Kiislamu ni Khilafah, mfumo uliorithiwa kutoka kwa Mtume (saw), ambao unatekeleza Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume wake kwa ukamilifu. Kwa hivyo, maadamu mfumo huu wa kidemokrasia haubadilishwi kwa mfumo wa Kiislamu, suala hili kamwe halitatatuliwa. Njia pekee ya kupata haki ya kweli ni kusimamisha tena dola ya Khilafah itakayohukumu kwa Quran na Sunnah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu