Jumapili, 04 Jumada al-awwal 1444 | 2022/11/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Demokrasia ni Chombo cha Kuitiisha Pakistan kwa Hadhara Fisadi ya Kimagharibi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Seneta Mushtaq Ahmad mnamo Jumatatu, 5 Septemba 2022, aliwasilisha mswada wa marekebisho katika Sheria ya Ulinzi wa Wanaobadili jinsia kwa Kamati ya Kudumu ya Seneti ya Haki za Kibinadamu. Katika mkutano huo, Seneta Mushtaq Ahmad alisema kuwa, "...sheria kuhusu jamii ya watu waliobadili jinsia ni kinyume na Qur'an na Sunnah na itakuza ushoga." Wizara ya Haki za Kibinadamu ilipinga marekebisho hayo.

Maoni:

Sheria ya Watu Waliobadili Jinsia (Ulinzi wa Haki) 2018 ilipitishwa na bunge la Pakistan, mwanzoni, mnamo Mei 2018. Iliwasilishwa kama mswada wa kusahilisha matatizo yanayowakabili wale wenye jinsia isiyoeleweka, kwani wanakabiliwa na ugumu wa kupata vitambulisho vya kitaifa na leseni za kuendesha gari. Hata hivyo, kiuhalisia ni jaribio la mwelekeo wa kijinsia, kitambulisho cha kijinsia, maelezo ya kijinsia na sifa za kijinsia kulingana na Kanuni za Yogyakarta zilizowekwa nchini Indonesia mwaka wa 2006, kisha zikapanuliwa mwaka wa 2017. Kanuni za Yogyakarta zinabainisha kuwa kitambulisho cha kijinsia kinaeleweka kukusudia hisia ya kina ya ndani na ya kibinafsi ya jinsia kwa kila mtu, ambayo inaweza kuendana au kutoendana na jinsia iliyo peanwa wakati wa kuzaliwa. Haishangazi kwamba Kifungu cha 2(f) cha Sheria ya Ulinzi wa Wanaobadili jinsia kinafafanua "kitambulisho cha kijinsia" kama "hisia ya ndani ya mtu kama mwanaume, mwanamke au mchanganyiko wa zote mbili au isiokuwa yoyote ambayo yaweza kuendana au la na jinsia iliyo peanwa wakati wa kuzaliwa."

Mnamo tarehe 27 Aprili 2021, sheria hii ilipingwa katika Mahakama ya Shariah ya Shirikisho ya Pakistan kwa kugongana na maamrisho ya Kiislamu. Ni sheria iliyopinda inayomruhusu mwanamume kujitangaza kuwa ni mwanamke na kisha kuoa mwanaume. Ni kufiniko cha kisheria kwa mashoga na wasagaji ndani ya dola iliyoasisiwa kwa jina la Uislamu. Suala hili sasa limekuwa mjadala mkubwa ndani ya Pakistan katika wiki mbili zilizopita. Ghafla, vyama vikuu vya kisiasa vya Kiislamu vyenye uwakilishi bungeni, vinahojiwa na watu ni vipi viliruhusu sheria hiyo ovu kupitishwa. Waislamu wanajua kuwa demokrasia haitokamani na Uislamu. Mara nyingi wanawauliza wanazuoni kutoka katika vyama hivi vya kisiasa vya Kiislamu kwa nini wanashiriki katika mfumo ambao hautomakani na Uislamu. Maulamaa kama hao hunadai kuwa demokrasia ndiyo chaguo pekee linalopatikana la kubadilisha sheria za kikafiri kuwa sheria za Uislamu.

Hata hivyo, demokrasia ni chombo kilichobuniwa na Magharibi kuyafanya matamanio na matakwa yao kuwa sheria. Haijalishi watu wa vyama vya Kiislamu wana ikhlasi kiasi gani, wanaoshiriki ndani ya demokrasia, demokrasia huzuia mabadiliko ya sheria zilizotungwa na mwanadamu kwa sheria za kiwahyi. Demokrasia inatoa taswira ya uongo kwamba kheri inaweza kuwa matokeo. Kiuhalisia, inakaribisha adhabu ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kutawala kwa ukafiri. Inawakengeusha wenye ikhlasi kutoka katika utabikishaji msingi wa Uislamu. Inawashirikisha ndani ya demokrasia, wakifukuzia maagizo machache yanayotoa taswira potofu kwamba demokrasia inaweza kufanywa kuulinda Uislamu.

Waislamu lazima wasipoteze muda zaidi katika demokrasia. Waislamu wamepoteza miaka thelathini kujaribu tu kuondoa riba kupitia demokrasia. Ni wakati sasa wa kuiondoa demokrasia na kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume inayofunga kabisa milango ya sheria zinazoruhusu uovu na dhambi.

(وَلُوطاً آتَيْنَاهُ حُكْماً وَعِلْماً وَنَجَّيْنَاهُ مِنَ الْقَرْيَةِ الَّتِي كَانَتْ تَعْمَلُ الْخَبَائِثَ إِنَّهُمْ كَانُوا قَوْمَ سَوْءٍ فَاسِقِينَ)

“Na Luut'i tukampa hukumu na ilimu na tukamwokoa na ule mji ulio kuwa ukifanya maovu. Hakika hao walikuwa watu wabaya, wachafu.” [Surah Al-Anbiyaa, 21:74]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu