Jumapili, 22 Muharram 1446 | 2024/07/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Katiba za kutungwa na Wanadamu ni rahisi kukengeukwa na kubadilishwa

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mahakama ya Upeo imetoa uamuzi wa kuusambaratisha mradi wa ujenzi wa madaraja lakini ikafungua dirisha kwa vinara wa makubaliano ya ‘handshake’ kuanzisha marekebisho  mpya ya kikatiba. Kwenye uamuzi wake wa kihistoria, siku ya Alhamisi 31 Machi, 2022 jopo la majaji saba lilibatilisha hoja tano za mahakama ya rufaa zilizotumia kupinga mabadiliko ya kikatiba kama yalivyopendekezwa na mradi wa BBI. Miongoni mwa masuala muhimu yaliyotajwa na mahakama ya upeo ni kwamba Katiba ya Kenya haina msingi wa kikanuni ‘basic structure’ kumaanisha kwamba hakuna kipengele cha kikatiba kinachowezwa kurekebishwa maadam sheria ni yenye kufuatwa.

Maoni:

Ni bayana kwamba uamuzi wa mahakama ya upeo kuhusu BBI umeonesha udhaifu mkubwa wa Demokrasia inayodai kwamba ubwana ni wa watu yaani kuwa mwanadamu ana mamlaka ya kutunga, kulinda na kuhifadhi kanuni. Kanuni za kutungwa na wanadamu hukabiliwa na ukiukwaji na mabadiliko, kwani kwa uhakika kiasili mwanadamu ni dhaifu, mwenye mapungufu na mwenye upeo maalum. Kwa hivyo hata hiyo nadharia ya mfumo wa kimsingi hausalimiki na kutovunjwa kwani mwanadamu ni mwenye kupelekwa na maslahi.

Mabadiliko ya kikatiba ya Kidemokrasia ambayo mara kwa mara hufanyika kwenye mataifa mbalimbali kwa hoja kuwa jamii hukabiliwa na dhurufu hivyo kuweka mazingira ya kuhitajika mabadiliko ya katiba ni dalili nyengine ya ajizi ya mwanadamu na mapungufu yake ya kutoweza kuweka sheria zinazodhamini mahusiano mazuri katika jamii. Uhalisia wa katiba za kutungwa ni kuwa haziwezi kuacha kufanyiwa marekebisho kwani haziwezi kukabiliana na kipengele cha wakati na hii ni kama inavyoshuhudiwa kwenye katiba zote za kutungwa zilizoko duniani.

Kwa kuwa huu ndio ukweli usiopingika, mwito wa marekebisho ya kikatiba na mabadiliko ndani ya jamii ya Kidemokrasia kamwe hautokoma. Mchakato huu utaendelea kusababisha mivutano ya kisiasa na vuta ni kuvute huku jamii siku zote ikiachwa kwenye ombwe. Kosa kubwa la Demokrasia lipo katika kumpa mwanadamu mamlaka ya ubwana wa kutunga kanuni huku ikikana mamlaka hayo kwa Mwenyezi Mungu muumba wa mwanadamu, uhai na ulimwengu aliye na haki pekee ya kuongoza wanadamu na kuweletea sheria.  Kwa hakika mwanadamu anahitaji muongozo ambao bila shaka lazima uwe ni wenye kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt). Uongozi huu ni sheria (Quran na Sunnah) hivyo kufaulu au kufeli kunategemea katika kushikamana au kutoshikamana na sheria hizi.

Kwa kufikia kwenye ukombozi halisi kutokana na kasoro na dosari za siasa ya Kidemokrasia inayotokamana na itikadi ya kisekula (kutenganisha Dini na Maisha) ambayo ndio msingi ambao juu yake umejengwa mfumo wa kibepari, jamii nzima wakiwemo wasomi, mufakirina na wanasiasa lazima wafanye kazi ya kufikia kwenye mfumo wa maisha unaotegemea maongozi ya Mwenyezi Mungu ambayo bila shaka hayafanyiwi marekebisho wala kuwa na uongozi wenye sifa ya uchu na tamaa za kibinafsi.

Binadamu anahitaji katiba ifaayo kwani huo ni waraka muhimu unaoainisha sura ya mfumo wa utawala na kuunda mkataba kati ya watawala na wananchi na vile vile kuwa kielelezo cha itikadi na maadili ya watu wanaowaongoza katika nyanja zote za maisha. Uislamu ukiwa kama itikadi toshelezi umethibitisha hitajio kubwa la katiba lakini ukafafanua kwa uwazi kwamba sheria ya Mwenyezi Mungu iliyoteremshwa na Muumba (swt) lazima iwe ndio msingi wa katiba inayoongoza wanadamu. Katiba hii inaweza tu kutekelezwa kwa njia ya Khilafah hali ambayo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu itakuja haraka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyomba vya Habari wa Hizb utTahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu