Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Uwepo wa Kizazi cha ‘Sandwich’, Maisha Duni chini ya Urasilimali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Zaidi ya Waindonesia milioni 50 wa umri wa uzalishaji wamo katika kizazi cha "sandwich". Wako chini ya mzigo wa kiuchumi wa kulazimika kuwasimamia watoto wao na wakati huo huo kusimamia mahitaji ya kizazi kilicho juu yao. Picha ya kizazi cha sandwich cha Indonesia ilinaswa katika kura ya maoni ya Utafiti na Maendeleo ya Kompas mnamo Agosti 9-11, 2022. Matokeo ya kura hiyo yalionyesha kuwa asilimia 67 ya waliohojiwa walidai kubeba mzigo wa kuwa katika kizazi cha sandwich. Ikiwa ni sawia na idadi ya watu wenye umri wa uzalishaji nchini Indonesia, ambayo ni sawa na watu milioni 206, inakadiriwa kuwa kuna watu milioni 56 ambao wanaangukia ndani ya kundi la kizazi cha sandwich. Kwa upande wa umri, kizazi cha sandwich cha Indonesia kimeenea katika vizazi vyote, sehemu kubwa zaidi iko katika kikundi cha kizazi cha Y (umri wa miaka 24-39), ambacho ni asilimia 43.6, ikifuatiwa na kizazi X (miaka 40-55) kwa asilimia 32.6. Kizazi cha sandwich pia kinapatikana kwa asilimia 16.3 miongoni mwa Kizazi Z (chini ya umri wa miaka 24) ambao ni wafanyikazi vijana.

Tantan Hermansah, mwanasosholojia kutoka Chuo Kikuu cha Kiislamu cha Jimbo la Jakarta, alisema mkusanyiko wa shinikizo lililohisiwa na kizazi cha sandwich linaweza kulipuka na kuwa mfadhaiko wa kijamii. Hatima ya kizazi cha sandwich nchini Indonesia, haswa wale walio na mapato ya chini, inatia wasiwasi sana. Wanalazimishwa na dhurufu kufanya kazi ngumu kama mashini - bila kufikia kiwango cha kutosha cha ustawi. Mapato yao yanapungua ili kukidhi mahitaji ya kimsingi ya familia zao na familia kubwa. Hawana nafasi ya kuweka akiba au kuwekeza. Kwa kweli, baadhi yao hawana fedha za burudani ili kukimbia uchovu wa maisha. Wakati huo huo, wanashuhudia maonyesho ya maisha ya kifahari kwenye mitandao ya kijamii ambayo huchochea furaha na starehe. Kwa kawaida, kizazi cha sandwich kiko karibu na jambo la mfadhaiko wa kijamii.

Maoni:

Neno kizazi cha sandwich ni aina ya usemi inayoakisi mfadhaiko wa kijamii kutokana na mkazo wa kiuchumi nchini Indonesia. Hali hii pia inawakilisha kwamba maisha ya kiuchumi yanazidi kuwa magumu huku uvamizi wa maadili ya kiliberali pia ukizidi kuwa mkali katika kushambulia mtindo wa maisha wa jamii ya Kiislamu.

Utekelezaji wa mfumo wa uchumi wa kirasilimali katika nchi nyingi za Kiislamu kwa hakika umezilazimisha familia nyingi za Kiislamu kuzingatia tu mapambano ya kukidhi mahitaji ya kimsingi ya familia zao kutokana na ukosefu wa usawa na umaskini ambao mfumo huu wa kikafiri unaendelea kuudumisha. Ukuzaji wa maadili ya kimada ya kisekula pia umeathiri ubora wa maingiliano wa kijamii na mahusiano katili ya kifamilia na kuwa "ya kibiashara". Kwa mfano, watoto ni uwekezaji, wazazi ni mashini za ATM, au gharama za elimu za watoto lazima 'zirudishwe' pamoja na mapato ya kazi za watoto. Hali ya 'kibiashara' ya maisha ya kirasilimali imetia sumu familia nyingi za Kiislamu pamoja na hali ngumu ya kiuchumi inayozidi kuwa ngumu kutokana na sera za serikali za kiliberali mamboleo kama vile kupanda kwa bei ya mafuta.

Kwa bahati mbaya, wataalamu wengine wa kifedha nchini Indonesia wanasema kuwa sababu zaidi ya kuwepo kizazi cha sandwich ni kufeli kwa kizazi kilichopita katika kupanga usalama endelevu wa kifedha kwa kizazi kijacho. Uchanganuzi wa aina hii huwa na upendeleo na una uwezo wa kusababisha hisia hasi (kulaumiana) kati ya vizazi. Kinyume chake, sababu haiwezi kukomea katika ngazi ya familia, bali ni pana zaidi na ya msingi, kama uwepo wa dola kukidhi mahitaji ya watu.

Sababu za kuwepo kwa kizazi cha Sandwich nchini Indonesia kwa kweli ni mbili, nazo ni (1) mtindo wa utumizi wa kimaisha unaotokana na mfumo wa thamani wa kisekula – fikra ya mada na (2) dori dhaifu ya serikali katika kuhakikisha mahitaji ya kimsingi ya watu wake kutokana na utabikishaji wa mfumo wa uchumi wa kirasilimali. Kwa hakika Qur’ani imetahadharisha juu ya dhiki ya maisha ya watu (maʻīsyat[an] ḍanka) – lau watu watajiepusha na maonyo ya Mwenyezi Mungu, hawatapata furaha, vifua vyao vina dhiki kwa sababu ya upotevu wao.

[وَمَنْ اَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِيْ فَاِنَّ لَهٗ مَعِيْشَةً ضَنْكًا وَّنَحْشُرُهٗ يَوْمَ الْقِيٰمَةِ اَعْمٰى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Surat Tāhā [20]: 124].

Ni wazi kwamba, taabu zinazokikumba kizazi cha leo ni matokeo ya ukoloni wa mamboleo wa kiuchumi unaofanywa na Magharibi, kutokana na uzembe wetu wa kuachana na sheria za Kiislamu katika nyanja zote za maisha. Serikali imezembea katika kukidhi mahitaji msingi ya wananchi na kuipa sekta binafsi zulia jekundu la kuchunga huduma za umma kwa wananchi. Sheria za Kiislamu zinanyanyaswa na wanafurahia zaidi sheria za kinyumbani (za kisekula zilizotungwa na binadamu). Mfumo wa kiuchumi unaegemea juu ya riba. Na mfumo wa kijamii unaiga kakamilifu hadhara ya Kimagharibi iliyojaa dhana ya uhuru wa tamaa.

Wakati ambapo kanuni za siasa uchumi wa Kiislamu zilizofafanuliwa na Shaykh Taqiyuddin an Nabhani zinasisitiza dori muhimu ya dola katika kukidhi mahitaji ya kimsingi ya watu ana kwa ana au mtu kwa mtu. Hazitathminiwi kwa msingi wa mkusanyiko mithili ya nadharia ya kiuchumi wa kirasilimali. Kanuni hii ina athari kubwa ya kijamii. Mahitaji ya kimsingi ya watu ndio ufunguo wa kwanza wa hadhara yenye afya, kiashiria cha maendeleo ya mwanadamu, ambayo itafungua ubora wa vizazi vya hadhara kwa njia endelevu.

Pindi mahitaji msingi yanaponyimwa, yataendelea kuwa na muonekano wa kindani na wa kibinafsi, yasoyoweza kuzingatia matatizo makubwa ya nchi yao, na daima yakiwa katika hali ya mgogoro katika viwango vya chini. Kwa upande mwingine, mahitaji ya kimsingi yanapotimizwa, wanadamu wanaweza kukua na kuimarika na kisha kufungua uwezo wao mwingi wa kifikra na umakini kwa matatizo makubwa ya kimkakati. Watageuzwa kuwa wanadamu wa kipekee kwa mchango wa kazi ya hadhara ili hadhara ya jamii iendelee kuendeshwa kwa heshima na utukufu.

Watabadilika na kuwa kizazi bora cha wanadamu ambao wanaishi maisha mazuri kwa sababu ya utiifu wao kwa Mola wao. Kutakuwa na thawabu kwa wale walioamini na wakatenda mema, yaani maisha ambayo ndani yake hisia ya furaha imejaa ili utulivu na wasaa katika kuishi maisha, bila ya kifua kilichobana na mzigo unaokandamiza.

[مَنْ عَمِلَ صَالِحًا مِّنْ ذَكَرٍ اَوْ اُنْثٰى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهٗ حَيٰوةً طَيِّبَةًۚ وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ اَجْرَهُمْ بِاَحْسَنِ مَا كَانُوْا يَعْمَلُوْنَ]

“Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini,tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda.” [An-Naḥl [16]: 97]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu