Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Zimbabwe Inahitaji Mabadiliko ya Kimsingi Kutokana na Mfumo wa Kibepari na Sio Sarafu Pekee

(Imetafsiriwa)

Habari:

Benki Kuu ya Zimbabwe hivi karibuni imezindua sarafu mpya ya dhahabu inayoitumainia kutokamana nayo itapunguza mahitajio ya pesa za kigeni. Katika uzinduzi rasmi wa sarafu hiyo jijini Harare, John Mangudya, Mkuu wa Benki Kuu ya Akiba nchini Zimbabwe alithibitisha kuwa sarafu hiyo itatumika kupunguza mahitajio ya dolari za Marekani nchini humo.

Maoni:

Zimbabwe ni nchi iliyokoloniwa na kupata uhuru wake wa bendera mwaka 1980. Tangu uvamizi na ukoloni wa Afrika kutoka kwa mabepari wamagharibi wenye kiu ya damu mwishoni mwa karne ya 19, Zimbabwe imekuwa chini ya ushawishi wa Uingereza mpaka leo na hili ni tatizo lake la msingi linalopaswa kutatuliwa, kwa kuondoa kabisa ukoloni mamboleo.

Zimbawe inatabikisha mfumo muovu wa kiuchumi wa kibepari ambao ndio chanzo kikuu cha majanga na mashaka yote ya kiuchumi yanaoikumba. Zaidi ya hapo, sera za uchumi wa kibepari zimepelekea mporomoko wake huku uchumi wake ukisinyaa kwa 6% mwaka 2019 na 10% mwaka 2020.

Kwa mujibu wa Benki ya Maendeleo ya Afrika, mgogoro wa kiuchumi umefanya mfumko wa bei kuwa sehemu ya uchumi wa Zimbabwe, ukipanda na kufikia 222.9% mwaka 2019 na  622.8% mwaka 2020, nakisi ya bajeti iliongezeka kutoka 2.7% mwaka 2019 hadi 2.9% mwaka 2020. Thamani ya ubadilishaji wa fedha za kigeni ilishuka na kuwa ZWL2.5 Februari 2019 na kujaribu kuimarika kwa ZWL82 kwa dolari ya Marekani Disemba 2020. Umasikini ulifikia 70.5% mwaka 2019 huku ukosefu wa ajira ukiendelea kukua kwa 21% .

Kutokana na kufungwa minyororo ya mashirika ya fedha ya kimataifa kama Mfuko wa Fedha wa Kimataifa(IMF), deni jumla la Zimbabwe ni dolari bilioni 11.1 (53.9% ya pato la taifa), ambalo 95.6% ni madeni ya nje, ambayo ni pamoja na dolari bilioni 6.4 nakisi ya marejesho kwa taasisi za fedha za kimataifa, nchi wahisani na wakopeshaji binafsi.

Katika hali hii, umasikini umekuwa ni sehemu ya maisha ya watu wa Zimbabwe kama matokeo ya sababu tulizozitaja hapo awali. Kuzinduliwa kwa sarafu mpya ya dhahabu kunawatia mashaka wataalamu wa masuala ya uchumi na watu wa kawaida nchini Zimbabwe kuhusu ufanisi wake. Prosper Chitambata, Mtafiti Mwandamizi na Mwanauchumi katika Taasisi ya Maendeleo ya Utafiti wa Kazi na Uchumi ya Zimbabwe, alisema: “Hata mahitaji ya dolari ya Marekani yataongezeka…watu wengi hawatakuwa na uwezo wa kununua sarafu hizi kwani watu wengi wanaishi kwa kipato cha kijungu mwiko” Hii ni kwa sababu gharama za sarafu moja ya dhahabu ni $1,800 ambapo kwa mfanyikazi wa kawaida wa serikali anayelipwa $180 hadi $200 kwa mwezi atalazimika kukusanya mishahara yake ya miezi kumi au mwaka mzima ili aweze kununua sarafu moja!

Sarafu ya dhahabu ni sehemu ya pesa za Kiislamu katika mfumo wake wa kiuchumi, kudumisha kiwango cha dhahabu na fedha lilikuwa ni jambo lililokuwepo katika kipindi chote chini ya Khilafah, na kwa hilo uchumi wa ulimwengu ulikuwa imara kwa karne 13. Uislamu pia unakomesha uchumi wa kinyonyaji, unakataza riba, benki za kinyonyaji, masoko ya hisa, ambayo kiujumla mambo kama haya hudhoofisha mfumo halisi wa uchumi katika mzunguko wa fedha.

Kwa muktadha wa Zimbabwe, inatarajiwa kwa kuanzishwa kwa sarafu mpya ya dhahabu hakutabadilisha chochote, kwani sarafu ni kiraka kimoja tu, ilhali mfumo mzima wa uchumi na siasa bado ni wa kibepari ambao ndio unaoendesha na kusimamia mambo ya watu ukitumia ukoloni kama njia ya kunyonya rasilimali za Zimbabwe na kutia umasikini watu na nchi. Kwa hiyo, kama kutakuwa hakuna mabadiliko ya kimfumo, mabadiliko ya sarafu ya dhahabu hayatafanya kazi na kuleta matunda yaliyokusudiwa.

Inachopaswa Zimbabwe kujua ni kuwa, ili viwango vya dhahabu viweze kufanya kazi ipasavyo panahitajika mfumo wa uchumi wa Kiislamu ambao nao pia hauwezi kufanya kazi isipokuwa pale ambapo Uislamu unatekelezwa kama mfumo katika nyanja zote za maisha chini ya serikali ya Kiislamu ya kiulimwengu (Khilafah).

Tunatoa mwito kwa watu wa Zimbabwe na nchi zinazoendelea kiujumla kuwa muda umefika wa kuachana na ubepari uliotuletea majanga yasiyoelezeka kwa wanadamu. Pia tunawakumbusha watu wa Zimbabwe haswa, kuwa Uislamu ndiyo uliyowapelekea ustaarabu katika karne ya 15 kutokea Afrika Mashariki na Msumbiji kupitia biashara na kuoana baina ya Waislamu na watu wa kabila la Shona, hali iliyopelekea kustawi kwa ufalme wa Mutapa na kukuwa kwa miji kama Salisbury (Harare) ikiwa na historia ya muda mrefu na utajiri katika uchimbaji wa dhahabu. Yote haya yalimalizwa baada ya uvamizi na ukoloni wa Kireno na baadaye Uingereza.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Said Bitomwa

Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Tanzania

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu