Njia ya Kujiondolea Dhambi ya Kuwatelekeza Waislamu wa Palestina, ni Kujitahidi Mchana na Usiku Kusimamisha Khilafah Rashida, na Kukusanya Majeshi
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
Kwa vile majeshi ya Waislamu hayakusonga kuinusuru Gaza, baba mwengine aliyedhulumiwa, Abu Umar, aliuawa shahidi, alipokuwa akiwatafutia watoto wake chakula. Alipokuwa akingoja kupokea msaada, risasi ya mdunguaji Myahudi muoga ilipenya kichwa chake. Yule rafiki aliyeuleta mwili wake alikuwa na njaa kwa siku tano, na akarudi kutoka kwenye kizingiti cha mlango wa shahada, labda kuuawa shahidi hivi karibuni. Hili sio tukio moja pekee. Makumi ya matukio kama haya yanashuhudiwa moja kwa moja kila siku, na Umma wa bilioni mbili.