Ijumaa, 20 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/12
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Tukio la Kifedha la Uingereza

“Mnamo Ijumaa asubuhi, Chansela wa Hazina ya Uingereza, Kwasi Kwarteng, aliitwa siku moja kabla kurudi London kutoka Marekani moja kwa moja hadi Downing Street, ambako aliachishwa kazi yake. Hatua hiyo ilikuja wiki tatu baada ya Kwarteng kutangaza bajeti ndogo yenye utata iliyojaa hatua za kupunguza ushuru ambazo hazijafadhiliwa zilizopelekea masoko ya fedha kudorora.

Soma zaidi...

Porojo za Vita Dhidi ya Ugaidi Zinaendelea

Mnamo Jumatatu tarehe 19/09/2022 Tanzania iliungana na nchi nyingine za Afrika katika kutekeleza Itifaki ya Mkataba wa Umoja wa Afrika (AU) wa Kuzuia na Kupambana na Ugaidi. Baada ya kupitishwa azimio la kuridhiwa kwa itifaki hiyo, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni alisema kuwa Tanzania ina nafasi kubwa ya kupata manufaa kadhaa, ikiwa ni pamoja na kuimarisha ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao na kurahisisha ubadilishanaji wa taarifa za kiintelijensia kuhusu ugaidi kupitia ushirikiano wa karibu kutoka kwa nchi wanachama.

Soma zaidi...

Uoanishaji wa Waislamu nchini Denmark Unahusiana na Maadili na Imani, Sio Kazi wala Elimu

Mnamo tarehe 30 Septemba, Wizara ya Uhamiaji na Uoanishaji ya Denmark ilichapisha ripoti ya hali ya kile kinachojulikana kama kipimo cha uoanishaji. Kipimo hicho cha uoanishaji kilichapishwa mnamo 2012, na kinakusudiwa kuonyesha maendeleo katika uoanishaji wa wahamiaji wasio wa Kimagharibi ndani ya malengo kama vile kazi, elimu na lugha.

Soma zaidi...

Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni

Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani.

Soma zaidi...

Jinsi Vita Vilivyoshindwa vya Amerika Dhidi ya ‘‘Ugaidi’’ Vingali Vinawatoa Kafara Watu

Thomas West, Mwakilishi Maalum wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Amerika kwa Afghanistan, katika hotuba yake ya hivi majuzi katika Kituo cha Mafunzo ya Kimkakati na Kimataifa (CSIS) alisema: "Kwa kweli ninaogopa - na nadhani hii ni itifaki - kwamba tunachokiona sasa ni kusimama kidogo katika miaka 44 ya mzozo na kwamba tunaweza kuona kurudi kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe katika wakati wowote”.

Soma zaidi...

Bangladesh Yazidi Kutumbukia ndani ya Mtego wa Indo-Pasifiki Uliotegwa na Marekani Mkoloni Mwenye Kiburi

Ripoti ya hivi punde ya Pentagon ilisema kwamba viongozi wa kijeshi wa Marekani wameanza kufanya maandalizi ya kulinda maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacifiki. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani inafanya mazoezi ya kijeshi na kubadilishana mipango na nchi mbalimbali za eneo la Indo-Pacifiki kwa malengo maalum. Makamanda wa Komandi ya Indo-Pacifiki ya Marekani walisisitiza kuongezeka kwa ushirikiano katika eneo lote.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu