Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Bangladesh Yazidi Kutumbukia ndani ya Mtego wa Indo-Pasifiki Uliotegwa na Marekani Mkoloni Mwenye Kiburi

(Imetafsiriwa)

Habari:

Ripoti ya hivi punde ya Pentagon ilisema kwamba viongozi wa kijeshi wa Marekani wameanza kufanya maandalizi ya kulinda maslahi ya Marekani katika eneo la Indo-Pacifiki. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, Marekani inafanya mazoezi ya kijeshi na kubadilishana mipango na nchi mbalimbali za eneo la Indo-Pacifiki kwa malengo maalum. Makamanda wa Komandi ya Indo-Pacifiki ya Marekani walisisitiza kuongezeka kwa ushirikiano katika eneo lote. Kwa mujibu wa duru za kidiplomasia, Marekani imeonyesha nia ya kuimarisha ushirikiano wa kiulinzi na usalama pamoja na Bangladesh katika miaka ya hivi karibuni. Ushirikiano wa kiusalama pia ulijadiliwa katika mkutano wa Balozi wa Marekani Peter Haas na Waziri Mkuu Sheikh Hasina huko Ganabhan jijini Dhaka mnamo Septemba 13. Kulingana na ripoti hiyo, China inazidi kuwa tishio kwa eneo hilo. Urusi pia ni nguvu kubwa katika eneo la Pasifiki. "Ni wazi, China inataka kuwa nchi pekee yenye nguvu duniani," Jenerali Wilsbach alisema. "Ni wazi kuwa China inataka kulazimisha utashi wake kwa ulimwengu, haswa washirika wake. Na ili kukabiliana na hilo, lengo letu ni Indo-Pacifiki iliyo huru na wazi. (Daily Samakal, Oktoba 3, 2022)

Maoni:

Baada ya kuanguka kwa Uingereza kama dola kuu, ili kuchukua uongozi wa ulimwengu wa sasa wa kisekula, Amerika iliangamiza nchi kama Afghanistan, Pakistan katika eneo hili. Na sasa ili kukabiliana na China na kuchelewesha kuibuka kwa Uislamu katika eneo hilo, kiongozi wa mfumo muovu wa kisekula Amerika inapanga kuzidisha shughuli za kimkakati za Indo-Pacifiki. Inaleta mzozo wa kina wa maslahi yake katika kanda hii. Wakati huu hawafurahishwi tu na kuidhibiti China, wanataka kuileta kwenye mzozo wa moja kwa moja. Wanataka kuikamata China chini ya miguu kama inavyofanya kwa Urusi sasa kupitia vita vya wakala na Ukraine. Ili kufanya hivyo Marekani inashinikiza nchi zaidi katika eneo hilo kufanya kazi kulingana nayo ili kuchochea mzozo katika eneo hilo. Kwa kuwa serikali nyingine nyingi za eneo hili ni za kitumwa kama ile ya Hasina nchini Bangladesh, Marekani inataka kupata kile inachohitaji ili kuzuia ushawishi unaoongezeka wa China kwa jina la ushirikiano au mkataba!

Ulimwengu umeshuhudia mawimbi ya mizozo kati ya dola za kibeberu hadi sasa. Kuanzia umaskini, njaa, msururu wa vita, mauaji ya watu wengi, uhamisho wa watu wengi, na kuvunjika kwa jamii na familia hadi mabadiliko ya tabianchi, tunaona maafa kila mahali yanayoletwa na wakoloni waovu na mfumo wao wa kiulimwengu wa kisekula. Marekani au Uingereza wakoloni wote wanashindana tu ili kuwameza maslahi makubwa. Na hivyo ndivyo ulimwengu wa baada ya ukoloni ulivyofanywa. Uwe ni laini au mgumu, wa kitambo au mamboleo, ukoloni katika miundo yote ni matokeo ya uwepo wa nguvu katika mikono huru ya mwanadamu mwenye ulafi na kiburi visivyoweza kudhibitiwa. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

(اسْتِكْبَارًا فِي الْأَرْضِ وَمَكْرَ السَّيِّئِ وَلَا يَحِيقُ الْمَكْرُ السَّيِّئُ إِلَّا بِأَهْلِهِ)

“Kwa kutakabari kwao katika nchi, na kufanya vitimbi vya uovu. Na vitimbi viovu havimsibu ila mwenyewe aliye vifanya.” [Surah Al-Fatir: 43].

Ni Khilafah Rashida pekee kwa njia ya Utume inayoweza kuwaokoa wanadamu kutokana na njama hii ovu. Inalazimika iwe adilifu kama ilivyoamrishwa na Mwenyezi Mungu (swt). Ulimwengu chini ya kivuli cha Khilafah uliliona hilo katika historia ya wanadamu.

Bangladesh na bara hilo dogo chini ya sheria za Kiislamu ilihisi hilo pia. Na itaweka historia nyingine ya baraka na rehma itakaporudi hivi karibuni bi idhnillah.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Talha Hossain
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu