Jumanne, 24 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh:

Kongamano la Kisiasa “Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?”

Hizb ut Tahrir/Wilayat Bangladesh yaandaa kongamano la kisiasa lenye kichwa:

“Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?”

Baada ya uasi wa Julai 2024 ambao ulimlazimisha dhalimu Hasina kukimbia, Wabangladeshi walitazamia Bangladesh mpya (Bangladesh 2.0). Ili kuzima uasi huo, kambi inayounga mkono Uingereza ilikabidhi mamlaka ya kisiasa kwa serikali ya mpito inayoongozwa na Yunus anayeunga mkono Marekani.

Wananchi walitaka mabadiliko makubwa nchini Bangladesh, lakini Marekani na Uingereza zilikula njama dhidi ya matakwa ya watu kwa kudumisha mfumo wa kikoloni wa Magharibi—mfumo kandamizi wa kirasilimali wa kisekula—kama ulivyo. Chini ya bendera ya mageuzi, walilinda mfumo uliofeli kwa kubadilisha nyuso pekee.

Serikali ya mpito imejiweka kama mlinzi wa uongo wa uasi, ikiwasaliti watu kwa upande mmoja kwa kuendeleza maslahi ya siasa za kijiografia na ya kiuchumi ya Marekani badala ya kuhakikisha usalama wa maisha na mali za watu. Kwa upande mwingine, vyama vya kisiasa vinavyounga mkono Marekani vinashiriki katika mapambano ya kupata mgao wao wa madaraka, kuhujumu sheria na utulivu kupitia mivutano ya kisiasa, unyang'anyi, unyakuzi na ghasia.

Ama wakoloni wa Kimagharibi na polisi wao wa kikanda, India, wao wanaendelea kuingilia siasa zetu mara kwa mara, hususan kwa kuendesha propaganda dhidi ya matakwa ya wananchi ya kuregea kwa mfumo wa Kiislamu na kuregea maisha kamili ya Kiislamu.

Kongamano hili la kisiasa litafichua njama za Marekani, Uingereza, na India dhidi ya matarajio ya watu katika uasi wa Julai 2024 na litajaribu kuelekeza uasi huo kwenye njia yake sahihi—mabadiliko ya kina ya dola.

Hivyo basi kuweni pamoja nasi...

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh

Ijumaa, 27 Rabi' al-Awwal 1447 H sawia na 19 Septemba 2025 M

- Wakati na Mahali -

Kichwa: Bangladesh 2.0: Utegemezi au Ukombozi?

Tarehe: 19 Septemba 2025 M

Wakati: 04:00 Alasiri (kwa saa za Madina Al-Munawwara) / 07:00 Jioni (kwa saa za Bangladesh)

Muda: Saa moja na nusu

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano -

Bonyeza Hapa

- Matangazo ya Moja kwa Moja ya Kongamano katika Tovuti ya Odysee -

Bonyeza Hapa

Kwa Maelezo zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Bangladesh:

Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh

Anwani ya barua pepe hii inalindwa kutokana na spambots. JavaScript lazima iwe itawezeshwa kwa kuweza kuona.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu