Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

[وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُوراً مُّبِيناً]

“Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi.” [An-Nisa 174]

(Imetafsiriwa)

Alama Ishara "#QuranBookClub," imepata umakinifu mkubwa katika Tiktok na maoni milioni 1.9. Ibara hii inayotamba katika Tiktok iliibuka miongoni mwa Waamerika wachanga ambao wanashangazwa na uvumilivu wa watu wa Palestina na wanaigeukia Quran kujaribu kuelewa vizuri zaidi yale yanayotokea huko Gaza na kuonyesha mshikamano na Waislamu wa Palestina. Uso wa ibara hii inayotamba ulikuwa mwanamke wa miaka 34 kutoka Chicago anayeitwa Megan Rice. Alianzisha "Klabu ya Kiulimwengu ya Kitabu cha Dini" juu ya Mizozo na mwishowe akasilimu.

9/11 pia ilisababisha idadi kubwa ya watu wanaonunua Quran na hatimaye kusilimu. Kwa bahati nzuri, kuna wale kati yetu ambao hutafuta majibu halisi wakati wa mitihani na kutoziamini simulizi zilizotabanniwa na Magharibi. Wanaona mbali zaidi ya propaganda na simulizi. Hao ndio watu wale wale ambao huchagua kuingia ndani ya Quran ili kuelewa nia zetu na nguvu zetu wakati wa shida ambayo ni imani ya kina katika Uislamu. Lakini, kazi ya kufichua ukweli ni ngumu inayokutana na mkanganyiko na upinzani.

Kwa watu kama Megan Rice au wanaume na wanawake wengi ambao walimiminika mabarabarani kuonyesha mshikamano na kutafuta majibu, tunastahili kutoa majibu sahihi kutoka kwa Uislamu. Mwenendo wa Kusoma Quran unaotamba kwenye TikTok na maandamano yanayounga mkono Palestina yanaakisi hamu ya kweli miongoni mwa idadi kubwa ya Waamerika wachanga kuungana na Uislamu, inayosukumwa na huruma na kiu kwa ajili ya ukweli, na ufahamu.

Ni dhahiri, Uislamu, pamoja na mfumo wake wa imani na thabiti (Aqida), una uwezo wa kutoa majibu na masuluhisho yanayohitajika mno. Kwa kuongeza, una uwezo wa kuzuia dhulma na ukatili unaofanywa na Magharibi na washirika wake. Jamii za Magharibi zinatafuta wokovu kutokana na unyonyaji wa kibepari, ubaguzi wa rangi, uhalifu, dawa za kulevya, msongo wa mawazo, na watawala mafisadi. Jambo kuu linalokosekana ni muundo mbadala ambao tunaweza kuuashiria kama mfano wa haki wanayoihitaji. Muundo huu mbadala wa maisha, utawala na sheria ni Khilafah. Mfumo huu wa kiwahyi wa Uisilamu unaweza kutoa utulivu na ustawi kwa kutekeleza masuluhisho ya kivitendo yaliyochipuza katika Uislamu kama nuru wazi ya kuondoa giza la mfumo wa sawa wa kiulimwengu.

[يَا أَيُّهَا النَّاسُ قَدْ جَاءكُم بُرْهَانٌ مِّن رَّبِّكُمْ وَأَنزَلْنَا إِلَيْكُمْ نُوراً مُّبِيناً]

“Enyi watu! Umekufikieni ushahidi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Na tumekuteremshieni Nuru iliyo wazi.” [An-Nisa 174]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Haitham Ibn Thbait
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut Tahrir Amerika

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu