- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Joyland: Kukanusha Sababu Saba Zilizojadiliwa Zaidi zenye Kupendelea Kuonyeshwa Filamu Hii
(Imetafsiriwa)
Miongoni mwa mabishano mengine mengi, ubishani mpya umeikumba nchi yetu kuhusu filamu ijayo, ya Joyland[1] na marufuku yake inayobishaniwa[2]. Filamu hiyo, kabla ya kutolewa rasmi, tayari imeshinda tuzo 4 kuu, miongoni mwazo tuzo ya 'heshima' ya Tamasha la Filamu la Cannes katika vigawanyo viwili, miongoni mwao ni kigawanyo cha Queer Palm kilichotolewa kwa maudhui husika ya LGBT[3] na tuzo ya jury iliyosifiwa sana[4]. Filamu hiyo pia ni kiingilio rasmi cha Pakistan kwa Tuzo za Oscar [5]. Inajivunia Malala Yousafzai, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel kama mtayarishaji wake mkuu [6] na mtengenezaji wa filamu wa India Apoorva Guru Charan anayeishi Marekani kama mtayarishaji wake mkuu, ambaye anadai kwa fahari "Nadhani hii ni filamu ya kwanza ya Pakistan ambayo ina ufadhili wa Amerika yote”[7]. Wale wanaounga mkono kuonyeshwa kwa filamu hiyo wanahoji kuwa inatokana na uhalisia wa jamii yetu na kwa hivyo hatupaswi kukwepa kuiwasilisha. Wale wanaopinga upeperushwaji wake wanakimbilia kwenye hoja kwamba itaeneza maovu katika jamii kwani ingawa inasawiri uhalisia, uhalisia wenyewe ni jambo ambalo haliruhusiwi Kiislamu na halikubaliki kijamii.
Katikati ya mjadala kwa kweli kuna swali la msingi zaidi, je watu wanapaswa kuwa huru kutoa rai na maoni yao bila kujali matokeo ya kijamii. La msingi zaidi, ni je kuna jamii yoyote inayoruhusu mazungumzo kama hayo yasiyo na kikomo kama, kwa jina la uhuru wa kujieleza, au hiyo ni hekaya tu ambayo jamii na serikali za kiliberali za kisekula zinataka wengine kuamini? Kwa kweli, jamii zote, ziwe za kitamaduni au za kiliberali zina mistari yao mekundu, hata hivyo, jamii hizi zimeweza kutoa hisia kwamba ziko huru kabisa linapokuja suala la kusema na kujieleza. Kukanusha hekaya hii sio vigumu sana wakati mtu anapozingatia istilahi tofauti tofauti ambazo jamii huria zimezianzisha ili kuzuia uhuru wa kujieleza. 'Habari za uwongo', 'kashfa', ‘uasi’ 'uchochezi', 'habari potofu', 'matamshi ya chuki[8]', 'kuchunguza ukweli[9]', 'upendeleo wa uchapishaji[10] 'kughairi utamaduni[11]' , 'ususiaji majukwaani[12]', 'uchunguzaji wa nukuu katika twitter[13]', na neno rasmi na la kisheria zaidi 'uchunguzi wa uwiano wa kesi[14]' zote ni aina na zana tofauti za kuzuia uhuru wa kujieleza. Kuna tani ya ushahidi ambao hata jamii huria zaidi zinaweka vikwazo vya kiubaguzi linapokuja suala la uhuru wa kujieleza.
Ni upi basi uhalali wa kimaadili wa watu wenye mawazo huria katika kupinga kupigwa marufuku kwa sinema ambayo imejaa maudhui machafu? Inaonyesha uhusiano wa nje ya ndoa katika mazingira ya watu wa jinsia moja, yote katika hali ya kuleta masaibu ya waliobadili jinsia mbele. Je, hakuna njia nzuri ya kuibua ufahamu kuhusu mateso ya jamii ya watu wa jinsia tofauti? Sasa kwa kuwa upepo wa hoja za uhuru wa kujieleza unaopepea umetolewa, tuendelee na hoja zengine zinazoletwa kwa ajili ya kuchuja maudhui hayo yasiyopatanika.
1. Watu hujifunza masomo muhimu: Mojawapo ya hoja kubwa zaidi ni kwamba sinema na drama huelimisha watu. Ingawa hii inaweza kuwa kweli kwa kiasi fulani, kwa uaminifu wote, je, hii ndio njia mwafaka na inayodhibitiwa ya kuelimisha watu wengi? Je, tunaweza kutathmini uharibifu utakaoleta kupitia kuchafua mamilioni ya akili zisizo na hatia ambao kamwe hawangewahi kufikiria kuhusu vitendo kama hivyo na sasa huenda wakawazia kuvihusu? Je, sisi kama jamii bado tunapambana na athari mbaya za filamu kwenye mfumo wa familia zetu?[15]
2. Vyombo vya habari pia huripoti matukio kama hayo au hata mabaya zaidi: Magazeti huripoti matukio lakini zaidi bila kuambatanisha hisia kwayo. Isitoshe, matukio kama haya yanaripotiwa zaidi katika habari kwa mtazamo sawa na jinsi jamii inavyoyaona. Kwa hivyo hadi sasa, mahusiano ya nje ya ndoa hayajaripotiwa kwa mtazamo chanya, isipokuwa kwa kuyaonyesha katika sinema na filamu. Hii pia inaonyesha jinsi vyombo vya habari mbali na chaneli za habari vinavyofanya kazi katika kubadilisha maadili na kujenga mazingira ya kukubalika kwa vitendo na dhana ambazo hazikubaliki.
3. Una uhuru wa kutotazama: Hoja hii kwa hakika imegusiwa katika sababu zilizotolewa hapo juu za kupiga marufuku maudhui kama hayo hapo awali. Ingawa tuko huru katika kiwango cha mtu binafsi kutotazama maudhui kama haya ikiwa hatupendi au hatukubaliani nayo, ni sharti la kimaadili kwetu kuwazuia wengine kueneza fahamu ambazo Uislamu unaziona kuwa potovu na zenye kuadhibiwa.
4. Kwa nini Uislamu unahatarishwa tu na sinema? Kwa mara nyengine tena, hili pia limegusiwa katika mjadala hapo juu. Kwa hakika si tishio kwa Uislamu, bali inahatarisha Waislamu na jamii kwa jumla, kwa kueneza uchafu na kujenga kukubalika kwa tabia hiyo chafu na haramu. Zaidi ya hayo, hata kama hakukuwa na hatari, ni suala la maadili. Kama mlinganisho, je, nchi za kiliberali za kisekula (nchi 36 [16] haswa) ambazo zimepiga marufuku uonyeshaji hadharani wa nembo za Nazi na/au kukataa mauaji ya kimbari zinahisi kutishiwa na nembo za mita? Je, hizo zinaleta tishio kubwa kwa uliberali au ni suala la kimaadili?
5. Mtazamo bora zaidi ndio utakaotawala: Wengine wanaweza kubisha kwamba sinema ni jukwaa linalofaa la kupigana na tofauti za kifikra. Kwa hivyo ikiwa mahusiano ya nje ya ndoa na jinsia ya tatu yanapaswa kukuzwa au la ni kwa hadhira kuamua. Ikiwa hii ingekuwa hoja nzuri kusingekuwa na haja ya kuzuia kauli za wale ambao wanatetea uhuru wake kwa nguvu. Walakini, wao ndio wakali zaidi katika kuizuia kimfumo. Kwa nini? Maana hata wao wanaelewa kuwa mawazo yanayovuka mstari fulani hayapaswi kuruhusiwa kukuzwa. Uislamu ni msafi kutokana na unafiki kama huo kwanza kabisa kwani kamwe hautetei uhuru wa kuzungumza ila tu kuuzuia baadaye. Kuhusu kujadili maswala haya, ndio kunapaswa kuwe na mijadala kama hii lakini sinema sio jukwaa sahihi kwa hili kwani mvuto wake ni wa mihemko kuliko akili. Zaidi ya hayo, watazamaji wasio na taarifa wa filamu hawaonyeshwi pande zote mbili za sarafu, mara nyingi huwaacha wakipendelea ajenda ya mtengenezaji wa filamu.
6. Kuna ubaya gani kutetea haki za LGBTQI? Labda hii ndiyo hoja inayovutia zaidi kwani inahusisha huruma. Ingawa masaibu ya jumuiya ya watu wa jinsia tofauti ni jambo lisilopingika, tunahitaji kuelewa jinsi Uislamu unavyoliona na kulishughulikia suala hili. Uislamu unatofautisha watu waliobadili jinsia na watu wa jinsia tofauti. Mambo matatu tofauti ya kuelewa ni kitambulisho cha kijinsia, kujieleza kijinsia, na jinsia ya kibayolojia. Kitambulisho cha kijinsia kinaregelea hisia ya ndani ya mtu kuwa mwanaume, mwanamke au kitu kingine; kujieleza kijinsia huregelea jinsi mtu huwasilisha kitambulisho cha kijinsia kwa wengine kupitia tabia, mavazi, mitindo ya nywele, n.k. Jinsia ya kibayolojia inaregelea hali ya mtu kama mwanamke, mwanamume, au jinsia tofauti kulingana na kromosomu zao, viungo vya uzazi na sifa nyingine. Kulingana na dalili wazi za Shariah, vigawanyo viwili vya kwanza, ambapo mtazamo wa mtu [17] au kujieleza [18] ni kinyume na jinsia yao ya kibayolojia, haikubaliki kabisa na umeharamishwa katika Uislamu. Sisi wanadamu hatuko huru kuchagua jinsia yetu kulingana na kile tunachohisi au kupenda, badala yake hili ni jambo linaloamuliwa kwa msingi wa ukweli wa kibaolojia. Kwa vyovyote vile, ikiwa kitambulisho cha kijinsia au kujieleza kijinsia hailingani na jinsia ya kibayolojia, hizi huitwa jike dume (mutarajallah) na dume jike (mukhanas). Kwa zile kesi ambazo ni nadra ambapo jinsia ya kibayolojia haieleweki, kwa ujumla inajulikana kama khuntha, wanapewa jinsia, ama ya kiume au ya kike, kwa usaidizi wa wataalamu. Pia husaidiwa na taratibu za upasuaji ikiwa inahitajika. Vile vile, mwelekeo pekee wa kingono unaokubalika ni kati ya jinsia tofauti, hilo ni wazi tu ndani ya mipaka ya Nikah. Sasa kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, hakuwezi kuwa na jinsia ya tatu na jinsia si kitu cha kunyumbuka kinachoweza kuvuka mipaka ya uhalisia wako wa kibaolojia, kwa hiyo watu waliobadili jinsia, yaani wale ambao hawazingatii jinsia zao za kibaolojia, wanaonekana kama mashoga na Uislamu wanapo dhihirisha kujamiiana na jinsia tofauti kulingana na kitambulisho chao wanachokihisi. Hivyo basi, maudhui ya sinema hii yana sifa ya ushoga pia na kwa hivyo hata ni machafu zaidi na ya kuchukiza kutoka kwa mtazamo wa Kiislamu na kitamaduni.
7. Lakini bodi ya kuhakiki imeipitisha! Hoja nyingine dhaifu lakini ya kawaida ni kwamba mara tu filamu inapopata maoni safi kutoka kwa bodi ya kuhakiki, hatupaswi kuwa na pingamizi yoyote. Hoja hii inapaswa kubadilishwa na kuulizwa bodi ya uhakiki ina uhalali gani ikiwa inapitisha filamu ya aina hiyo katika nchi yetu? Au tukienda mbali zaidi, vipi kuhusu sinema na filamu zote ambazo zimejaa ghasia, uasherati, na kila aina nyingine ya maovu ambayo wanadamu wanaweza kuyafikiria, kwa jina la kuakisi jamii? Bodi Kuu ya Wachunguzi wa Filamu, iliyoanzishwa chini ya Sheria ya Picha za Video, 1979 [19] inasema kwa uwazi kama "Kanuni zake za kwanza za mwongozo katika kupasisha filamu" kwamba "Filamu haitaidhinishwa kwa maonyesho ya umma ikiwa, kwa maoni ya Bodi, filamu hiyo au sehemu yake yoyote inaathiri utukufu wa Uislamu au heshima, usalama au ulinzi wa Pakistan au sehemu yake yoyote, mahusiano wa kirafiki na nchi za nje, utulivu wa umma, adabu au maadili au kupelekea kufanywa, au kuchocheza, uhalifu.” Inapaswa kuwa wazi kwamba ndani ya demokrasia ya kisekula mithili yetu, sheria kama hizo ni domo tupu mbele ya ajenda kubwa yenye nguvu ya kimagharibi ambayo ni nadra kukosa ufadhili.
Mwishowe, ndio tunaelewa kuwa hatuwezi kuweka kikomo cha taarifa ya kila aina na kwa hivyo njia ya kwanza kabisa ya kujihami inabaki kuwa maadili, vima, na imani ya mtu mwenyewe, hata hivyo, hii haiwezi kuwa sababu ya kueneza maudhui machafu kama haya bila kuzuiliwa katika jamii. Pamoja na ahkam za kujikinga sisi wenyewe na watoto wetu kutokana na moto wa jahanamu[20], ahkam za kukataza maovu (nahi anil munkar)[21] pia ziko imara sana na haziwezi kukanushwa. Hii inadhihirisha umuhimu na baadhi ya changamoto za malezi.
Kwa kuhitimisha, ni lazima ifahamike kwamba hisia zinazozunguka suala hili zimedhihirika wazi miongoni mwa jamii kwa jumla ambapo isipokuwa watu wachache wa kisasa miongoni mwetu, watu wanachukizwa zaidi na mada ya filamu inayohusu uasi wa kingono na ushoga. Kwa hivyo, tunaona upinzani wa umma kuhusu suala hili hata hivyo masuala mengine mengi muhimu hukwepa uchunguzi kama huo wa umma. Kwa mfano, kwa nini licha ya kuitwa jamhuri ya Kiislamu, kila aina ya ukiukaji wa Quran na Sunnah unafanyika chini ya usimamizi wa vyombo mbalimbali vya kiserikali, iwe ni riba iliyoenea, kuingiliwa na nchi za kigeni, utozaji ushuru wa dhulma, uasherati au maovu mengine mengi kama haya? Mwenyezi Mungu (swt) atuepushe na maovu yote na atuwezeshe kutimiza wajibu wetu kama wazazi na wanajamii.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Abdul Baseer – Wilayah Pakistan
[1]https://www.imdb.com/title/tt19719976/
[2]https://www.aljazeera.com/news/2022/11/17/pakistan-lifts-ban-on-joyland-film-about-transgender-love-affair
[3]https://en.wikipedia.org/wiki/Queer_Palm
[4]https://www.indiewire.com/2022/05/cannes-un-certain-regard-winners-2022-1234729113/
[5]https://www.hindustantimes.com/entertainment/others/pakistan-lifts-ban-on-official-oscar-entry-joyland-film-may-release-on-friday-101668616312631.html
[6]https://tribune.com.pk/story/2380414/malala-joins-joyland-as-executive-producer
[7]https://variety.com/2022/film/news/joyland-pakistan-transgender-cannes-1235273919/
[8]https://www.un.org/en/hate-speech/understanding-hate-speech/what-is-hate-speech
[9]https://en.wikipedia.org/wiki/Fact-checking
[10]https://www.bmj.com/rapid-response/2011/10/31/what-publication-bias
[11]https://en.wikipedia.org/wiki/Cancel_culture
[12]https://blogs.lse.ac.uk/humanrights/2021/05/18/do-no-platform-policies-violate-freedom-of-expression/
[13]https://www.theguardian.com/technology/2021/jan/25/twitter-birdwatch-misinformation-donald-trump-election
[14]https://link.springer.com/article/10.1007/s12142-020-00608-8
[15]http://al-milal.org/journal/index.php/almilal/article/view/162
[16]https://en.wikipedia.org/wiki/Bans_on_Nazi_symbols
[17] Mtume (ﷺ) amewalaani madume jike (wanaume wanaojifananisha na wanawake) na wale wanawake wanaojifananisha na wanaume, na akasema: “Watoeni katika nyumba zenu.” (Sahih al-Bukhari)
[18] Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ) amewalaani wanaume wanaojifananisha (wanaochukua tabia) na wanawake na wale wanawake wanaojifananisha (wanaochukua tabia) na wanaume. (Sahih al-Bukhari)
[19]http://punjablaws.gov.pk/laws/1517a.html
[20] “Enyi mlio amini! Jilindeni nafsi zenu na ahali zenu na Moto ambao kuni zake ni watu na mawe…” (Surah At-Tahrim: 6)
[21] “Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.” (Surah Aal Imran:110)