Alhamisi, 23 Rajab 1446 | 2025/01/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Athari Pana, Hatari za Usalama za Msukosuko wa Kisiasa wa Pakistan

(Imetafsiriwa)

Msukosuko wa sasa wa kisiasa nchini Pakistan kimsingi haukufungika kwenye mzozo kati ya PTI ya Imran Khan na serikali ya PDM. Haijafungika hata kwenye mvutano kati ya vikundi vya jeshi lenye nguvu. Msukosuko wa kisiasa una athari pana zaidi. Inapanuka ili kuwezesha malengo na maslahi ya Marekani katika eneo hili, kwa wakati huu. Hii ni bila kujali kama uwezeshaji huu ni wa kubuniwa kimakusudi, au kwa matokeo ya bahati mbaya, ya kusikitisha.

Marekani inataka kuitangaza India kama mchezaji mkuu wa kieneo, ili iweze kuitumia India dhidi ya China na Waislamu. Wakati Marekani inaisaidia India kidiplomasia, kiuchumi na kijeshi ili kukuuza hadhi yake ya kikanda, India haiwezi kupata dori kubwa, isipokuwa Pakistan inyimwe ushawishi wake ulioenea katika eneo hilo. Ni lazima kuipunguza Pakistan, ili kutoa nafasi muhimu kwa India, kuchukua dori kubwa ya kikanda.

Zaidi ya hayo, India haiwezi kupangwa dhidi ya China, isipokuwa iwe na hakikisho kwamba Pakistan haitaingilia kati, na kuanzisha mzozo na India, wakati wowote ule. Hii inahitaji kuweka pembeni uwezo wa Pakistan wa kupambana na kuichokoza India. Hili nalo linahitaji kupunguza uwezo wa jeshi la Pakistan, kupambana na kubughudhi matarajio ya kikanda ya Modi.

Kwa hivyo, ni muhimu kwa Washington kutoa nafasi kwa ajili ya mapambano ambayo yanaiingiza Pakistan katika mzozo haribifu wa ndani, unaohujumu fahari na hadhi ya majeshi. Zaidi ya hayo, kuyahusisha majeshi katika masuala na mizozo midogo midogo ya ndani, ili yasiweze kuzingatia kuchukua hatua zozote za nje, ni muhimu kwa malengo ya Marekani. Hii ni huku uongozi wa kijeshi ukichukua msimamo wa upande mmoja wa kujizuia kwa ajili ya amani wa kikanda, katika hali ya uchokozi unaoongezeka wa India. Haya yote yanaandamana na juhudi za uongozi wa kijeshi kushawishi safu na faili yake kwamba haiwezi kupambana na nguvu inayokua ya jeshi la India.

Ingawa msukumo huu wa kujisalimisha mbele ya India unaendelea kwa miaka michache sasa, hali ya sasa ya kisiasa imeupeleka kwenye ngazi nyingine. Zaidi ya hayo, iwe tishio la usalama linaloongezeka ni la kubuni, au la matokeo, ya msukosuko wa kisiasa uliopo sasa, inaonyesha kufeli kwa uongozi wa kijeshi, ambao ndio mamlaka halisi nchini. Inasikitisha kwamba unaendeleza desturi ambayo inajulikana vyema kuwa mkuu mpya wa jeshi huteuliwa kwa idhini ya Washington, na hivyo kulidunisha vibaya jeshi la Pakistan hadi kuwa ni tawi la USCENTCOM.

Uongozi wa kijeshi umefeli kwa sababu haujautabanni Uislamu kama msingi wa mwenendo hatua zake. Lau kama ingefanya hivyo, meza zingegeuzwa dhidi ya New Delhi na Washington, kwa athari ya haraka. Uislamu unawajibisha Nusrah (kutafuta usaidizi) kwa ajili ya kusimamisha Uislamu kama njia ya utawala, kutokomeza chombo cha kikoloni, Demokrasia. Uislamu kwa upande wake unaamuru kukata mafungamano yoyote na mataifa adui ya kigeni, na kukomesha unyonyaji wa kigeni wa kijeshi na uchumi wa Pakistan. Uislamu unaamuru kuunganishwa kwa Ardhi za Kiislamu ili kuupa Umma tamkini, katika kuwakabili na kuwashinda maadui zake. Na Uislamu unaamuru uhamasishaji wa nguvu za serikali ili kukomboa Ardhi za Waislamu, ikiwemo Kashmir Iliyokaliwa kimabavu, na kuwapeleka maadui katika mtafaruku. Hatua hizo za kijasiri kamwe hazitafanyika wakati uongozi wa kijeshi unaunga mkono Demokrasia na mfumo wa sasa wa kilimwengu wa wakoloni.

Hakika, njia pekee ya kutoka katika mgogoro wa sasa ni kwa uongozi wa kijeshi kutoa Nusrah kwa Hizb ut Tahrir. Ikiwa haitafanya hivyo, ni kwa hatari yake yenyewe na hatari ya nchi ambayo imeapa kuilinda. Na juu ya yote, inawaweka walioghafilika katika hatari ya kualika adhabu kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَابْتَغُواْ إِلَيهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُواْ فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)

“Enyi mlio amini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka.” [Surah Al-Maida 5: 35]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Tariq – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu