Jumatatu, 21 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mfumo wa Elimu Huunda Fikra Zetu

Elimu ni kusudio msingi la jamii yetu hivi leo. Ni moja ya Malengo muhimu ya Maendeleo Endelevu ya Umoja wa Mataifa, kufikiwa kwake ni shabaha ya takriban kila mtu duniani kote. Hivi sasa, mkazo wa mfumo wa elimu umehusishwa na takwimu – shule ina wanafunzi wangapi? Wanaipata kwa masafa gani? Kuna uwiano gani baina ya wanafunzi wa kike na kiume shuleni?

Shabaha kuu ya dola ni juu ya kujua kusoma na kuandika na tukiwa kama raia, lengo letu kubwa ni kufikia kiwango cha elimu ambacho kitatuwezesha kusonga mbele duniani – na sio fikra zinazoenezwa wakati wanafunzi wakipokea elimu hii. Kunaweza kuwepo na hoja kuwa mabadiliko haya – ya namna ya mfumo wa elimu unavyo chukuliwa kuwa ni ghali mno lakini suala msingi ni hili, kwamba: Mfumo wa Elimu hukuuza fikra maalum kwetu.

Fikra hizi ziliingizwa ndani ya mfumo wa elimu kwa lengo – ili kuwadhoofisha vijana na vizazi mtawalia vya watu kote duniani, na kutilia nguvu mshiko ambao nchi zinazojulikana kama zenye Uchumi Ulioendelea, zilionao juu yetu.

“Nimesafiri India yote kwa marefu na mapana na sikumuona muombaji ambaye ni mwizi, utajiri kiasi hiki ambao niliuona katika nchi hii, kiwango bora cha maadili, watu wa kiwango hicho bora, ambacho sifikirii kama tutaweza kuishinda nchi hii, hadi tuvunje uti wa mgongo wa taifa hili, ambao ni urithi wake wa kiroho na kithaqafa na hivyo basi, napendekeza kuwa tubadilishe mfumo wake wa elimu wa zamani ulio mkongwe, thaqafa yake…” Tamko la Lord Macaulay kwenye Bunge la Uingereza (2 Februari 1835)

Hili wazo la kuziathiri fikra zetu na matendo yetu kupitia mfumo wa elimu sio kitu kisichotarajiwa. Bali ni jambo ambalo tunahitajia kulitambua. Tunaweza kwenda nyuma wakati mfumo wa elimu ulivyowatayarisha watu kwenye kazi zilizopangwa za viwandani, iliofananishwa na kauli ya Rockefeller ‘Ninataka taifa la wafanyakazi, sio wanafikra’, hadi katika mazingira ambapo shabaha juu ya haja kwa wanafunzi kujenga fikra zao za kukosoa na za kibinafsi.

Hata hivyo, hiyo haina maana kuwa tuko huru kutokana na maadili ya kirasilimali - mfumo wa elimu ambao unaendeleza fikra ya umakinifu hautugeuzi moja kwa moja kuwa wenye fikra huru - kwa kuwa tunafundishwa kuchambua, kutathmini na kufikiri ndani ya mipaka ya fikra ya Uhuru.

Ili kuwachanganya vijana, wanataaluma mafisadi wanajitahidi kuwashawishi wanafunzi kwamba hawafungamanishwi na fikra nyengine zozote - fikra ya uhuru, dini, uadilifu wa kijamii, uchumi na masuala mengine mbali mbali kuwa ni ya wao wenyewe, na kwa namna hiyo wayafuate kwa uaminifu wote. Lakini hilo liko mbali na ukweli - wanatufinyanga kuwa watu ambao huenda bila kujijua hufanya kazi ndani yake, na kuunga mkono mfumo. Sisi bila kujua tunazichukua fikra zinazogongana na za Kiislamu na hivyo kujenga shakhsia iliopotoka.

Kile kilicho muhimu kukielewa ni kuwa fikra wakati wote huwepo, na mfumo wa elimu muda wote utazijenga ndani yetu. Lakini kama Waislamu tuna chaguo, kuuelewa Uislamu kuwa ni kitu ambacho tunakiamini kuwa ni haki na kukubali fikra za Kiislam kuwa ni msingi wa fikra na shakhsia zetu.

Hii haimaanishi kuwa tuwe nyuma – bali kinyume chake, fikra ya Uislam imetupelekea kwenye maendeleo. Katika kipindi cha nyuma imetutolea watu walionawiri chini ya mfumo huu. Dola ya Kiislam ilikuwa ikistawi katika kila nyanja, wakati Ulaya ikiwa imezama katika zama za kiza. Mifano kwenye hili ni mingi, kutokea kwenye utambuzi wa vipimo vya elimu ya sayari, hadi kwenye uundaji wa kitabu cha mwanzo cha ufafanuzi wa elimu ya upasuaji. Kama Waislam, tunahitaji kuishi kwenye jamii ambapo fikra na mawazo tunazoamini kuwa za kweli zinacheza dori kubwa katika jamii – mafanikio huja kama matokeo ya hili.

Tunahitaji kutambua kuwa kuna hitajio la wazi la kusimamisha tena Dola ya Kiislam, kupitia njia ya Mtume (saw). Hadi hapo itapokuwepo Dola ya Kiislam na mfumo wa elimu kujenga fikra za Kiislam miongoni mwetu, na kutuwezesha kuendelea na kutekeleza fikra hizo kwa kiwango cha juu, tutabaki kuwa dhaifu. Tutabaki siku zote kuwa watumwa. Ili kubadilisha haya, tunahitajika kusimamisha dola ya Kiislam, na kusoma chini ya mfumo wa Elimu ya Kiislamu.

Mwenyezi Mungu (swt) anasema:

    (يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَابْتَغُواْ إِلَيهِ الْوَسِيلَةَ وَجَاهِدُواْ فِي سَبِيلِهِ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ)

“Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na tafuteni njia ya kumfikilia. Na wanieni kwa juhudi kwa ajili yake ili mpate kuokoka.” [Al-Maida: 35].

(أُوْلَـئِكَ عَلَى هُدًى مِّن رَّبِّهِمْ وَأُوْلَـئِكَ هُمُ الْمُفْلِحُونَ)

“Hao wapo juu ya uongofu utokao kwa Mola wao Mlezi, na hao ndio waliofanikiwa.” [Al-Baqara: 5]

أقيموا_الخلافة#
#ReturnTheKhilafah
#YenidenHilafet
خلافت_کو_قائم_کرو#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Fatima Musab

Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu