Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uharibifu Mkubwa dhidi ya Familia (Sehemu ya 2):
Uhuru Unapunguza Idadi ya Familia

Maana ya uharibifu katika makala hii ni fujo na machafuko yanayo athiri mamilioni ya familia kutoka Magharibi kuelekea Mashariki na limekuwa janga la kibinadamu ambalo limesababishwa pakubwa na msukumo wa harakati za kuwawezesha wanawake. Katika hali yake ya usasa, ukombozi wa wanawake ukioanishwa na nidhamu ya kiuchumi ya kisekula, ambayo kumezaliwa zama mpya zenye uharibifu wa umama. Sehemu ya kwanza ya makala hii ili tathmini moja ya sababu ya uharibifu huu nao ni uhamiaji wa ukombozi wa wanawake unaosukumwa na nidhamu ya kiuchumi ya kisekula inayopatiliza kina mama, hivyo basi imekuwa na dori ya moja kwa moja katika kuwatelekeza mamilioni ya watoto. 

Hivi sasa katika sehemu ya pili tutatathmini namna uhuru, ukiwa ni moja ya misingi muhimu ya usekula urasilimali namna ulivyo sababisha idadi ya familia kupungua na hata kupelekea katika kuhatarisha mujtama kutokana na sera ya "wanawake na uchumi". 

“Kifo cha Familia" ndani ya Ulimwengu wa Kisekula wa Viwanda

'Kifo cha familia' kinaangaziwa na janga la ukosefu wa uzazi ndani ya Japan. Linasababisha madhila ya kiuchumi na kijamii ambayo hayajawahi kuonekana kama ilivyoelezewa na Mary Brinto, mwanasosholojia wa Harvard kwa Business Insider mwaka jana. Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) nalo pia lilionya nchi nyingine za Asia ziwe macho zisifuate mkondo wa Japan wa "kuwa mtu mzima kabla kuwa tajiri." Mnamo 2016 ripoti ya UBS ilionyesha kubadilika kwa mitazamo kuelekea ufanyajikazi na dori za kijinsia kuwa kutapelekea mataifa ya viwanda ikijumuisha Amerika kupata uzito sawa na wa kiuchumi. Hofu ya jamii za kiuchumi nyingi ni mwenendo wa idadi ya watu unaodhihirika duniani utapelekea mataifa mengi yenye uchumi mkubwa kutaabika kama inavyotaabika Japan. Kwa maana nyingine watu wanawasiwasi kwamba uchumi wa dunia utabadilika kuwa kama wa Wajapani. 

Sera ya kirasilimali ya "wanawake na uchumi" ndani ya Japan, ambayo ni mazao ya uchumi wa uhuru unawalazimisha wanawake kufanyakazi lakini kila wanawake wengi walipokuwa wafanyikazi nao uzazi ukaanza kushuka. Leo, uzazi wa Japan uko kwa kiwango cha 1.41. Natija yake ni kwamba idadi ya watu inapungua ilhali unyama wa kufanyakazi masaa mengi unaendelea. Kwa zaidi ya miongo miwili, hadithi kuhusiana na wanandoa wachanga Wajapani walikuwa wakipigana ili kufaulisha mahusiano yao ndani ya tamaduni ya ufanyajikazi unaowatarajia wanaume kuwa ndio wachumaji na wanawake ndio wasimamizi wa nyumba wakiwasilishwa kuwa ni vita ambavyo haviwezi kufaulu. Bali wanandoa wengi wanalazimishwa kutizama muda wao ukipotea na wakisalimisha kila kitu kutoka siku ya usiku wa kukutana ili kuanza familia. Wakati huo huo, wanawake wengi wanatizama kuajiriwa kuwa ni kuwapa cheo cha juu kuliko umama, na kuwapelekea wengi kupoteza nishati ya kuwa wake na kupata watoto wengi. 

Janga la uzazi pia limeikumba Korea Kusini. Utafiti wa Baraza la Huduma za Utafiti la Kitaifa (NARS) ndani ya Seoul mnamo Agosti 2015 lilipendekeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa Korea Kusini kupotea kutokana na kupungua kwa idadi ya kuzaana na kuwa chini ya 1.19 kwa kila mwanamke mnamo 2013. Ili kujibu hilo, jarida la The Diplomat lilielezea kuwepo kwa tishio kubwa la idadi ya watu kwa maana ya Kupotea kutalikumba eneo hilo na sio tu Korea Kusini na Japani. Taiwan na Singapore nazo pia zinapambana kugharamikia kifedha idadi kubwa ya watu wazee kutokana na kupungua kwa watu jumla. Ni kinaya na kituko kwamba nchi ambazo zinatajwa kuwa ndio "Maajabu ya Asia Mashariki" kutokana na kufaulu kwao katika kubadilisha na kuwa eneo lenye uchumi mkubwa sasa hivi yanakodolea hatari ya vizazi vyao kuangamia kama taifa.

Takribani sawia na majirani zake ndivyo hali ilivyo ndani ya Uchina. Gazeti la The People's Daily liliripoti mnamo Disemba 2016 kwamba Uchina ya viwanda nayo pia kwa haraka inakaribia kuwa nchi ya makapera na wari kwa kuwa idadi ya watu wake ambao hawajaoana inakaribia milioni 200. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na Tencent mnamo 2016, asilimia 36.8 ya wanawake Wachina ambao hawajaolewa wanaamini kuwa ndoa sio jambo la msingi ukitaka kuishi maisha ya furaha. Wafuatiliaji wa idadi za watu wanaamini kwamba uhuru wa wanawake Wachina wa sasa ni moja ya sababu ya kuwepo kwa idadi ya watu ambao hawaoani. Uchina – ndio nchi yenye watu wengi duniani – nayo pia itapungua watu kama inavyowafuata wakuu wake Wamagharibi kama ilivyo pia ndani ya Mashariki, Japan na Korea Kusini. Idadi kubwa ya wanawake ambao hawajaolewa nayo pia itafuatiwa na kupungua kwa idadi ya kuzaana ambayo hatimaye itapelekea idadi ndogo. Haya yanatokea katika kila nchi ya kirasilimali ambayo imepanuka kiuchumi. Wanawake wanapoweka kipaombele ni kufaulu kimadaniya na hawazingatii kujenga familia, hawakiamini kiapo cha ndoa na hata kuwatizama watoto kuwa ni mzigo wa kiuchumi basi hili kiukweli ni dalili ya mwanzo ya kufariki kwa taifa ambalo linaendelea kuzeeka likisubiri kifo chake. Ni taifa ambalo haliwezi tena kudhibiti madhara makubwa katika maisha yake ya kijamii ndani ya mujtama wake – italipa gharama kubwa kutokana na ukuwaji wa uchumi wake iliyokuwa inautafuta kwa gharama yoyote.

Nchi za Kimagharibi ndizo hasa zilizokuwa zinakuza majanga haya ya kijamii kabla ya nchi za Mashariki ya Asia na kutoka kwao ndipo tunapojifunza kwamba "kifo cha familia" hakisukumwi tu na uhuru wa kiuchumi pamoja na 'wanawake na uchumi'; bali pia inajumuisha uhuru wa jamii pamoja na misingi ya ubinafsi ambayo imesababisha majanga makubwa ya kiafya. Hali hizi kimsingi zinaangamiza maisha ya familia na zimepelekea kuwepo na nchi za ukame wa watu katika nchi nyingi za Ulaya na Amerika. Mnamo Januari 2018, Uingereza (UK) ilimteua waziri wa upweke ili kupambana na kile ambacho Waziri Mkuu Theresa May alikitaja "uhalisia wa majonzi ya maisha ya kisasa" kwa watu wengi kwa maana zaidi ya watu milioni 9 daima huwa wanajihisi kuwa wapweke na takribani wazee 200,000 nchini hawajawahi kuwa na mazungumzo na rafiki au jamaa zaidi ya mwezi. Lakini watu wa UK hawako peke yao katika upweke. Ndani ya Amerika (US), kama makala ilivyoandikwa ndani ya Harvard Business Review, "Upweke ni janga la kiafya linaloendelea kuongezeka. Tunaishi ndani ya zama ambazo teknolojia imetuunganisha zaidi katika historia ya wanadamu, lakini bado upweke umezidi maradufu tangu miaka ya 1980, leo zaidi ya asilimia 40 ya watu wazima ndani ya Amerika wanaripotiwa kuhisi upweke, na utafiti unapendekeza kwamba idadi kamili inawezekana kuwa juu zaidi." 

Uislamu Unatoa Suluhisho la Kudumu kwa Familia

Mawimbi makali ya uharibifu ambao yanaukumba muundo wa familia ndani ya nchi za kisekula za viwanda yamepelekea "kifo cha familia", hivi sasa yanaendelea kuhisika ndani ya ardhi za Waislamu. Ndani ya Malaysia, kwa mfano matarajio ya kutafuta maendeleo na cheo kama ilivyo katika nchi zilizoendelea zimeipelekea Malaysia kukodolea hali ya "Maradhi ya Thaqafa ya Chicago" ambapo ni taifa ambamo watu wanapata mapato makubwa lakini linafuatiwa na kusambaratika kimaadili. Profesa kutoka katika Taasisi ya Kimataifa ya Watu na Fikra ya Kiislamu (ISTAC), Mohd. Kamal Hassan aliionya serikali ya Malaysia ISIkuze dalili sawa na za Magharibi. Alisema, "Pia inatokea ndani ya Malaysia na itakuwa mbaya zaidi lau haitodhibitiwa kwa sababu misingi ya maadili na kujiheshimu binafsi kukochini, hili ni kubwa kupitia uhalifu kama vile kupora mpaka kifo, kuua na kubaka." Hakika huu ndio wasifu wa nchi za kisekula za viwanda hivi leo, ambapo maendeleo makubwa yanafuatiwa na majanga ya kijamii, kuporomoka kwa taasisi ya familia, kusambaa kwa uhalifu, vurugu dhidi ya wanawake na watoto na idadi kubwa ya kujitoa uhai kwa kuongezea na kushuka kwa idadi ya kuzaana ambayo kwa kiasi kikubwa ni kutokana na kuhusishwa kwa wanawake katika ufanyajikazi. Inadhihirisha ufinyu wa mtazamo wa kimfumo wa dola za kisekula za kirasilimali kwa kupatiliza madaniya na maslahi ya kiuchumi na kupuuza furaha ya familia na mujtama kwa ujumla.

Hivyo basi ni suala nyeti kwa Waislamu kurudi katika mafundisho ya Kiislamu na kujihusisha pasina kusita katika kampeni ya kuitekeleza nidhamu ya kisiasa tukufu ya Kiislamu katika kuhifadhi kizazi cha binadamu na kudumisha uzuri wa ustaarabu wa Kiislamu. Kumbuka Mwenyezi Mungu (swt) amesema:
﴾يا أَيُّهَا النَّاسُ اتَّقُوا رَبَّكُمُ الَّذي خَلَقَكُمْ مِنْ نَفْسٍ واحِدَةٍ وَ خَلَقَ مِنْها زَوْجَها وَ بَثَّ مِنْهُما رِجالاً كَثيراً وَ نِساءً وَ اتَّقُوا اللَّهَ الَّذي تَسائَلُونَ بِهِ وَالْأَرْحامَ إِنَّ اللَّهَ كانَ عَلَيْكُمْ رَقيباً﴿ “Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni." [An-Nisa': 1]

Mafundisho ya Kiislamu yanaweza kuwa ni njia yenye nguvu katika kuhifadhika katika zama hizi za uharibifu. Msingi muhimu wa mafundisho ya Kiislamu kattu hayawezi kupitwa na wakati na daima yatakuwa sambamba na familia ya zama hizi na hivyo basi lazima tujifunge nayo kikamilifu: Miongoni mwayo ni:

1. Uislamu unashaajiisha ndoa na kuzisifu taasisi za ndoa kuwa ndio njia pekee ya kuhifadhi kizazi.

2. Uislamu pia inazo hukmu za familia ambazo zinapangilia majukumu ya waume na wake ili kuweka maisha ya amani ya familia makini pamoja na kuasisi utulivu baina ya wanandoa.

3. Uislamu unasisitiza kuhusu ubora wa jukumu la umama kwa wanawake.

4. Lengo la ndoa katika Uislamu ni kumuabudu Mwenyezi Mungu (swt) kwa maana ni kuhifadhi kizazi na kupatikane amani (utulivu/ sakinah, mapenzi/ mawaddah na kuhurumiana/ rahmah), sio tu kukidhi haja ya kijinsia au kwa ajili ya kupata cheo katika mujtama. Hivyo basi, Uislamu umesisitiza msingi na umuhimu wa kuwepo na akili tambuzi katika kukifunza kizazi kilichopo na kijacho.

5. Uislamu umeweka msingi wa itikadi na kuamini (tawakul) katika Rizq kwa Waislamu ili isiweze kuyumbisha mpangilio wa majukumu ndani ya familia, kwa maana kuwa wanaume ndio wachumaji wa familia. 

6. Uislamu unayo nidhamu ya kiuchumi ambayo inabuni uchumi mzuri, unaozalisha na ulio na uwezo wa kuondosha ukosefu wa ajira mkubwa, kuhakikisha kunapatikana mahitaji msingi ya raia na wakati huo huo unawaruhusu watu binafsi kuweza kupata mahitaji ya ziada. Msingi wa sera zake umeelekezwa katika kusambaza utajiri ili kudhamini mahitaji mzingi ya raia wote, kuzuia ukandamizaji wa kiuchumi na unyanyasaji wa wanawake. Napia itawawezesha wanaume kutimiza majukumu yao ya kukidhi mahitaji ya kifedha kwa familia zao ilhali wakati huo huo dola imewajibishwa kuwapa wanawake ambao hawana jamaa wakiume msaada.

7. Uislamu umewawajibisha watawala Waislamu kuungana chini ya kivuli cha Khilafah ya Kiislamu kwani ndio kivuli cha kweli cha Waislamu ambacho kitailinda familia, heshima ya kina mama na kukitukuza kizazi cha Waislamu na kuwapa hadhi. Wakati huo huo Khilafah itailinda familia kutokana na machafuko ya ulafi wa Urasilimali na mizozo ya kijamii inayosababishwa na uhuru.

Hivyo basi, Khilafah itaweza kujenga familia madhubuti na kuangamiza vigezo vyote ambavyo vinaiharibu kama ilivyodhihirishwa katika matamshi ya Uthman (ra): "Hakika Mwenyezi Mungu anampa madaraka mtawala ili kuondosha kile ambacho hakiwezi kuondoshwa na Qu'ran." Wallahu a’alam

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Fika Komara
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:44
Yaliyomo ndani ya kifungu hichi: Je ni kweli wanakataa “ndoa za mapema”?! »

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu