Jumapili, 11 Dhu al-Qi'dah 1445 | 2024/05/19
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Gaza Yafunua na Kufichua

(Imetafsiriwa)

Katika wiki ndefu, zenye uchungu, tangu 7 Oktoba 2023, Gaza imefunua haki, na kufichua batili. Imebaini ukweli juu ya watu wa Gaza, Ummah wa Kiislamu kwa jumla, na wasio Waislamu wenye akili adilifu kote ulimwenguni. Imefichua uhalisia wa umbile la Kizayuni, dola za Magharibi zinazolisaidia na watawala wa Waislamu wanaoshirikiana. Kwa kufichua na kufunua, imetoa mwelekeo kwa Ummah wa Kiislamu na majeshi yake, juu ya kile ambacho kinapaswa kufanywa sasa.

Gaza imefunua kheri katika watu wake. Watu wake wana uvumilivu juu ya hasara kubwa. Wao ni shupavu usoni mwa uvamizi mkubwa. Hawalalamiki juu ya mitihani mizito. Wanatabasamu ili kuwapa wengine faraja, huku wao wenyewe wakiwa na maumivu. Wanagawiana chakula, katikati ya uhaba mkubwa na njaa. Wanainua mikono yao katika Dua ili kuwalipa fidia kwa hasara zao kubwa. Wameutikisa ulimwengu kwa Iman yao, wakijitahidi kupendwa na Mwenyezi Mungu (swt). Hakika, pindi Mwenyezi Mungu (swt) anapowapenda watu, Yeye (swt) huwapa mitihani. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ إِذَا أَحَبَّ قَوْمًا ابْتَلَاهُمْ فَمَنْ صَبَرَ فَلَهُ الصَّبْرُ وَمَنْ جَزِعَ فَلَهُ الْجَزَعُ»

“Hakika pindi Mwenyezi Mungu (swt) anapowapenda watu huwapa mitihani. Basi mwenye kusubiri atalipwa ujira wa Subira, na mwenye kunung’unika atalipwa manung’uniko.” [Imepokewa na Ahmad kupitia Mahmud b. Labeed].

Gaza amefichua kheri katika Ummah wa Kiislamu. Waislamu hawana utulivu wana maumivu, kwa mateso ya watu wa Gaza. Wanafanya kila wanachoweza. Wanaomba dua, mpaka mikono yao inauma. Wanatoa misaada, wakizibakisha tupu nyumba zao. Wanamsusia adui, na kusababisha hasara kubwa. Wanaomba mipaka ifunguliwe, ili waweze kutuma vijana wao. Wanayataka majeshi yao kutaharaki. Hakika Waislamu ni mwili mmoja, uliounganishwa na Iman yao. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«تَرَى الْمُؤْمِنِينَ فِي تَرَاحُمِهِمْ وَتَوَادِّهِمْ وَتَعَاطُفِهِمْ كَمَثَلِ الْجَسَدِ إِذَا اشْتَكَى عُضْوًا تَدَاعَى لَهُ سَائِرُ جَسَدِهِ بِالسَّهَرِ وَالْحُمَّى»

“Utawaona Waumini, katika kuhurumiana kwao na kupendana kwao na kuoneana upole kwao, ni mithili ya mwili mmoja. Pindi kiungo chochote kinaposhtakia maumivu, mwili wake mzima huitikia kwa kukosa usingizi na homa.”

Gaza imefunua upokewaji wa Uislamu, miongoni mwa watu wenye akili adilifu wa ulimwengu. Wengi wasiokuwa Waislamu wameonyesha hasira yao kwa dhulma dhidi ya watu wa Gaza. Wengi sasa wanatofautisha kati ya Uzayuni na Uyahudi. Wengi wameathirika na uvumilivu wa Waislamu wa Gaza. Baadhi yao wameanza kutafuta chanzo cha uvumilivu kama huo. Baadhi ya hawa wamesilimu, wakaribishwa kwa dhati na Ummah wa Kiislamu. Kukubaliwa huku kwa Uislamu ni katika wakati ambao hakuna dola inayotabikisha Uislamu. Vipi basi katika wakati ambapo Uislamu unatabikishwa na dola, na Uislamu unaonekana katika utukufu wake kamili? Thauban ameripoti kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «إِنَّ اللَّهَ زَوَى لِيَ الأَرْضَ فَرَأَيْتُ مَشَارِقَهَا وَمَغَارِبَهَا وَإِنَّ أُمَّتِي سَيَبْلُغُ مُلْكُهَا مَا زُوِيَ لِي مِنْهَا» “Hakika Mwenyezi Mungu alinikundulia mimi ardhi. Basi nikaiona mashariki yake na magharibi yake. Hakika ufalme wa Ummah wangu utafikia ncha hizo ambazo zilikunduliwa kwangu.” [Muslim].

Gaza amelifichua umbile la Kizayuni, ukatili wake na uadui wake, na pia udhaifu na uoga wake. Umbile la Kiyahudi halikuacha aina yoyote ya jinai pasi na kuitenda. Lililenga watoto kwa walengaji shabaha, kama ambavyo lililenga mahospitali kwa mabomu. Baadaye likaficha uhalifu wake kwa pazia la uongo na nyudhuru zilizotolewa na Marekani, lilianza kutekeleza uhalifu wake bila ya udhuru. Linaua kwa ukatili na udhalimu, likikosa kabisa "maadili" au "desturi" au "ubinadamu," ambayo wanadamu wameyazoea katika vita. Hakika, maneno ya Mwenyezi Mungu (swt) ni kweli kuhusu wao,

[لَا يَرْقُبُونَ فِي مُؤْمِنٍ إِلًّا وَلَا ذِمَّةً ۚ وَأُولَٰئِكَ هُمُ الْمُعْتَدُونَ]

Hawatazami kwa Muumini udugu wala ahadi; basi hao ndio warukao mipaka.” [Surah At-Tawba 9:10]. Yote haya ni mbali na ukweli kwamba Gaza imefichua udhaifu wa vikosi vya ukaliaji kimabavu. Licha ya silaha zao za kisasa, vikosi vioga vya askari wa Kizayuni havikuweza kuvishinda vikundi vidogo vilivyo na silaha duni, mujahidina mashujaa. Vipi basi lau wangekabiliana na jeshi moja la Waislamu?

Gaza imefichua serikali za Kimagharibi katika kuunga mkono kwa udhalimu wa Wazayuni. Dola ya Kizayuni inatekeleza ukatili wake mbele ya macho ya Magharibi muongo na mnafiki. Kujitolea kwa Magharibi kwa haki za binadamu, haki za wanawake, haki za watoto na haki za wanyama kumefichuliwa wazi. Kwa kuongezea, umbile la Kiyahudi linawauwa Waislamu kwa ridhaa na idhini ya Marekani, na ushiriki wake changamfu na msaada, kupitia propaganda za vyombo vya habari, ufadhili na silaha. Ushiriki wa Marekani sio chini ya kura yake ya turufu dhidi ya azimio lililopendekezwa la Umoja wa Mataifa la kusitisha mapigano mnamo 8 Disemba 2023. Yote haya sio chini ya idhini ya Marekani ya suluhisho ovu la dola mbili. Ni mpango wa kikatili wa Marekani unaokusudia kuikabidhi sehemu kubwa ya Ardhi Iliyobarikiwa kwa wavamizi wachokozi, na kuliacha umbo lisilo na silaha na duni, chini ya pazia la "Dola ya Palestina." Hakika, serikali za Kimagharibi na umbile la Mayahudi ni kama Mwenyezi Mungu (swt) ilivyowasifu, pindi Yeye (swt) aliposema,

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا الْيَهُودَ وَالنَّصَارَى أَوْلِيَاءَ بَعْضُهُمْ أَوْلِيَاءُ بَعْضٍ]

“Enyi mlio amini! Msiwafanye Mayahudi na Wakristo kuwa ni marafiki. Wao ni marafiki wao kwa wao.” [Surah Al-Ma’ida:51].

Gaza imefichua watawala wa Waislamu. Hata wakati umbile la Mayahudi likilipua mahospitali na shule, serikali ya Jordan ilidumisha daraja lake la angani kwa umbile la Kiyahudi, likitoa vifaa muhimu vya Kimarekani. Imarati (UAE) ilitia saini makubaliano ya kuendesha daraja la ardhini, kati ya bandari za Dubai na Haifa, kupitia eneo la Saudia na Jordan, kwa lengo la kukiuka vitisho kwa njia za usafirishaji wa meli. Watawala wa Waislamu wanafanya hivyo, badala ya kukata bahari, ardhi, na anga za ulimwengu, kuzuia usambazaji wa mafuta, na kutumia nguvu zao zote kukomesha umwagaji damu, wakati wanao uwezo wa kufanya hivyo. Misri inadumisha kufunga Kivuko cha Rafah, licha ya jeshi lake kuwa tayari zaidi na uwezo wa kuwanusuru Waislamu wa Gaza. Ama watawala wa Pakistan na Uturuki, wanapeleka askari wao kote ulimwenguni kwa maslahi ya Washington, huku, wakizuia askari walio tayari na wenye uwezo kutokana na kuinusuru Gaza katika kipindi chake cha uhitaji mkubwa. Baada ya kuwaangusha Waislamu wa Gaza na Ummah wa Kiislamu, sasa wanafanya kazi kutekeleza khiyana nyengine, suluhisho la dola mbili la Marekani. Wanafanya haya yote ingawa Mwenyezi Mungu (swt) amesema,

[إِنَّمَا يَنْهَاكُمْ اللَّهُ عَنْ الَّذِينَ قَاتَلُوكُمْ فِي الدِّينِ وَأَخْرَجُوكُمْ مِنْ دِيَارِكُمْ وَظَاهَرُوا عَلَى إِخْرَاجِكُمْ أَنْ تَوَلَّوْهُمْ وَمَنْ يَتَوَلَّهُمْ فَأُوْلَئِكَ هُمْ الظَّالِمُونَ]

“Hakika Mwenyezi Mungu anakukatazeni kufanya urafiki na wale walio kupigeni vita, na wakakutoeni makwenu, na wakasaidia katika kufukuzwa kwenu. Na wanao wafanya hao marafiki basi hao ndio madhaalimu.” [Surah Al-Mumtahina 60:9].

Gaza imefunua na kufichua na imetimiza jukumu lake mbele ya Mwenyezi Mungu (swt). Ni juu yetu kuhakikisha kuwa hatujafanya mapungufu kwetu. Imetuonyesha hali na njia ya kusonga mbele. Waislamu wa Gaza ni wema. Ummah wa Kiislamu unasonga kwenye Dini yake. Kuna kundi kubwa la wasiokuwa Waislamu ambao wanaweza kuona dhulma ya umbile la Kiyahudi na serikali za Kimagharibi zinazoliunga mkono, kwa upande mmoja, na misimamo mizuri ya Waislamu. Umbile la Mayahudi sio watu wanaoheshimu mikataba wala ahadi. Serikali za Kimagharibi ni zile zinazounga mkono umbile la Mayahudi katika vita vya wazi dhidi ya Waislamu. Watawala wa Waislamu ndio kikwazo pekee kwa majeshi kutaharaki kunusuru Uislamu na Waislamu. Mbele kuna njia moja pekee sasa. Ummah na majeshi yake lazima wawaondoe watawala wa Waislamu. Ni hapo ndipo Ummah wa Kiislamu unaweza kulazimisha kurudi nyuma kwa maadui zake kutoka kwa ardhi zake. Kwa hivyo, hebu Ummah na uyatake majeshi yake yaipe Hizb ut Tahrir Nusrah yao kwa ajili ya Khilafah kwa Njia ya Utume. Hebu uharibifu wa Gaza na uwe sura ya mwisho ya giza tangu kuvunjwa kwa Khilafah 1924 M, 1342 H.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Musab Umair – Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu