Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sio Suala Kupata Mamlaka Pekee, Badala Yake Mamlaka Hayo Yanapaswa kuwa kwa Ajili ya Uislamu

(Imetafsiriwa)

Taliban waliuchukua mji mkuu wa nchi hiyo Kabul na kuingia kasri la raisi wa Afghanistan baada ya raisi Ghani kukimbia. [Al Jazeera I 15 Agosti 2021]

Kulingana na makubaliano yaliyosainiwa katika Mkutano wa Pugwash nchini Qatar, Amerika iliondoka kambi ya anga ya Bagram wa Afghanistan baada ya takriban miaka 20 kupitia kukata umeme na kukimbia usiku bila kumjulisha kamanda mpya wa Kiafghan wa kambi hiyo. Halafu Taliban wakaingia kasri la raisi baada ya raisi Ashraf Ghani kuikimbia nchi hiyo kutokana na kusonga mbele kwa kasi kwa Taliban, ambapo ilishuhudiwa kundi hilo likiichukua miji mikuu ya majimbo 34 ya Afghanistan katika kipindi kisichozidi wiki mbili. Inawezekana katika siku chache, Taliban itaunda serikali mpya na kuanzisha Imarati ya Kiislamu ya Afghanistan kama ilivyokuwa katika kipindi cha 1996-2001.

Wakati wa mkutano wa Pugwash nchini Qatar, Taliban ilisaini makubaliano na Amerika juu ya kuondolewa kwa vikosi vya Amerika na NATO nchini Afghanistan na kujaribu kuonyesha picha mpya ya kisiasa kwa jamii ya kimataifa. Inafahamika kuwa tangu 2005 mtirirko wa mikutano ilifanyika katika mji wa Pugwash na mashauriano kadhaa na vikundi vya Waafghani na watu binafsi katika wigo wa kisiasa ili kuhamasisha mazungumzo na kubadilishana  maoni yanayowezekana kuelekea kupunguza vurugu na mizozo ndani ya Afghanistan. Amerika imehamasisha vibaraka wake wengi katika eneo hilo na ulimwengu wa Kiarabu ikiwemo Pakistan, Uzbekistan, Qatar, Falme za Kiarabu, Saudi Arabia pamoja na Iran ili kuishinikiza Taliban kukubali masharti ya Amerika juu ya mzungumzo ya amani. Wakati wa mikutano hiyo, Imarati ya Kiislamu ya Taliban ilijitolea kuheshimu Uhuru wa Kujieleza, Haki za Wanawake, uhusiano mzuri na nchi jirani na jamii ya kimataifa katika upande wa kuheshimiana. Zaidi ya hayo, walikubali kuliheshimu shirika la kipagani la Umoja wa Mataifa, Kongamano la Kiislamu lisiloegemea upande wowote, na Sheria ya Kimataifa ambayo haipingani na maadili ya Kiislamu na kitaifa kulingana na mtazamo wao.

Kwa kuongezea, Amerika inakusudia kutengeneza umbali, tofauti na hata uhasama kati ya Taliban na Mujahidina wengine wasio na wa Kiafghani kwa kutangaza masharti ya kimfumo; kwamba Mujahiddina lazima wajitenge na Al Qaeda, wakubaliane na katiba ya kisekula, ardhi ya Afghanistan haipaswi kutumiwa dhidi ya Amerika na washirika wake. Masharti haya katika makubaliano hayo yanamaanisha waziwazi kwamba Mujahidina ambao sio Waafghani hawapaswi kuendesha operesheni zao ndani ya Afghanistan. Kwa hiyo, Taliban wanalazimika kukata uhusiano na al-Qaeda na vikundi vingine vya kisilaha na havipaswi kuruhusiwa kuendesha operesheni zao nchini Afghanistan. Imarati ya Kiisalmu ya Taliban iliahidi kuwa haitadhuru nchi na mataifa mengine, wala hawataruhusu wengine kuitumia Afghanistan kwa faida yao wenyewe.

Inahitajika kutaja kwamba kwa sababu ya ujinga wa kisiasa walionao Taliban na shauku yao kubwa ya kuegemea njia ya mapigano pekee, imesaidia Amerika na NATO kuwatumia kama kifaa cha vita walivyovianzisha dhidi ya Waisalmu. Taliban wako katika kiwango kama alichokuwa nacho Mtume wetu (saw) ambaye alipewa ahadi kubwa kama atakubali kuachana na ulinganizi wa Kiislamu wakati akiwa Makkah. Mtume wetu (saw) hakukataa tu mapendekezo yao, lakini pia alisisitiza kwamba ataendelea kulingania Uislamu au afe kwa kusudi hili. Tunatumai kwamba Taliban inapaswa kujifunza kitu kutoka katika Seerah ya Mjumbe (saw) na haitanaswa na mkono wa makafiri kwa kisingizio cha amani inayotolewa kutoka Amerika.

Taliban inapaswa kufahamu kwamba, Amerika haina mpango wa kidhati wa kuleta amani nchini Afghanistan kwa sababu inajaribu kuwaoanisha ndani ya michakato ya Demokrasia na Umagharibi kama vile ilivyofanyika kwa muungano wa kaskazini na chama cha Kiisalmu cha Hekmatyari. Inaeleweka wazi kutokana na  ukweli uliotajwa hapo awali na shinikizo kwamba mchakato huu, kwa kweli, ni njama tu ya kisiasa ya kuvunja, kudhoofisha na kuisalimisha Taliban, kwa upande mmoja, kumaliza vita virefu zaidi vya Amerika nchini Afghanistan ambavyo vimegharimu $ 2 trilioni, na kwa upande mwengine, kuisaidia Amerika kutimiza kwa bidii malengo ambayo haikuweza kutimiza kwa miaka ishirini iliyopita kwa njia ya vita.

Leo hii, jambo nyeti kwa Waislamu ni kurejesha dola moja ya Kiislamu ya Khilafah ambayo itaendesha vita vya jihad dhidi ya uvamizi wa makafiri pamoja na kuvunja mahusiano yote na nchi zilizomstari wa mbele kuwapiga vita Waislamu na kuwabadilisha watawala vibaraka na serikali ziliopandikizwa katika za ulimwengu wa Kiislamu. Uundaji tu wa Imarati ya Kiislamu pekee hauwezi kutatua kadhia yetu nyeti na itawapoteza muelekeo Waislamu juu ya kufikiria kidhati kuanzisha Dola moja ya Kiislamu ya Khilafah. Hivyo basi, fahamu ya Imarati inawasaidia tu Wamagharib katika mchakato wao wa kuzuia kusimama kwa dola moja halisi ya Kiislamu ambayo itasimamia masuala ya Ummah kwa Shariah tukufu ya Mwenyezi Mungu Azza wa Jal.

Taliban inapaswa kuelewa kwamba fikra na fahamu za Uislamu katika mifumo ya utawala, siasa, uchumi, jamii, elimu; na mengineyo zote zimekamilika na ziko tayari kwa utabikishaji wa kivitendo ndani ya dola ya Kiislamu. Hizb ut Tahrir imeunda ufahamu kamili ya maisha ya Kiislamu, chini ya Dola ya Khilafah na kutabanni rasimu ya katiba ya dola hii, yenye vifungu 191; iliyovuliwa kwa Ijtihad sahihi kutoka kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake (saw) na vyanzo vilivyoashiriwa nazo: Ijma ‘As-Sahaba (Makubaliano ya masahaba) na Qiyas (mlinganisho) ya Kisheria. Tunatoa wito kwa watu wanyofu wenye nguvu nchini Afghanistan kuungana na Hizb ut tahrir na kutambua kuwa Mwenyezi Mungu (swt) huwapa ushindi wale wanaounusuru Uislamu.

[لِلَّهِ ٱلْأَمْرُ مِن قَبْلُ وَمِن بَعْدُ * وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ ٱلْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ ٱللَّهِ يَنصُرُ مَن يَشَاءُ وَهُوَ ٱلْعَزِيزُ ٱلرَّحِيمُ]

“Amri ni ya Mwenyezi Mungu kabla yake na baada yake. Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Surah Ar-Rum 30:04-05]

        #Afganistan         #Afghanistan              أفغانستان#

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Hameed Bin Ahmad

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu