- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
NATO Yahangaikia Uhusiano Stahiki
(Imetafsiriwa)
Mkutano wa mwanzo baina ya Ulaya na Amerika ulifanyika karibuni katika mkutano wa Wakuu wa Nchi za NATO mjini Brussels. Baada ya Donald Trump kuikosoa Ulaya kwa kutotekeleza jukumu lao katika mahusiano ya ushirikiano wao unaovuka ng'ambo ya bahari ya Atlantiki kufikia kiwango cha chini kabisa baina ya washirika. Joe Biden kwa sasa akiwa raisi mpya wa Amerika amekuwa na shauku kuwasilisha upande mpya wa mahusiano ya Amerika na miungano na kufufua ushirikiano wa usalama wa eneo la nje ya bahari ya atlantiki na kuwa ni sehemu muhimu ya mkakati wake unaofuatia ule wa Trump. Lakini NATO imekuwa ikifanya jitihada kwa miongo kadhaa kujitafsiri upya na haitegemewi kulifikia hili katika hali ya sasa ya ulimwengu.
NATO imeendesha dori muhimu katika kuunganisha uwezo wa kijeshi wa Amerika na Ulaya wakati wa Vita Baridi. Wakati vilipomalizika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, bara la Ulaya liliharibiwa kutokana na vita vilivyoenea barani humo. Umoja wa Kisovieti uliibuka kuwa dola kubwa na mipaka yake ilienda hadi Berlin Ujerumani. Ulaya ilikuwa kwenye maangamizi na hakukuwa na fursa ya kujihami dhidi ya maelfu ya vifaru vya Kisovieti ambavyo macho yao yakiangazia kila kitu Magharibi mwa Berlin na ilikuwa katika uhalisia huu ambao umeipelekea Amerika kutoa uhakikisho wa usalama Ulaya kulihami bara la Ulaya ili lisiingie kwenye ukomunisti. Hadi 1991 lengo la NATO lilikuwa wazi, adui alikuwa wazi na uwezo wa kijeshi, operesheni ya kikanuni na mkakati ulikuwa wazi kabisa. Kila taifa la Ulaya lilikuwa wazi katika jukumu lake dhidi ya ukomunisti.
Tokea kuvunjika kwa Umoja wa Kisovieti mwaka 1991, NATO imekumbana na mgogoro wa utambulisho. Kuondoshwa kwa kitisho cha kijeshi cha Usovieti imeifanya NATO kutohitajika na licha ya uingiliaji wa muungano katika vita vya Balkan imebakia kuwa muungano usio na adui wa kweli na lengo. Katika miaka ya 90, Vita Vikuu vya Pili vilishapita zaidi ya miongo minne nyuma katika historia na Ulaya haikuona hitajio la kuendelea kubakisha vikosi vingi vya kijeshi katika muungano wa eneo la nje ya bahari ya atlantiki dhidi ya Urusi. Katika miaka ya 90, Ulaya haikuitegemea Amerika kama ilivyokuwa katika miaka ya 50 na hivyo fedha nyingi zilikwenda kwenye uendelezaji wa majeshi ya kitaifa kwa lengo la kujenga usalama wa nchi badala ya wao kuwa na ushirikiano na muundo wa kimuungano. Miaka ya 90 pia ilishuhudia Mkataba wa Maastrich uliounganisha Ulaya, na ikiwa ni jumuiya, imekuja kushindana na Amerika kiuchumi. Ulaya haikuona umuhimu wa NATO katika ulimwengu wa baada ya Usovieti na hii inaweza kuonekana katika kupungua matumizi yake ya kijeshi.
Ulaya pia imeiangalia Urusi tofauti sana na vile ilivyokuwa ikiiangalia wakati wa Vita Baridi. Kwa miongo miwili baada ya 1991 Ulaya Mashariki ilifunguliwa kuingia Ulaya na Umoja wa Ulaya ulitanuka kwa kuingiza mataifa mengi kadiri ilivyoweza yaliyokuwa kwenye Usovieti. Urusi ilitoa kitisho kidogo tu, na baadhi ya mataifa kama Ujerumani yalitegemea mahusiano ya nishati pamoja na Urusi. Hata hivi leo Urusi haifanani na Umoja wa Kisovieti, ni dhaifu zaidi. Mkakati mkuu wa Urusi sio tena Jeshi Jekundu bali ni mkakati wa kijeshi wenye mchanganyiko kama kuunga mkono vyama vya mrengo wa kulia, mapambano ya kimtandao na taarifa potofu. Mkakati huu ni dhihirisho la uwezo finyu wa Urusi.
Kila miongo inavyopita, tofauti baina ya Ulaya na Amerika inaongezeka. Bomba la mafuta la Nord Stream 2 limeleta mgawanyiko miongoni mwa mataifa ya Ulaya kama lilivyoleta kwa Amerika. Amerika hivi sasa inaangalia kuiweka China badala ya Umoja wa Kisovieti kuwa ni adui mkuu wa washirika na kwa hili, Ulaya na Amerika haziko sambamba. China haina mipaka au bahari ya pamoja na Ulaya na hivyo kutoa hatari ndogo kwa bara Ulaya na pia hutoa manufaa mengi ya kiuchumi kwa upande wa biashara, teknolojia na Miradi ya Moja kwa moja ya Kigeni (FDI). Wakati Umoja wa Kisovieti ulitoa kitisho cha karibu sana cha usalama, China iko upande wa pili Eneo la Eurasia kulingana na Ulaya inavyohisi. China inatoa teknolojia kwa Ulaya ambapo Umoja wa Kisovieti haukuweza kuitoa na hii ndio sababu kwa nini Amerika inahangaika kupata ushirikiano wa Ulaya dhidi ya China.
Kwa namna nyingi NATO ni taasisi ambayo imeundwa kwa kipindi kirefu, enzi za karne iliyopita. Amerika hivi sasa inaikabili China zaidi katika mawanda ya kiuchumi na NATO haikuwa mshirika wa kiuchumi na hivyo Amerika itajitahidi kuiweka Ulaya kutimiza mahitaji ya kifedha dhidi ya China, ambayo hawaitazami China kuwa ni kitisho cha kijeshi. Kwa kipindi kirefu NATO ilikuwa ni zana iliyotumiwa na Amerika kwenda nayo sambamba, hivi leo zana hii imekosa mazingira ya kuchukua jukumu sawa, licha ya kauli kubwa kubwa na taarifa za pamoja.
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Adnan Khan