Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Umma wa Uislamu Hivi Karibuni Utachukua Nafasi Yake ya Juu Je, Wito wa Watoto Wake Wenye Ikhlasi Utaitikiwa?
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu (swt) asema katika ayah ya 110 ya Surat Aal-i-Imran

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْراً لَّهُم مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu.” Katika Tafsir ya Ibn Kathir:

[كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ]

“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu”: watu bora kwa watu, muwalete kwa minyororo shingoni mwao mpaka waingie katika Uislamu...” Maana yake: ni umma bora na wenye manufaa zaidi ya watu kwa watu.

Ummah wa Uislamu ni ummah ambao:

Mwenyezi Mungu aliukirimu kwa kubeba ujumbe huu mtukufu ambao Mwenyezi Mungu aliutuma kama muongozo na rehma kwa walimwengu.

Jukumu: Mtume wake (saw) aliukabidhi amana yenye thamani kubwa; Dini ya Mwenyezi Mungu aliyoichagua kwa waja wake.

Mtume wake (saw) aliuacha ukiwa mtukufu, akiongoza ulimwengu, kuusimamia, na kuutawala kwa mujibu wa Shariah ya Mwenyezi Mungu.

Unaunganishwa na dola ambayo kwayo hukmu za Mwenyezi Mungu hutabikishwa na kuenea kati ya watu wote ili kuelekeza maisha yao na kueneza rehma na uadilifu wa Mwenyezi Mungu miongoni mwao.

Lakini watu wa batili walipanga njama dhidi ya Ummah huu na wakaivunja dola yake na wakalazimisha sheria ngeni kwao na kwa itikadi yake; sheria za kibinadamu zinazotokana na itikadi ya ukafiri zilimfanya Mwenyezi Mungu kuwa mshirika katika hukmu yake, wakauonjesha misiba na kuupotosha kutoka katika hukmu za Dini yake iliyotabikishwa juu yake kwa karne nyingi, hivyo ukaeneza uadilifu, usalama na utulivu ndani yake na kuuhuisha na watu wote kwa maisha mazuri.

Madhalimu hawa wahalifu wamechagua dini nyengine isiyokuwa Dini ya Mwenyezi Mungu ili kuilazimisha kwa Umma wa Kiislamu na juu ya wanadamu wote.

[أَفَغَيْرَ دِينِ اللّهِ يَبْغُونَ وَلَهُ أَسْلَمَ مَن فِي السَّمَاوَاتِ وَالأَرْضِ طَوْعاً وَكَرْهاً وَإِلَيْهِ يُرْجَعُونَ]

“Je, wanataka dini isiyo kuwa ya Mwenyezi Mungu, na hali kila kilichomo mbinguni na katika ardhi kimesilimu kwa kumt'ii Yeye kikipenda kisipende, na kwake Yeye watarejeshwa?” [Aal-i-Imran: 83]. Wakamkataa Mwenyezi Mungu, Muumba wao, na wakabadilisha kilicho bora kwa kilicho duni

[وَمَا أُمِرُواْ إِلاَّ لِيَعْبُدُوا إِلَـهاً وَاحِداً لَا إِلَـهَ إِلاَّ هُوَ سُبْحَانَهُ عَمَّا يُشْرِكُونَ]

“Na wala hawakuamrishwa isipo kuwa wamuabudu Mungu Mmoja, hapana mungu ila Yeye. Subhanahu, Ametakasika na hayo wanayo mshirikisha nayo.” [At-Tawba: 31]. Walibadilisha sheria zilizo na mapungufu na zisizo na uwezo badala ya Sheria za Mwenyezi Mungu, Al-Khabir Al-A’lim.

Uhalisia wa maisha ya mwanadamu umekuwa uhalisia kinyume na inavyopaswa kuwa! Mwenyezi Mungu (swt) ameumba maisha haya, na Yeye Peke Yake ndiye Mjuzi wa kile kinachoyatengeneza na kile kinachoyaongoza. Ili maisha haya yawe katika hali yake ya kimaumbile, ni lazima aabudiwe Mwenyezi Mungu Peke Yake, asiye na mshirika wala hakuna amri isipokuwa amri yake.

[أَلاَ لَهُ الْخَلْقُ وَالأَمْرُ]

“Fahamuni! Kuumba na amri ni zake.” [Al-A’raf : 54]. Hili ndilo Mwenyezi Mungu analoridhika nalo kwa waja Wake.

[الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِيناً]

“Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini.” [Al-Ma’ida : 3]. Ni neema kubwa ya Mwenyezi Mungu (swt) juu ya Umma wa Kiislamu, kwani Mwenyezi Mungu aliikamilisha Dini kwa waja wake, kwa hivyo hawahitaji Dini isiyokuwa hiyo, wala Mtume asiyekuwa Mtume wao (saw). Mwenyezi Mungu (swt) alimfanya kuwa wa Mwisho wa Mitume na akamtuma kwa wanadamu na majini. Hakuna Halali isipokuwa Alichohalalisha na hakuna Haramu isipokuwa Alichoharamisha, na hakuna Dini isipokuwa Aliyoipitisha sheria yake. Endapo wakikengeuka kutoka katika mfumo huu wa maisha, watapotea na kuishi katika taabu na kurudi kwenye giza na upotofu.

[وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُهُ يَوْمَ الْقِيَامَةِ أَعْمَى]

“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu.” [Ta-Ha: 124]

Ni mfumo wa maisha unaowaonyesha Waislamu njia ya wokovu na kuwafanya kuwa taifa bora linalowaongoza watu kwenye wema na kuwalinda kutokana na maisha duni na ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu. Ni mfumo wa maisha unaojumuisha tiba na suluhisho zote za matatizo yanayomkabili mwanadamu, haijalishi ni mengi au magumu kiasi gani, kwa sababu ni masuluhisho kutoka kwa Al-Khabir Al-A'lim (Mwenye habari, Mjuzi wa yote. ). Ni hitajio halisi na ukweli wa Shariah ambao mtu hawezi kuukosa na kuishi maisha yake bila yake. Ni mfumo wa maisha ulioundwa na muumba na mwelekezi wa Ulimwengu huu. Ni ukweli wa kiulimwengu uliothibitishwa na aliyoyapitia mwanadamu pale alipoishi bila ya hukmu za Mola wake na sheria zake, na haja yake katika maisha ilidhihirishwa na yale yaliyowasibu Waislamu hasa na wanadamu kwa jumla pale walipoitelekeza sheria ya Mwenyezi Mungu na maisha yao kutenganishwa na Dini yao.

Mapigo mengi yaliupata Ummah huu, yaliyoushinda mbele ya maadui zake, waliowanyanyasa watoto wake, wakabomoa nyumba zake, wakapora utajiri wake, na kuua maelfu ya vijana, wanawake na watoto wake, lakini ni Ummah ambao haujafa na kamwe hautakufa.

Umma wa Uislamu ni Umma uliopanuka, na unazaa; ni Ummah uliobeba bendera ya Dini hii na utaibeba mpaka Siku ya Kiyama, haijalishi kile kinachousibu au maumivu unayoyapata. Vipi basi taifa ambalo umbo lake lilifinyangwa na Qur’an na muundo wake kuasisiwa na Mtume (saw), linaweza kuwapandikiza Shahada kwa watoto wake, na kuwakabidhi amana ili wafe? Yakini yetu iko madhubuti na haiteteleki na matukio uchungu ambayo Ummah uliyapitia, wala  kwa raundi walizoshinda maadui wahalifu. Ushindi huo bila shaka unakuja, na tamkini hiyo ndio matokeo yake, hakuna shaka juu yake. Tuna yakini kwamba Mwenyezi Mungu (swt) ataidhihirisha dini hii, atainusuru, na ataitukuza, kama alivyowaahidi waja wake wanyoofu.

[وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُم فِي الأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِن قَبْلِهِمْ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur :55].

Maadui wa Ummah huu wamechanganyikiwa kuhusu hilo! Ni tofauti sana na mataifa mengine kwamba endapo yangeguswa na machache katika yale yaliyousibu, isingebakia alama yake, bali ni Umma mtukufu ambao Dini yake iliyoutukuza ni tukufu. Watu wengi wa batili (Mkruseda na wale wanaoichukia Dini hii katika historia yote) wamejaribu mbeleni ya kuuua, lakini wameshindwa. Vita vya haki na batili ni vya kuendelea na vya kudumu mpaka Mwenyezi Mungu atakapoirithi ardhi na vilivyoko juu yake.

Ikiwa taghut (batili) imechukua udhibiti wa Ummah wa Uislamu, na ikiwa wameudhoofisha na kulivunja umbile la dola yake, ni kwa sababu ya utiifu wa baadhi ya nafsi dhaifu miongoni mwa watoto wake, ambao akili zao duni zimeshambuliwa na thaqafa ya Kimagharibi na fikra zake potovu, na kushindwa kwa waoga wengi walioziuza nafsi zao na heshima zao, wakauacha Ummah wao, na kuidunisha Dini na heshima yao.

Wamagharibi wametambua kwamba nguvu ya Umma wa Uislamu iko katika umoja wake na katika kuishi kwake katika kivuli cha dola moja inayoelekeza maisha yake kwa mujibu wa hukmu za Mwenyezi Mungu, hivyo kufanya kazi ya kuuangamiza umoja huu ili kuudhoofisha na kuudhibiti, na kuanza kuufanyia kazi mpango huu karne nyingi zilizopita, kueneza thaqafa yake ambayo inatokana na ukweli kwamba Dini lazima ifungwe kwenye pembe za misikiti na kutengwa na maisha. Janga kubwa lilikuwa ni kupindua dola yake na kuzigawanya nchi zake katika vijidola vidogo, ambavyo kwavyo walipandikiza vibaraka ambao wangetekeleza mipango yao na kueneza thaqafa yao ya kuwapotosha Waislamu kutoka kwenye Dini yao na kuwafanya watilie shaka uhalali wake na uwezo wake wa kutatua mengi ya matatizo magumu.

Hali ya Umma hivi leo na vile unavyoishi chini ya kivuli cha migawanyiko ya Sykes-Picot na udhaifu na udhalilifu uliotokana na hilo uliwawezesha maadui wa kundi hilo lenye nguvu lililostahamili kwa muda mrefu mbele ya majaribio yao kudhoofisha na kuuhujumu. Hali hii ya Ummah inadhihirisha wazi kwamba Waislamu, kwa jinsi walivyo katika suala la kugawanyika na kusambaratika, hawawezi kurudi kwenye heshima na izza yao. Ummah wao hauwezi kushika nafasi yake ya asili ya kuwa kiongozi wa mataifa unayoyaongoza kwenye njia ya kheri na kuyaangaza maisha ya watu kwa nuru ya Uislamu, isipokuwa kwa kuregea kwenye uhai chini ya kivuli cha dola inayowaunganisha na kuwatawala kwa sheria ya Mwenyezi Mungu na kuieneza kama rehma kwa walimwengu.

Hali ya Umma hivi leo - hata kama kuna majaribio mengi ya kuuhuisha - inafichua kufeli kwa masuluhisho haya ya kiviraka, ambayo uliifanya hali kuwa mbaya na ngumu zaidi, kwa sababu ni masuluhisho yanayoupotosha Ummah na kuuweka mbali na kuufahamu uhalisia wa hali yake na kujua sababu halisi za udhaifu na udhalilifu wake na kuupurukusha kutokana na kutafuta njia sahihi ya wokovu.

Lakini licha ya kila kilichopangwa kwa ajili yake kutoka ndani na nje, Ummah huu kamwe hautakufa, na Mwenyezi Mungu (swt) ataifanya Dini yake ishinde na kuikamilisha Nuru yake.

[وَيَأْبَى اللَّهُ إِلاَّ أَن يُتِمَّ نُورَهُ وَلَوْ كَرِهَ الْكَافِرُونَ]

“…na Mwenyezi Mungu anakataa ila aitimize Nuru yake ijapo kuwa makafiri watachukia.” [At-Tawba: 32].

Ulinganizi huu umehifadhiwa, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, na kamwe hautakufa:

Pindi Mtume wake (saw) alipozingirwa huku akimhakikishia swahaba wake katika Pango la Thawr:

«يَا أَبَا بَكْرٍ، مَا ظَنُّكَ بِاثْنَيْنِ اللَّهُ ثَالِثُهُمَا»

“Ewe, Abu Bakr, unadhani vipi, kwa watu wawili, ambao watatu wao ni Mwenyezi Mungu?” Yeye (saw) anaufundisha Ummah wake kumtegemea Mwenyezi Mungu, na nusra yake, na anawafundisha masomo katika uthabiti juu ya haki

Hata siku ya Badr, Waislamu walipokuwa wachache na makafiri ni wengi, na Mtume (saw) akamwambia Abu Bakr wakati wa vita:

«أَبْشِرْ يَا أَبَا بَكْرٍ، أَتَاكَ نَصْرُ اللَّهِ، هَذَا جِبْرِيلُ آخِذٌ بِعِنَانِ فَرَسِهِ يَقُودُهُ عَلَى ثَنَايَاهُ الْغُبَارُ»

“Pokea bishara njema, ewe Abu Bakr, nusra ya Mwenyezi Mungu imekujia. Huyu ni Jibril ameshika hatamu za farasi wake, anamuongoza kwenye vumbi kwenda zizini kwake.”

[إِذْ يُوحِي رَبُّكَ إِلَى الْمَلائِكَةِ أَنِّي مَعَكُمْ فَثَبِّتُواْ الَّذِينَ آمَنُواْ سَأُلْقِي فِي قُلُوبِ الَّذِينَ كَفَرُواْ الرَّعْبَ فَاضْرِبُواْ فَوْقَ الأَعْنَاقِ وَاضْرِبُواْ مِنْهُمْ كُلَّ بَنَانٍ]

“Mola wako Mlezi alipo wafunulia Malaika: Hakika Mimi ni pamoja nanyi, basi watieni nguvu walio amini. Nitatia woga katika nyoyo za walio kufuru. Basi wapigeni juu ya shingo na wapigeni kwenye kila ncha za vidole.” [Al-Anfal: 12].

Sio katika Vita vya Al-Ahzab, ambavyo vilikuwa ni vita vya mishipa ya fahamu na vilikuwa ni mojawapo ya vita vikali zaidi na muhimu sana katika historia ya Uislamu, kwani hatima ya ujumbe huu mtukufu ilikuwa sawa na hatima ya mtu anayetembea ukingoni mwa ardhi iliojaa hatari,

[إِذْ جَاؤُوكُم مِّن فَوْقِكُمْ وَمِنْ أَسْفَلَ مِنكُمْ وَإِذْ زَاغَتْ الأَبْصَارُ وَبَلَغَتِ الْقُلُوبُ الْحَنَاجِرَ وَتَظُنُّونَ بِاللَّهِ الظُّنُونَا * هُنَالِكَ ابْتُلِيَ الْمُؤْمِنُونَ وَزُلْزِلُوا زِلْزَالاً شَدِيداً]

“Walipo kujieni kutoka juu yenu, na kutoka chini yenu; na macho yalipo kodoka, na nyoyo zikapanda kooni, nanyi mkamdhania Mwenyezi Mungu dhana mbali mbali * Hapo ndipo Waumini walipo jaribiwa, na wakatikiswa mtikiso mkali.” [Al-Ahzab: 10]. Na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akatamka:

«لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ وَحْدَهُ، صَدَقَ وَعْدَهُ، وَنَصَرَ عَبْدَهُ، وَأَعَزَّ جُنْدَهُ، وَهَزَمَ الْأَحْزَابَ وَحْدَهُ، فَلَا شَيْءَ بَعْدَهُ»

Hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja pekee, imetimia ahadi yake, na amemnusuru mja wake, na akalipa ushindi jeshi lake, na akawashinda Ahzab peke yake, basi hakuna chengine baada yake. Utulivu ulirudi kwenye nafsi, na nguvu za Waislamu zilionekana mbele ya migogoro na matatizo.

Sio wakati Watatari waliposhambulia Baghdad na kuwaua Waislamu kwa muda wa siku arubaini na damu kumwagika katika mitaa yake hadi Mwenyezi Mungu (swt) alipomtuma Al-Muzaffar Qutuz, kiongozi wa Kiislamu ambaye alitoa kilio chake maarufu "Wa Islamah" huko Ain Jalut. Kwa hivyo jeshi la Uislamu likaitikia wito huu na kuwamaliza Watatari, na Uislamu ukawa mshindi.

Misiba mingi iliikumba Ummah, na ukatokana nayo, ikiwemo maudhi na matatizo, na bado ungali unataabika kwayo, lakini haikuua, haikuuangamiza, na kamwe haitauangamiza. Hivyo basi ulinganizi wa Uislamu ni ulinganizi ambao Mwenyezi Mungu (swt) ameuhifadhi mpaka Siku ya Kiyama, na ni nuru aliyoituma (swt) kwa waja wake, na Umma wa Uislamu ndio uliochaguliwa na Mwenyezi Mungu kubeba ulinganizi huu, kwa hiyo unawezaje kufa?

Umma wa Uislamu kamwe hautakufa, Mwenyezi Mungu (swt) ameukabidhi amana ujumbe huu, na hata ukiwa dhaifu na dhalili kiasi gani, utaregea, kwa idhini yake, na kuwa taifa bora zaidi iwapo utarejesha mamlaka izza yake zilizonyakuliwa na kuchukua hadhi na dori ambayo Mwenyezi Mungu amezifanya kuwa heshima na jukumu kwake.

Umma wa Uislamu ni umma ambao Mwenyezi Mungu alitaka ubakie maadamu wema ungalipo hapa duniani; Yeye (swt) aliutaka uwaongoze watu kwenye wema na kueneza rehma ambayo Mwenyezi Mungu (swt) aliituma kwa waja wake. Dori yake ni kiongozi muanzilishi ambao unaweza tu kuiregesha tena iwapo utarudisha maisha yake chini ya Uislamu ndani ya dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume ambayo Mwenyezi Mungu aliwaahidi waja wake wema na Mtume wake (saw) akawapa bishara njema.

Na huyu hapa mwanzilishi ambaye hakuwadanganya watu wake na wala kamwe hatawadanganya, akiwanyooshea mkono watoto wa Ummah wake akiwataka wajipange nyuma yake na wamuunge mkono ili awe ni kiongozi anayewaongoza kwenye wokovu kutoka katika utiifu kwa Magharibi na hadhara yake na kuregea kuishi chini ya hukmu za Uislamu zitakazowatoa watu wote kutoka katika giza wanamoishi hadi kwenye nuru ya uongofu na rehma ya Mwenyezi Mungu. Enyi watoto wa Umma wa Uislamu, wanazuoni wake, na watu wenye nguvu na ulinzi wake, njooni muitikie wito wa Hizb ut Tahrir na muinusuru Dini yenu na mchukue nafasi ya Ansari (wenye kunusuru).

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zeina As-Samit

 

Fuatilia na Sambaza Alama Ishara za Kampeni:

#Time4Khilafah

#EstablishKhilafah

#ReturnTheKhilafah

#TurudisheniKhilafah

#KhilafahBringsRealChange

#بالخلافة_يحصل_التغيير_الحقيقي

أقيموا_الخلافة#

كيف_تقام_الخلافة#

#YenidenHilafet

#HakikiDeğişimHilafetle

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu