Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
H. 8 Rabi' II 1447 | Na: 1447 / 03 |
M. Jumanne, 30 Septemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Simama pamoja na Watu Wasioteteleka wa Gaza, Sio na Trump Mwenye Kiburi!
(Imetafsiriwa)
Miaka miwili imepita tangu mauaji ya halaiki yanayofanywa na umbile nyakuzi la Kiyahudi huko Gaza, ambalo liliyafanya ili kuficha kushindwa kukubwa lilikokupata mnamo Oktoba 7, 2023. Miaka miwili ambayo kila siku ilishuhudia mauaji mapya na ukatili usioelezeka, na dunia nzima imeshuhudia ukatili wa Mayahudi wanyakuzi ambao unakinzana na akili. Watoto, watoto wachanga, nyumba, shule, misikiti na hospitali zililengwa. Watawala wa nchi za Kiislamu walikutana mara kwa mara, wakazungumza, wakalaani, na kisha kutawanyika. Kila shutma iliwashajiisha Mayahudi kufanya uvamizi na mauaji makubwa zaidi. Umbile la Kiyahudi lilifikia hatua ya kuzuia kuingia kwa kipande cha mkate au tama la maji ndani ya Gaza kwa miezi mingi mirefu.
Wauaji wanyakuzi hawakuishia Gaza bali pia walishambulia Syria, Lebanon, Iran, Yemen, na Qatar, na kisha Sumud Flotilla iliyosafiri baharini kutoka Tunisia. Wakati matukio yote hayo yakifanyika, Erdoğan na baadhi ya watawala wa Kiarabu walikutana jijini New York katika meza ya rais mwenye kiburi wa Marekani Trump kujadili mpango ambao ni pamoja na kuwapokonya silaha mujahidina, kuikalia kimabavu Gaza, na kuisaliti Palestina, na wakammiminia sifa tele.
Hizb ut Tahrir / Wilayah Uturuki, katika kumbukumbu ya mwaka wa pili wa vita vya Mayahudi dhidi ya Gaza, iliandaa matembezi chini ya kauli mbiu “Tunataka Vitendo, Sio Maneno,” jijini Istanbul, Ankara, na Şanlıurfa, kwa ushiriki na uungaji mkono wa makundi ya Kiislamu na uwepo wa makumi ya maelfu ya Waislamu. Mwenyezi Mungu ayalipe kheri makundi yote ya Kiislamu yaliyotembea nasi, Waislamu wote walioshiriki, na wanazuoni na walinganizi waliosema ukweli bila ya woga. Wakati wa taarifa kwa vyombo vya habari zilizotolewa baada ya matembezi, watawala walihutubiwa kwa matakwa ya vitendo:
Enyi wenye uwezo na mamlaka! Mumeshutumu, kulaani vikali, na kufanya mikutano ya kidiplomasia isiyo na matunda, huku mamia ya maelfu ya watu wasio na hatia wakiuawa. Na munajua vizuri kwamba yote haya hayakuwa hatua za kweli au za kuzuia. Mayahudi wanyakuzi hawazuiwi na maneno, na mauaji ya halaiki ambayo yameingia mwaka wake wa tatu hayatakwisha kwa hotuba za hamasa, na watu wanaodhulumiwa wa Gaza hawataokolewa kwa mazungumzo tu. Huu sio wakati wa maneno bali ni wakati wa vitendo, na kinachotakiwa si kauli za kulaani bali ni hatua za kivitendo na za kuzuia.
Matakwa yalitolewa kwa mamlaka kusimama na watu wasioteteleka wa Gaza, sio na Trump mwenye kiburi, na kuondoka kutoka kwa maneno kwenda kwenye vitendo vinavyoonekana. Matakwa hayo yalijumuisha kufungwa kwa Kambi ya Incirlik na kituo cha rada cha Kürecik, kuondolewa kwa uraia kutoka kwa raia wenye uraia wa nchi mbili wanaohudumu katika jeshi la uvamizi na kufunguliwa mashtaka kwao, kukatwa kabisa kwa mahusiano ya kibiashara na kidiplomasia na umbile hilo nyakuzi, kukataliwa kwa maazimio tasa ya Umoja wa Mataifa, kufunguliwa kwa ukanda wa kibinadamu hadi Gaza, ulinzi kwa Sumud Flotilla na wanajeshi wa majini, kuliorodhesha umbile la Kiyahudi kama umbile la kigaidi, na kusitishwa kukaririwa kwa mpango wa suluhisho la dola mbili wa Marekani.
Ulazima wa kusimama na mujahidina pia ulisisitizwa ili kwamba asibakie hata mnyakuzi mmoja katika ardhi ya Palestina. La kusikitisha, siku moja tu baada ya wito huu, Erdoğan alitangaza kuunga mkono mpango wa Trump mwenye kiburi na kumsifu. Mpango huu, unaoungwa mkono na Uturuki na tawala za Kiarabu, unauzingatia upinzani wa Gaza kama ugaidi na unaupa uhalali uvamizi wa Palestina yote. Tunamuomba Mwenyezi Mungu mpango huu usifanikiwe. Kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, wale wanaosubiri afueni kutoka kwa Trump watavunjika moyo sana.
Ama ujumbe kwa muuaji Netanyahu na Mayahudi wanyakuzi ni: Enyi waoga waovu! Kina mama wa Kiislamu wanawanyonyesha watoto wao uadui wenu, kina baba wanawashauri watoto wao wa kiume kupigana nanyi, na vijana wanahesabu siku za kujiunga na jeshi litakalokushindeni. Ni jeshi la Khilafah Rashida, na siku hiyo, vifua vya Waumini vitajaa furaha kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, na nyuso za madhalimu zitakuwa nyeusi
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Uturuki
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: http://www.hizb-turkiye.org |
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org |