Jumatatu, 14 Rabi' al-thani 1447 | 2025/10/06
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Onyo la Tom Barrack kwa Lebanon Dhidi ya “kuregea Bilad Al-Sham”!

Kukiri kwa Siri kwa Marekani kwamba Mradi wa Kuunganisha Ummah Kupitia Usimamishaji wa Khilafah ndio Hasimu Pekee wa Kweli wa Mradi wa Marekani katika Kanda hii

(Imetafsiriwa)

Mnamo 12 Julai 2025, katika mahojiano na Arab News, Mjumbe Maalum wa Marekani katika Mashariki ya Kati, Tom Barrack, alizindua mfululizo mpya wa taarifa zinazofichua mradi wa Marekani katika eneo hili na kuthibitisha kina cha mgogoro ambao utawala wa Marekani unakabiliana nao katika kutekeleza mradi wake wa “Mashariki ya Kati Mpya”. Barrack alifichua kwamba Marekani iliwezesha mazungumzo ya siri kati ya Lebanon na umbile nyakuzi la Kiyahudi: “Marekani iliwezesha mazungumzo ya nyuma ya pazia kati ya Lebanon na ‘Israel’... mambo yanakwenda kwa kasi kubwa!” Hata haraka zaidi, kulingana na yeye, ni mazungumzo kati ya serikali mpya ya Syria na Mayahudi: “Niliuona uhalisia kwamba Syria inasonga kwa kasi ndogo kuchukua fursa ya kihistoria iliyotolewa na @POTUS' kuondolewa kwa vikwazo: Uwekezaji kutoka Uturuki na Ghuba, mawasiliano ya kidiplomasia kwa nchi jirani.” Alionya kwamba ikiwa Lebanon haitaelekea kwenye suluhisho la Marekani, itaregea Al-Sham huku ikipunga karata ya mipaka na kitambulisho cha kisiasa, na kuonya juu ya hatima mpya ya Lebanon ikiwa haitafuata njia ya uhalalishaji mahusiano na kujisalimisha: “Trump alikuwa jasiri katika kuipa Syria nafasi, na kile kilichotokea tangu uingiliaji kati wa Magharibi na Sykes-Picot hakikuwa kizuri ...”, “Lebanon iko katika hatari ya “kuregea katika Bilad Ash-Sham” ikiwa itashindwa kuchukua hatua kwa haraka katika muundo mpya wa kieneo!” Ama kuhusu washirika wa Amerika kutoka kwa wachache ambao iliandaa kwao makongamano ya hivi karibuni na kuahidi vijidola vidogo hapa na pale sasa inawageukia, ikisema kupitia mjumbe wake: “Msimamo wa Amerika unakataa ufederali nchini Syria, na kusisitiza kwamba nchi hiyo lazima ibaki na umoja, na jeshi moja na serikali moja.” Aliendelea “Hakutakuwa na nchi sita. Itakuwepo Syria moja tu.” Akiondoa uwezekano wa kuasisi dola huru Kikurdi, Alawiye  au Druze. Na akaongeza: “Marekani haitoi masharti lakini haitaunga mkono matokeo ya utengano: Hatutakuwa huko milele kama yaya!” Katika ujumbe mkal i wa kidiplomasia ambao unapuuza ahadi zote na kujitolea kote, alitangaza kwa fahari “msamaha” kwa mashirika ambayo, hadi hivi karibuni, yaliitwa ya “kigaidi.” Aliiondoa kibandiko hicho kutoka kwa Hay'at Tahrir al-Sham (HTS) na akafungua mlango wa mazungumzo na chama cha Iran na silaha zake nzito, licha ya kubaki kwenye orodha ya “magaidi”! Hata alikipa mgongo chama cha SDF (Syrian Democratic Forces), ambacho kilikuwa kimemtumikia kwa miaka mingi akiwapa chaguo kati ya utiifu au kubadilishwa: “Hatuna deni lao la haki ya kuanzisha serikali huru ndani ya dola... ndio, tunawajibu wa kuwatendea haki... ikiwa hawana busara, basi ajenda badali inakuja kwenye ajenda!” Hii ndiyo mantiki ya siasa za Marekani: kazi kwa badala ya kubakia hai, kusalim amrti kwa badali ya uridhishaji Marekani! Na hii ndio Amerika isiyo na imani na isiyo na heshima.

Enyi Waislamu nchini Lebanon hasa, na Ash-Sham kwa jumla: Tunajua kwamba Marekani haijali kuhusu hatima ya Lebanon au Syria. Inaona watu wa eneo hilo kama ala tu na vibali vya mikataba na miungano yake. Kile ambacho Marekani inajali sana ni kulioanisha umbile la Kiyahudi katika eneo hili kama “mshirika wa asili,” huku ikisambaratisha mabaki ya umoja wa Ummah na kupora rasilimali zake hasa katikati ya mbio za kimataifa kwa ajili ya gesi na madini ya kimkakati, na mzozo wake wa kiuchumi na China. Kile amabcho Barack alisema kuhusu Lebanon kurudi Ash-Sham sio kutekeleza kwa ulimi, bali ni kauli yenye kina cha kimkakati. Inadhihirisha kwamba Marekani inaogopa Ummah kurudi kwenye asili yake, kwenye umoja wake, na kwenye mradi wake wa kisiasa wa Kiislamu. Ni kauli inayobeba vitisho na kukubali kwa wakati mmoja: tishio kwa wale wanaokataa suluhisho la Amerika la kuhalalisha mahusianio na kusalimu amri, ili wasirudi kwenye asili yao! Na kukiri kwamba asili hii ni umoja wa Ash-Sham, kwa hakika Umma wa Kiislamu kwa jumla bado uko hai katika fahamu za watu, umekita mizizi ndani ya ardhi, na umo ndani ya nafsi, licha ya miaka yote ya kutengwa na majaribio ya kufuta kitambulisho cha kweli cha eneo hili. Hii inaashiria kwamba Ummah bado ndani yake una cheche ya mwamko wa Kiislamu, na kwamba mradi wa Khilafah ambao unadhihirisha umoja wa Ummah, sio Ash-Sham tu, na ambao unapigwa vita na Marekani na Mayahudi bado ni tishio kubwa zaidi kwa udhibiti wao na maslahi yao katika eneo hili. Na tishio hili linatumiwa na Barrack na utawala wake kama kitisho cha kuwafanya ‘walio wachache’ waogope hatima yao chini ya njia hii badali, na hivyo kuwasukuma katika mikono ya mradi wa Marekani hata kufikia kiwango cha kuwafanya kuukubali kama mradi wao wenyewe.

Ama sisi katika Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Lebanon, tunaweza tu kujiona kama Hizb kuu ilio na wasiwasi na kauli kama hizo na tunazijibu kwa kujiamini kikamilifu:

• Mzozo mkuu katika eneo hili ni mapambano ya kihadhara kati ya Umma wa Kiislamu na nchi za kisela za kikafiri za Magharibi, mgongano wa maadili na fahamu za kihadhara. Magharibi kamwe haijaacha kufanya njama dhidi ya Ummah huu na kuukandamiza. Ukoloni wake ulianza kwa kuivunja Khilafah, na kufuatiwa na mgawanyiko na usambaratishaji. Tunatangaza kwamba ukoloni huu hautakwisha isipokuwa kwa kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ambayo Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliahidi kwamba itafuata utawala huu dhalimu wa sasa ambao mwisho wake tunaushuhudia, kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

• Kauli hizi, licha ya vitisho na kiburi vyake, zinaakisi ukweli mmoja wa wazi: mradi wa Kiislamu wa umoja, ulioonyeshwa kwa kusimamishwa kwa Khilafah kwa njia ya Utume, ndio unaozitia wasiwasi sana duara za ufanyaji maamuzi jijini Washington. Zinafanya upya hesabu zao za udhibiti na ushawishi katika eneo hili. Hata Mayahudi, kupitia kwa Netanyahu mwenyewe, wameeleza kwa uwazi kabisa hofu yao kuhusu Khilafah kuanzishwa katika mwambao wa Bahari ya Mediterania, na wameeleza nia yao ya kuishambulia popote itakaposimama.

• “Mchezo wa walio wachache” ambao Magharibi inacheza hivi sasa kama ilivyocheza hapo awali kuiangusha Dola ya Kiislamu (Khilafah) unaelekezwa kwa wasiokuwa Waislamu, ambao Waislamu wanawazingatia kuwa raia wa dola ya Kiislamu: “Wana haki na wajibu sawa na Waislamu.” Watu hao walio wachache waliishi chini ya utawala wa Kiislamu hapo awali na hawakupata dhulma. Wengi wao hata walisifu utawala wa Kiislamu. Tunapozingatia alichosema Barrack katika kutishia SDF na wengine anaowaita “walio wachache” kwamba wasipozingatia ajenda yake, watapata tabu – tunaona kwamba ameianika wazi serikali yake kuwa ndiyo inayowatumia watu hawa kwa maslahi yake binafsi, sio yao, kama inavyodai kwa uongo! Hii inaonyesha tofauti kubwa kati ya Uislamu ulivyowatendea walio wachache na ile ya Marekani na Magharibi. Historia ni shahidi mkuu na mfuchuzi mkuu.

Enyi Waislamu: Mradi wa Kiislamu wa kuunganisha Ummah yaani, Khilafah kwa njia ya Utume sio hofu ambayo Marekani na wajumbe wake wanajaribu kuionyesha. Badala yake, ni mradi wa maisha yenye adhama, heshima, na haki. Barrack, iwe anatambua hilo au la, amefichua kwamba mradi huu wa kisiasa wa Kiislamu Khilafah ndio hasimu pekee wa kweli wa mradi wa Marekani, na kwamba hofu ya kweli jijini Washington na miongoni mwa Mayahudi ni kutokana na kurudi kwa Khilafah ambayo itaunganisha Ummah na kukomesha utumwa.

Enyi Waislamu: Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Lebanon tunawalingania muunde mustakabali wenu wenyewe kwa mikono yenu wenyewe, sio kwa mikono ya Magharibi, wala kwa makongamano ya njama, wala kwa vitisho na kauli za mabalozi na wajumbe.

Kuweni kama alivyokukusudieni Mwenyezi Mungu muwe: Umma mmoja, sio wa Mashariki wala wa Magharibi, unaoongoza, usioongozwa; kutawala kwa Uislamu, sio kwa mifumo ya Sykes-Picot.

Iregesheni Lebanon kwa mikono yenu mwenyewe kwenye asili yake halisi – sehemu ya Ash-Sham, na kwa upana zaidi, sehemu ya ardhi za Waislamu na muwe Ummah wa uadilifu ambao Mwenyezi Mungu Mtukufu aliusifia:

[وَكَذَلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطاً لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيداً]

“Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.” [Surah Al-Baqarah: 143].

H. 20 Muharram 1447
M. : Jumanne, 15 Julai 2025

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Lebanon

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu