Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  1 Rabi' II 1446 Na: HTS 1446 / 12
M.  Ijumaa, 04 Oktoba 2024

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
(Imetafsiriwa)

Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema:

[وَلَنَبْلُوَنَّكُم بِشَيْءٍ مِّنَ الْخَوْفِ وَالْجُوعِ وَنَقْصٍ مِّنَ الْأَمْوَالِ وَالْأَنفُسِ وَالثَّمَرَاتِ وَبَشِّرِ الصَّابِرِينَ * الَّذِينَ إِذَا أَصَابَتْهُم مُّصِيبَةٌ قَالُوا إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ * أُولَئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ وَأُولَئِكَ هُمُ الْمُهْتَدُونَ]

“Hapana shaka tutakujaribuni kwa chembe ya khofu, na njaa, na upungufu wa mali na watu na matunda. Na wabashirie wanao subiri, Wale ambao ukiwasibu msiba husema: Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea. Hao juu yao zitakuwa baraka zitokazo kwa Mola wao Mlezi na rehema. Nao ndio wenye kuongoka.” [Al-Baqrah:155 - 1].

Baada ya kukubali Qada’a ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan yamuomboleza:

Sheikh Alim Ahmad Al-Hussein Muhammad Ahmad Mudawi

Mmoja wa Mashababu wake aliyebeba Dawah ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, akistahamili madhara ya madhalimu jeuri mpaka yakini ilipomjia jana, Alhamisi, tarehe 30 Rabi ' al-Awwal 1446 H, sawia na 3/10/2024, kwenye Kisiwa cha Tuti jijini Khartoum.

Mwenyezi Mungu amrehemu Sheikh Alim Abu Abdul Mun'im, amsamehe, na amjaalie Firdaws ya juu katika Jannah.

Ajaaliye kaburi lake liwe bustani miongoni mabustani ya Jannah. Alijulikana kwa kufunga na kusimama katika swala, kipenzi miongoni mwa watu wake, kiasi ambacho walikuwa wakisema kuwa yeye ni Swahaba. Alikuwa mkarimu na mtukufu.

Macho yanabubujika machozi, moyo unahuzunika, na tumehuzunishwa sana na kuondoka kwako, ewe Abu Abdul Mun'im, lakini hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mola wetu:

[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ] “Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqra:156].

Rambirambi zetu ziende kwa familia yake, jamaa na ndugu zake katika Dawah.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 0912240143- 0912377707
http://www.hizb-sudan.org/
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu