Alhamisi, 19 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/21
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Sudan

H.  16 Rajab 1444 Na: HTS 1444 / 30
M.  Jumanne, 07 Februari 2023

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan Wakutana na Rais wa Baraza la Fiqh ya Kiislamu
(Imetafsiriwa)

Ujumbe kutoka Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Sudan, ukiongozwa na Ustadh Ibrahim Othman (Abu Khalil) - Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Sudan, akifuatana na Ustadh Abdullah Hussain - Mratibu wa Kamati Kuu ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Sudan, na Ustadh Khalid Al Noor - Mwanachama wa Hizb ut Tahrir, walikutana na Baraza la Fiqh ya Kiislamu jijini Khartoum, Dkt. Abd Al-Rahim Adam Muhammad - Rais wa Baraza, na Mhandisi Al-Zubair Muhammad Ali - Katibu Mkuu wa Uimarishaji wa Fikra katika Baraza. Hii ikiwa ndani ya wigo wa mikutano ya Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Sudan na viongozi wa jamii, wasomi, wanasiasa na wengineo, kama sehemu ya kampeni ya hizb ya kutokomeza mihadarati.

Baada ya kuukaribisha ujumbe huo, mkuu wa ujumbe huo, Ustadh Abu Khalil, alizungumzia madhumuni ya mkutano huo, na kwamba uliingia ndani ya wigo wa kampeni ya Hizb iliyozinduliwa katika Shirika la Habari la Sudan (SUNA) kupambana na mihadarati, akionyesha kuwa mihadarati ni njia mojawapo ya vita vya kisasa, ambavyo ni vita vya kizazi cha tano, na kwamba tangu mwaka 2013, dawa za kulevya zimekuwa zikifurika Sudan, ili kuharibu fikra za vijana wanaotegemewa kwa mabadiliko ya kweli, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Abu Khalil pia alionyesha ukosefu wa umakini wa serikali katika kupambana na mihadarati. Badala yake, mkuu wa Baraza Kuu, Al-Burhan, anapeana mikono na mhalifu muuaji Cohen, waziri wa mambo ya nje wa umbile la Kiyahudi, akijua kuwa dola ya Kiyahudi inahusika katika kuisheheni Sudan kwa dawa za kulevya, na kwa hivyo haipasi kuitegemea serikali hii ili kuondoa dawa za kulevya, bali ni lazima tufanye kazi ya kusimamisha dola ya Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, ili vijana na jamii ihifadhiwe, kupitia kuondoa madawa ya kulevya na maovu yote mara moja.

Kisha Dkt. Abd Al-Rahim akazungumza, akisema: Nyinyi pekee ndio mnaojua dori ya baraza hili, na kwa hilo tunawashukuru kwa ziara hii, na kwa juhudi mnazozifanya katika suala hili, kuashiria kwamba wao pia wana mipango katika mapambano dhidi ya mihadarati. Kisha akampa nafasi Ndugu Al-Zubayr - Katibu Mkuu wa Uimarishaji Fikra katika Baraza, ambaye alieleza kwa kina mipango wanayoifanya.

Kwa kumalizia, mkuu wa Baraza la Fiqh ya Kiislamu alikubali kwamba kukabiliana na tishio hili la Magharibi kunaweza tu kufanywa na dola yenye nguvu, ambayo ni Dola ya Khilafah. Ndugu Abdullah Hussain aliwasilisha baadhi ya machapisho yanayohusiana na suala la madawa ya kulevya yaliyotolewa na hizb, pamoja na matoleo ya Jarida la kila wiki la Ar-Raya linalotolewa na Hizb ut Tahrir.

Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu