Ijumaa, 25 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/27
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina

H.  28 Sha'aban 1443 Na: BN/S 1443 / 13
M.  Alhamisi, 31 Machi 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi kutoka Kizazi cha Kwanza cha Hizb ut Tahrir

[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً]

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzaab: 23]
(Imetafsiriwa)

Hizb ut Tahrir katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina inamuomboleza mmoja wa wanaume wa Hizb ut Tahrir, mbebaji Dawah kutoka kizazi cha kwanza katika safu zake, mtu mwema kutoka mji wa Al-Khalil. Marhum kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt):

Al-Hajj Tahir Abdul Razzaq Al-Ju’bah (Abu Muhammad)

Aliyekwenda kwenye rehma za Mwenyezi Mungu (swt) asubuhi ya leo Alhamisi, 31/3/2022. Al-Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, alitumia maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu na kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida kwa njia ya Utume, popote alipoishi na kusafiri. Yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alikuwa mstari wa mbele kuubeba ulinganizi huu. Alifanya kazi ya kusimamisha dola ya Uislamu na kuzungumza juu ya ufaradhi wake katika darsa zake misikitini, katika mikusanyiko yake, na hotuba yake. Alifahamika, Mwenyezi Mungu amrehemu, kwa bidii yake ya kuhudhuria na kushiriki katika amali nyingi za Dawah katika Ardhi Iliyobarikiwa hadi alipolemazwa na maradhi na uzee.

Inashuhudiwa kwamba yeye, Mwenyezi Mungu amrehemu, alitabanni maslahi ya watu na akapigania mambo yao. Al-Hajj alikuwa mtu mashuhuri katika familia yake na katika mji wa Al-Khalil. Alijulikana kwa kupatanisha watu, akitumia wakati na bidii yake kuzuia umwagaji damu na kutatua mizozo. Alishiriki hata katika hatua za mwisho za kutatua tatizo kubwa miezi iliyopita katika mji wa Al-Khalil. Alihudhuria huku ikiwa ni vigumu kusimama kwa miguu yake.

Mwenyezi Mungu ambariki marehemu wetu kwa rehma zake kubwa, na amjaalie maskani yake katika Mabustani yake makubwa, Inna Lilah Wa Inna Ilaihi Raji’uon, “Sisi ni wa Mwenyezi Mungu na kwake Yeye tutarejea”. Mwenyezi Mungu awalipe malipo makubwa jamaa zake na awajaalie subira na faraja, tunamuomba Mwenyezi Mungu aijaalie Qur’an Tukufu kuwa ni muombezi wake siku ya kiama. Al-Hajj, Mwenyezi Mungu amrehemu, amekichukua Kitabu cha Mwenyezi Mungu kuwa ni mwandani wa karibu, ambapo hakukiacha tangu maradhi yake yamfungie nyumbani kwake. Hatusemi ila yanayomridhisha Mwenyezi Mungu. Ni cha Mwenyezi Mungu alichokitoa na ni cha Mwenyezi Mungu alichokichukua, kila kitu kwake kimewekwa kwa muda maalumu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Ardhi Iliyobarikiwa – Palestina

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Ardhi ya Baraka-Palestina
Address & Website
Tel: 

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu