Ijumaa, 10 Rabi' al-awwal 1446 | 2024/09/13
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  7 Safar 1445 Na: 1445 / 07
M.  Jumatano, 23 Agosti 2023

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Hotuba ya Modi Siku ya Uhuru wa India ni Tangazo Kuhusu Kuchukua Uongozi wa Kanda. Ima Tusimamishe Khilafah au Tuwe Watumwa wa Dola ya Kibaniani

(Imetafsiriwa)

Akizungumza katika Siku ya Uhuru wa Dola ya Kibaniani, Mchinjaji wa Gujarat na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, alisema, "Sote tunajua kwamba nchi yetu ilivamiwa (na Waislamu) miaka 1200 iliyopita. Jimbo dogo (Sindh) na mfalme wake (Raja Dahir) walishindwa. Lakini, sisi (Mabaniani) hatukujua kwamba tukio hili moja lingeitumbukiza India katika miaka elfu moja ya utumwa. Tulikuwa tumekwama kwenye kinamasi cha utumwa. Kila aliyekuja, alitupora na kututawala. Ni milenia yenye msiba ilioje hii.”

Modi aliongeza, "Nina hakika kabisa kwamba kama vile mfumo mpya wa ulimwengu ulivyoanzishwa baada ya Vita vya Pili vya Dunia, mfumo mpya wa ulimwengu, mpangilio mpya wa dunia, mlingano mpya wa kisiasa wa kijiografia unazaliwa baada ya Corona. Mtajivunia kuwa ulimwengu unatambua talanta za wananchi wangu bilioni 1.4. Mumesimama katika hatua muhimu ya mabadiliko.”

Kwa hivyo, Siku ya Uhuru wa India, Modi alitangaza kuwasili kwa mfumo mpya wa ulimwengu. Kwa baraka za wakoloni. Dola ya Kibaniani inapaswa kuchukua udhibiti wa kanda hii. Italipiza kisasi kwa Waislamu kwa milenia yao ya utawala. Modi tayari ameanza mradi huu. Basi, je, tuna njia gani nyingine zaidi ya kusimamisha Khilafah?

Baada ya serikali ya BJP kuoanisha Dola ya Kibaniani na agizo la Marekani, Marekani imekuwa mshirika mkuu wa Dola ya Kibaniani. Marekani imebadilisha kabisa mienendo ya zamani ya kanda. Marekani iliwahi kutoa msaada kwa Pakistan dhidi ya Dola ya Kibaniani. Pakistan iliwahi kuwa kibaraka muhimu zaidi wa Marekani katika eneo hilo. Pakistan ilitimiza matakwa ya Marekani, kuanzia kufungua milango kwa China, hadi kuwezesha uvamizi wa Afghanistan. Hata hivyo, leo hii, Marekani inaichukulia China ya sasa na Khilafah itakayosimamishwa hivi karibuni kama matishio makuu ya kimkakati ya kikanda.

Marekani inaichukulia Dola ya Kibaniani kama mshirika wake dhidi ya China na Waislamu. Haijalishi ni kiasi gani serikali ya Pakistan inaibembeleza Marekani, lengo la kimkakati la Marekani ni kuidhoofisha Pakistan na Waislamu. Tayari imechukua hatua nyingi kuhakikisha hilo. Marekani ilitumia FATF kuondoa mashirika ya wanajihadi wa Kashmiri. Ilitumia IMF kuangamiza uchumi wa Pakistan. Imehakikisha kuendelea kupunguzwa kwa bajeti ya kijeshi katika hali halisi. Imehakikisha kupunguzwa kasi ya kuundwa kwa makombora na silaha zengine za kimkakati. Inaligeuza jeshi shujaa na lenye nguvu la Pakistan kuwa jeshi la kupambana na ugaidi.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan! Uongozi wa Pakistan unafuata maagizo ya Marekani. Unaigeuza Pakistan kuwa kibaraka wa Dola ya Kibaniani kwa badali ya kiti chake cha enzi. Hata hivyo, ina hofu kwamba hamtaruhusu hilo. Kwa hivyo, inachukua hatua kwa busara.

Uongozi wa Pakistan unafanya mazungumzo ya siri na India. Umejiwekea mipaka kwa shutma za umma, baada ya kuunganishwa kwa lazima kwa Kashmir na Modi. Ulimpa Modi zawadi ya kusitisha mapigano kwenye Mstari wa Udhibiti. Ulifungua Ukanda wa Kartarpur. Uliruhusu mashirika ya ndege ya India kuruka kupitia anga ya Pakistan. Uliruhusu biashara ya bidhaa nyingi za India. Unanyamaza kimya juu ya uvamizi wa Kashmir. Unatuma timu ya michezo ya Pakistan kwenda India ili kuendeleza uhalalisha mahusiano zaidi. Haukupatiliza fursa ya kuhamishwa kwa kikosi cha mashambulizi cha India kutoka mpaka wa Pakistan hadi China. Unabadilisha mizani ya kijeshi kati ya Pakistan na India mara kwa mara. Unavunja moyo majeshi yetu na watu wetu katika kujisalimisha, kupitia kuwasilisha "ushahidi" wa ukuu wa Dola ya Kibaniani.

Ni wazi kwa wanaofahamu kwamba Demokrasia, mifumo mseto, udikteta, utawala wa kiteknolojia na serikali za muda zote zimefeli. Wakati umewadia sasa wa kuifanya Afghanistan kuwa sehemu nyeti na muhimu ya Khilafah iliyosimamishwa nchini Pakistan, chini ya ruwaza pana ya Uislamu, badala ya "kina cha kimkakati," chini ya ajenda finyo ya utaifa. Nchi za Asia ya Kati kuwa sehemu ya Khilafah itakuwa ni hatua ya kimaumbile inayofuata. Upanuzi wa Khilafah hadi Ghuba utakuwa "mshindo mkubwa" kwa Dola ya Kibaniani. Huu utakuwa ndio mwanzo wa kuunganisha Ulimwengu wa Kiislamu na kuitupa Marekani nje ya kanda hii. Wanajeshi na maafisa wa Jeshi la Pakistan wako tayari kwa misheni hii kuu.

Enyi Waislamu wa Majeshi ya Pakistan! Toeni Nusrah kwa Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Ni baada ya hapo tu ndipo tunaweza kuanza misheni hii kivitendo. Khilafah ndio chaguo pekee litakalotuokoa kutoka katika utumwa wa Dola ya Kibaniani. Ndiyo njia pekee ya Shariah ya kusimamisha tena utawala wa Uislamu juu ya Bara Ndogo lote la India. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[إِنَّهُمۡ يَرَوۡنَهُۥ بَعِيدٗا وَنَرَىٰهُ قَرِيبٗا]

“Hakika wao wanaiona iko mbali, Na Sisi tunaiona iko karibu.” [Surah Al-Ma’arij 70:6-7].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu