Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
H. 10 Safar 1445 | Na: 1445 / 10 |
M. Jumatatu, 25 Septemba 2023 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Huku Ongezeko Kubwa katika Viwango vya Riba Likiangamiza Uchumi, Benki Zinafaidika Pakubwa
(Imetafsiriwa)
Ripoti ya ukaguzi wa nusu ya mwaka wa Benki Kuu ya Pakistan, iliyochapishwa mnamo 18 Septemba 2023, ilifichua kwamba faida ya mabenki ilikuwa rupia bilioni 126 katika nusu ya kwanza ya mwaka uliopita. Imeongezeka zaidi ya maradufu, hadi rupia bilioni 284 katika nusu ya kwanza ya mwaka huu. Sababu kuu ya hili inatangazwa kama kuongezeka kwa viwango vya riba.
Kwa miaka michache iliyopita, serikali ya Pakistan imekuwa ikichapisha sarafu kwa kiwango kikubwa. Inatoa pesa hizi kwa mabenki na kisha kuziondoa kwa viwango vya juu vya riba kutoka kwa mabenki haya. Inasimamia nakisi yake ya bajeti ya fedha kwa njia hii ya uharibifu. Katika kipindi kati ya 1 Julai 2022 na 2 Juni 2023, serikali ya majimbo imechukua mikopo ya rupia bilioni 3,216 kutoka mabenki. Watawala hawasitishi uchapaji wa sarafu nyingi. Badala yake, wanaongeza faida za wawekezaji katika riba, kwa kuongeza viwango vya riba. Machakato huu umeyageuza mabenki kuwa mashini za pesa kwa wawekezaji. Hii ni kwa sababu ya deni kubwa kwa upande mmoja, na viwango vya juu vya riba kwa upande mwingine. Benki zinazalisha faida mara mbili na mara nne hapo kwa hapo, kutokana na mapato haya ya riba.
Mwaka huu, serikali inalipa rupia bilioni 2,000 kwa mitambo ya nguvu za umeme ya kibinafsi kama malipo ya kiwango cha uzalishaji umeme. Mgao wa simba wa kiasi hiki utalipwa kwa mabenki kama malipo ya riba. Lengo kuu la kuweka mzigo mkubwa wa ushuru kwenye bili za umeme ni malipo ya riba ya serikali. Kwa njia hii, Ummah unakandamizwa kutoka pande zote. Katika wakati ambapo viwango vya juu sana vya riba vimelemaza sekta zote za uchumi, ikiwemo viwanda, biashara na kilimo, faida za mabenki ni kubwa mno. Kwa hivyo, utajiri wa jamii nzima unajilimbikiza mikononi mwa wachache. Matokeo yake, Ummah na uchumi unaharibiwa.
Ni thabiti katika Uislamu kwamba Riba ni dhambi kubwa na laana. Imesimuliwa kutoka kwa Abdullah bin Masud (ra) kwamba Mtume (saw) amesema,
«لَعَنَ اللَّهُ آكِلَ الرِّبَا وَمُوكِلَهُ وَشَاهِدَيْهِ وَكَاتِبَهُ قَالَ وَقَالَ مَا ظَهَرَ فِي قَوْمٍ الرِّبَا وَالزِّنَا إِلَّا أَحَلُّوا بِأَنْفُسِهِمْ عِقَابَ اللَّهِ عَزَّ وَجَلَّ»
“Mwenyezi Mungu amemlaani mlaji riba, na mwenye kutoa, na mashahidi wake wawili, na mwenye kuiandika. Akasema riba na zinaa hazitodhihiri miongoni mwa watu, isipokuwa watu hao wamejihalalishia nafsi zao adhabu ya Mwenyezi Mungu Azza wa Jal.” (Musnad Ahmad).
Yeyote anayekula riba hunyimwa mafanikio Akhera. Kwani Mwenyezi Mungu (swt) amesema,
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَأْكُلُوا الرِّبَا أَضْعَافًا مُّضَاعَفَةً وَاتَّقُوا اللَّهَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ]
“Enyi mlio amini! Msile riba mkizidisha juu kwa juu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mpate kufanikiwa.” [Surah Aali-Imran 3:130].
Mfumo wa kirasilimali wa kidemokrasia wenyewe ni laana. Unaruhusu miamala ya riba inayotuzamisha katika deni lolote. Mafanikio katika ulimwengu huu na akhera hayawezekani kwa Waislamu chini ya mfumo huu wa kidemokrasia. Kwa kuwepo mfumo huu usio wa kikafiri, aina yoyote ya juhudi za ustawi hazipunguzi mateso yetu. Badala yake, tunateseka zaidi na zaidi. Tunaburutwa mbali zaidi na mafikio yetu halisi, ya ufanikisi na mafanikio. Wakati umewadia sasa wa kuuzika mfumo huu wa kikafiri nchini Pakistan na kusimamisha Khilafah kwa Njia ya Utume. Itamaliza kudumaa kwa uchumi wa nchi hii kupitia kukomesha riba, na hivyo kumaliza mrundiko wa utajiri mikononi mwa wale wanaofanya biashara katika deni.
Mwenyezi Mungu (swt) amesema,
[وَمَاۤ اٰتَيۡتُمۡ مِّنۡ رِّبًا لِّيَرۡبُوَا۟ فِىۡۤ اَمۡوَالِ النَّاسِ فَلَا يَرۡبُوۡا عِنۡدَ اللّٰهِ]
“Na mnacho kitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Mwenyezi Mungu.” [Surah Al-Rum 30: 39].
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Pakistan |
Address & Website Tel: https://bit.ly/3hNz70q |