Alhamisi, 19 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/09/11
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Hizb ut Tahrir / Sweden: Kisimamo “Mauaji dhidi ya Raia mjini Gaza hivi sasa! Simama kwa Heshima!”

Kufuatia kukiuka makubaliano duni ya usitishaji mapigano ya umbile la Kiyahudi mnamo siku ya Jumanne, 18/03/2025, na kuanza tena kwa mauaji ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao ni wanawake, watoto na wazee, Hizb ut Tahrir / Sweden iliandaa kisimamo katika robo ya Waislamu wa mji mkuu, Stockholm, chenye kichwa “Mauaji dhidi ya Raia mjini Gaza hivi sasa! Simama kwa Heshima!”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Matembezi ya Ukombozi: “Enyi Majeshi (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?”

Matembezi yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 28 Machi 2025 sawia na tarehe 28 Ramadhan 1446 kuanzia Msikiti wa Al-Fath yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia kuinusuru Gaza dhidi ya uadui wa Marekani Mzayuni, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunis na kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu kutoka Tunisia ya kijani. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likisomeka, “Enyi majeshi! (Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi?)”

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan: Enyi Jeshi la Pakistan! Songeni kwa ajili ya Kuinusuru Gaza, kwa Kumtii Mwenyezi Mungu!

Televisheni ya serikali ya Pakistan ilisema mnamo 19 Machi 2025: “Pakistan inalaani vikali mashambulizi ya anga ya Israel.” Hivi ndivyo watawala wa Pakistan walivyolaani hujuma ya Mayahudi na jinai zake zinazoendelea dhidi ya Ukanda wa Gaza! Bila kusonga askari au kuinua silaha!

Soma zaidi...

Hizb ut Tahrir / Uholanzi: Matembezi Jijini Amsterdam “Harakati kwa ajili ya Gaza!”

Kufuatia umbile halifu la Kiyahudi kukiuka makubaliano dhaifu ya kusitisha mapigano alfajiri ya Jumanne, Machi 18, 2025, na kuanza tena mauaji ya kimpangilio ya Waislamu wasio na ulinzi, ambao wengi wao ni wanawake, watoto, na wazee, Hizb ut Tahrir / Uholanzi iliandaa matembezi na kisimamo cha halaiki katika mji mkuu wa Uholanzi, Amsterdam, kwa kichwa: “Harakati kwa ajili ya Gaza!”

Soma zaidi...

Hotuba ya Amiri wa Hizb ut Tahrir, Mwanachuoni Mkubwa, Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah kwa Wanaozuru Ukurasa wake kwa Mnasaba wa Idd ul Fitr iliyobarikiwa ya Mwaka 1446 H sawia na 2025 M

Ndugu na Dada Wapendwa: Idd hii inakuja na dola ovu ya Kiyahudi inafanya ukatili dhidi ya watu, miti na mawe huko Gaza na Palestina yote, inafanya hivyo kwa msaada wa Marekani, ambayo inaipatia mabomu, makombora na ndege. Ingawa si ajabu kwamba umbile la Kiyahudi kwa kuungwa mkono na Marekani linatekeleza hili, kwani wao ni adui wa Uislamu na Waislamu, lakini cha ajabu ni kwamba hakuna hata mmoja wa watawala katika nchi za Kiislamu anayechukua hatua, hasa wale walioko pambizoni mwa Palestina, ili kuyakusanya majeshi yao kuinusuru Gaza, watu wake, Al-Aqsa, na viunga vyake, na kuling'oa umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mizizi yake, na kisha kuiregesha Palestina yote kwa watu wake. Je, yule anayeikalia kwa mabavu ardhi ya Kiislamu na akawatoa watu wake humo hastahiki kupigwa vita na majeshi ya Waislamu na kufukuzwa humo kama walivyowafukuza watu wake?

Soma zaidi...
Jiunge kwa hii RSS feed

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu