Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
H. 4 Muharram 1447 | Na: 1447 / 02 |
M. Jumapili, 29 Juni 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya')
[مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)
Kwa imani kamili juu ya qadhaa ya Mwenyezi Mungu na kutaka malipo kutoka Kwake, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Jordan inaomboleza kwa kuondokewa na mmoja wa wabebaji wake wa Da’wah: Ustadh Yusuf Dhiab Al-Shalabi (Abu Diya'), ambaye alifariki dunia kwenda kwenye rehema za Mwenyezi Mungu Mtukufu mnamo Alhamisi, tarehe 1 Muharram 1447 H sawia na 26 Juni 2025 M, akiwa na umri wa miaka 89, baada ya kuugua kwa muda mrefu ambapo alikuwa na subira na kwa kutarajia malipo ya Mwenyezi Mungu.
Abu Diya’ alitumia miaka ya maisha yake kujitahidi, kutangaza haki, na kujishughulisha kikamilifu katika kila mnasaba uliohitaji ujasiri katika kubeba dawah, kwa kutumia Kiarabu chake fasaha cha kale, ambapo alikijua vyema na kukifundisha. Alifuatilia kwa bidii mambo ya Umma wa Kiislamu, bila kuogopa lawama katika njia ya Mwenyezi Mungu.
Azma yake kamwe haikuyumba licha ya kuandamwa, kufungwa, na kunyanyaswa, wala ugonjwa wake haukumzuia hadi miaka ya mwisho kabisa ya maisha yake. Mwenyezi Mungu ammiminie rehema pana ndugu yetu mwendazake, amlaze mahala pema peponi, atukuze malipo ya familia yake na wapenzi wake, na awape subira na faraja. Hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu: Ni cha Mwenyezi Mungu Anachokichukua na ni Chake Anachotoa, na kila kitu kiko Kwake kwa kipimo.
[إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |