Jumatano, 07 Muharram 1447 | 2025/07/02
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  1 Muharram 1447 Na: 1447 / 01
M.  Alhamisi, 26 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Jinsi Dola Kubwa Zinavyozaliwa Utotoni mwao
(Imetafsiriwa)

Ni kweli kwamba dola kubwa hazizaliwi ghafla mara moja, lakini hakuna shaka kwamba zinajengwa juu ya itikadi ambayo kwayo mfumo huchipuka. Wakati wa kuzaliwa kwake, fikra yake ilijumuishwa katika kundi ambalo lilijitolea mhanga mali zake za thamani zaidi na kuiunga mkono kivitendo ndani yake. Hili lilizaa dola yake, ambayo ilijizatiti kujitengenezea njia kuelekea uongozi wa kimataifa kwa msingi wa itikadi yake, kufikia haki na rehema kulingana na viwango vya asili ya kimungu katika miongo michache tu. Ni lazima kwa Ummah ambao kwa hakika unataka kurudisha nafasi yake ya hadhi miongoni mwa mataifa, si tu duniani kote, kuregea kubeba ujumbe wake kwa ulimwengu na kulazimisha uongozi wake wa kifikra na utawala wake juu ya fikra za dhulma, ubabe, na utumwa, na kufikia ukombozi wa kifikra na wa kimada. Umma huu lazima uvuke hisia, mambo ya kijuujuu, na lugha ya maneno hadi vitendo.

Njia ya kusimamisha dola kama hiyo ni rahisi sana na sifa zake ziko wazi sana, hasa ikiwa dola hii ilikuwa imesimamishwa hapo awali na ilikuwa imefikia hadhi kubwa miongoni mwa dola kwa zaidi ya karne kumi, na maelezo na hatua za kuanzishwa kwake na kanuni ambazo juu yake ilijengwa zilipitishwa kwa vizazi kwa kipindi cha muda. Hivyo basi, dola kubwa tunayoizungumzia ikazaliwa, na hii ndiyo njia iliyofuatwa na kiongozi wake, Muhammad (saw) na maswahaba zake, Mwenyezi Mungu awe radhi nao, katika kuisimamisha baada ya Yeye (saw) kupata nusra ya watu wa Yathrib. Ni njia madhubuti inayopelekea kwenye lengo la kusimamisha dola ya Kiislamu kwa sababu ni wahyi kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt).

Umma wa Kiislamu, Ummah bora kabisa ulioletwa kwa ajili ya wanadamu, unapitia miaka yake migumu zaidi katika zaidi ya karne moja. Ardhi zake zimekiukwa na kukaliwa kimabavu, rasilimali na utajiri wake kuibiwa, na watu wake huko Gaza na Ukingo wa Magharibi wanaangamizwa kila siku kwa miaka miwili. Watu binafsi, makundi, na nchi zimejiweka mbali na Uislamu na utekelezaji wa hukmu zake, na kumuasi Mwenyezi Mungu imekuwa ni jambo dogo kwao. Fahamu ya udugu katika Dini imerudi nyuma na imejikita kwenye hisia tu, mbele ya vitambulisho vibovu vya utaifa na kabila ambavyo vimeugawanya badala ya kuuunganisha, na kuutumbukiza kina cha chini kabisa. Haya ni mafungamano ambayo Uislamu umeharamisha na pandikizwa na mkoloni kafiri Magharibi kupitia tawala ambazo zimesaliti Dini na watu wao. Iliwateua kutekeleza misheni hizi za kishetani na kuwaundia duara potovu za kisiasa za aina hiyo hiyo. Hivyo basi, mambo ya Waislamu yanatawaliwa na Kafiri Magharibi, ambayo huanzisha vita dhidi ya nchi zao na kuvisimamia kwa zana zake ipendavyo na kuvimaliza inapotaka kulingana na maslahi yake, kama tulivyoona katika vita vya hivi karibuni kati ya Iran na umbile la Kiyahudi.

Kisha Waislamu, huku wakitamani kutoka katika matatizo haya na masuala ambayo yameangamiza nafsi zao na kuwafanya wajisikie wanyonge na wadhalilifu, wanauliza juu ya utatuzi wa masuala yao msingi na ya matagaa. Sio kwa sababu ya utambuzi wao kwanza kwamba wanaishi katika hali halisi ya kifisadi inayohitaji mabadiliko ya kina, makubwa, kwa sababu masuluhisho ya kivipande - kama vile mageuzi na kujitambulisha na uhalisia wa watawala wao - hayana maana na yanarefusha tu muda wa ufisadi. Uvamizi wa kithaqafa wa Kimagharibi umeenea katika njia yao ya kufikiri na tabia, uhalisia ambao unazidi kukua kwa uharibifu wa uhusiano wa Umma na Uislamu na kuufanya kuwa mtawala wa mambo yao. Ni lazima kuharibu uhusiano huo na kukata fungamano lolote kati ya Ummah na watawala wake na kuwatenga na duara zao za kisiasa kwenye serikali.

Kuwepo kwa vyama vya kisiasa vyenye ufanisi katika Ummah vinavyotabanni fikra ya Uislamu na njia yake ya mabadiliko, ambayo Hizb ut Tahrir ni ya kipekee ndani yake, kuna dori kubwa zaidi katika kuufanya Ummah kubeba itikadi yake na kuunda kiota maarufu kwa rai jumla kwa ajili ya kufanya maregeo ya dola ya Khilafah kuwa kadhia yao nyeti. Hii inahitaji kujitolea na mapambano kwa ajili ya mabadiliko msingi yanayotarajiwa, pamoja na wale wanaofanya kazi kwa ajili ya kuregesha dola yao ambayo imetoweka kwa karne moja. Wajibu huu ni faradhi kwa Ummah kwa ujumla wake, si kwa chama peke yake, ambacho kinatafuta pamoja na Ummah na kupitia kwao kujenga dola mpya ya Kiislamu na sio tu kuchukua madaraka. Kisha Uislamu hautakuwa na ushawishi ndani ya serikali na badala yake nyuso zitabadilishwa kwa nyengine, kama ilivyotokea hivi karibuni, na mahusiano na sera zitabaki kama wanavyotamani makafiri na hali ya Waislamu itabaki kama ilivyo, hatima zao kudhibitiwa na vikosi vya ukafiri, ubabe, na ufuska!

Enyi Waislamu: Enyi mnaoadhimisha mwaka uliobarikiwa wa Hijra ya Mtume, ni haki yenu kujua kwa nini tarehe ya Hijra ilikuwa tukio adhimu zaidi katika historia yenu. Ilikuwa ni mabadiliko ya Uislamu kutoka kwa nadharia kwenda kwa vitendo, chini ya kivuli cha dola kuu ambayo Mtume (saw) aliisisi mjini Madina, na akaisafisha ndani yake Bara Arabu kutokana na aina zote za ushirikina. Alianza kupeleka ujumbe wa Uislamu kwa ulimwengu, na akafuatiwa na Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Khilafah hii ilikuwa ni mfano wa kuigwa wa utawala na idara, ndani na nje ya nchi, pamoja na mazingira yake ya kisiasa ya Maswahaba, Mwenyezi Mungu awe radhi nao.

Kwa hivyo, Enyi Waislamu: Ikiwa kweli mnataka heshima, utu, ushindi, na ukombozi kutoka kwa ukoloni, watawala wenu dhalimu, na sheria dhalimu za kimataifa, basi lazima mtekeleze kivitendo kile ambacho Hijrah ilikuwa kwa ajili yake, ambayo ni kusimamishwa kwa dola ya Kiislamu. Hizb ut Tahrir imeeleza jinsi ya kuisimamisha, basi fanyeni kazi nayo kuisimamisha. Ni kwa njia hii tu ndipo Hijrah itakuwa na maana ya halisi na ya kivitendo. Hivyo itazaliwa dola kubwa, ambayo itapigana dhidi ya vikosi vya ukafiri na uvamizi na itakuwa ni hasimu  mkuu, na ushindi utaandikiwa juu yenu, Mwenyezi Mungu akipenda, kama ilivyozaliwa dola kubwa iliyoanzishwa na Mtume wa Uongofu na Rehema (saw).

[وَنُرِيدُ أَن نَّمُنَّ عَلَى الَّذِينَ اسْتُضْعِفُوا فِي الْأَرْضِ وَنَجْعَلَهُمْ أَئِمَّةً وَنَجْعَلَهُمُ الْوَارِثِينَ]

Na tukataka kuwafadhili walio dhoofishwa katika nchi hiyo na kuwafanya wawe waongozi na kuwafanya ni warithi. [Al-Qasas: 5]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu