Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  11 Safar 1444 Na: 1444 / 05
M.  Jumatano, 07 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mazoezi Makubwa ya Kijeshi yenye Lakabu “Simba Mwenye Hamu 2022 nchini Jordan kwa Mara ya 10 Marekani Haitaweza Kutangaza Vita vyake dhidi ya Uislamu na Waislamu
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumapili, Amri Kuu ya Kijeshi ya Marekani (CENTCOM) ilitangaza kuanzisha mazoezi ya pamoja ya kijeshi nchini Jordan, ikisisitiza kujitolea kwa Washington kwa washirika wake katika Mashariki ya Kati kwa ulinzi wa pamoja dhidi ya matishio mbalimbali.

CENTCOM ilisema katika taarifa yake kwamba mazoezi hayo yatadumu kwa wiki mbili kuanzia tarehe 4 hadi 15 Septemba, ikibainisha kuwa ni "moja ya mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi katika eneo hilo."

Jeshi la Jordan pia lilitangaza kuzinduliwa kwa mazoezi makubwa ya kijeshi ‘Simba Mwenye Hamu 2022’ nchini humo pamoja na mwenzake wa Marekani, kwa kushirikisha nchi 27 zikiwemo nchi tisa za Kiislamu.

Takriban wanajeshi 1,700 wa jeshi la Marekani, wanajeshi 2,200 wa Jordan, na wanachama 591 wa muungano wa kijeshi unaoundwa na nchi zinazoshiriki watashiriki katika mazoezi hayo, kulingana na taarifa. Mazoezi ya ‘Simba Mwenye Hamu’ yamekuwa yakifanyika katika eneo la Jordan tangu 2011 katika nyanja mbalimbali za mafunzo ya majeshi, na idadi ya kadhaa shule na vituo vya mafunzo.

Huu hapa utawala wa Jordan ambao unaendelea kuichukulia Marekani kama dola rafiki na mshirika, ambayo inadai kuwa inaichukulia kama mshirika wake wa kimkakati kwa kuzingatia kuridhia kwake masuala yake ya kiuchumi, kisiasa, kijeshi na kiusalama, jambo ambalo taifa na watu wa Jordan wamekataa, na wanakataa kata kata ushiriki wa Amerika katika jeshi la Jordan kwenye ardhi ya Jordan, ambayo inapaswa kuwa vikosi vya Jordan kuilinda nchi na watu kutoka kwa maadui halisi. Sio siri kwa mtu yeyote, na kura za maoni hazihitaji kuthibitisha kwamba umbile la Kiyahudi mnyakuzi wa Al-Aqsa, Al-Quds na Palestina, na nyuma yake Amerika na Magharibi, ni adui nambari moja kwa Waislamu kwa jumla na haswa kwa watu wa Jordan. Amesema Mwenyezi Mungu (swt):

[هُمُ الْعَدُوُّ فَاحْذَرْهُمْ قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ]

Hao ni maadui; tahadhari nao. Mwenyezi Mungu awaangamizilie mbali! Vipi wanapotoka na haki?” [Al-Munafiqun:4].

Mkataba wa ulinzi wa pamoja kati ya Marekani na Jordan ambao utawala huo uliuwasilisha kwa Marekani na kuifungua Jordan kwa upana kwa majeshi ya Marekani kukiuka matukufu na ubwana wake na kupeleleza kila jambo dogo na kubwa ndani yake, unakataliwa na watu wote wa Jordan, na Marekani haijaridhika na mkataba huu, hivyo mazoezi makubwa zaidi ya kijeshi yanayoruhusu sekta zake mbalimbali za kijeshi kuendelea na kwa miaka kadhaa ya muongo uliopita wa mafunzo na kubainisha udhaifu na nguvu za nchi hii, kuzitumia katika kile inachopanga kwa siku zijazo au kwa kile inachokihofia, ni kuukabili Ummah katika vita vyake dhidi ya Uislamu na kufuja utajiri wa nchi za Kiislamu, kwani inajua kuwa tawala zinazosalimu amri kwake katika nchi za Kiislamu zitatoweka hivi punde, na vita vyake viwe pamoja Ummah huu.

"Simba mwenye ni amali yenye mambo mengi ambayo inaonyesha kujitolea kwetu kwa ushirikiano na vikosi vya pamoja vinavyofanya kazi katika mazingira magumu ambayo hayatoi ushindi rahisi au ushindi wa haraka," alisema Meja Jenerali Steven J. deMilliano, Mkurugenzi wa Idara ya Mazoezi na Mafunzo, katika Kituo Kikuu cha Utoaji Amri za Kijeshi cha Marekani. Uhusiano wa kijeshi wa Marekani na Majeshi ya Jordan, mmoja wa washirika wenye nguvu na wa kutegemewa wa Kituo Kikuu cha Utoaji Amri za Kijeshi cha Marekani katika eneo hilo. "Kwa upana zaidi, ushirikiano huwezesha majeshi kukuza uwezo na kujibu haraka hali zinazohitajiwa."

Aliongeza, akionyesha haja ya kufanya upya mazoezi haya kila mwaka ili kuendana na maendeleo ya kijeshi na kiteknolojia: "Marudio haya ya 10 ya ‘Simba mwenye hamu’ yatajumuisha misheni ya makombora ya masafa marefu, matishio ya kimtandao kutoka kwa wapinzani bandia, mawasiliano na uratibu kati ya mashirika, ukuzaji wa ujuzi wa kukabiliana na ugaidi, uwiano wa ulinzi wa anga na makombora, kuendeleza ustadi wa usalama wa baharini na mipakani, kukabiliana na maafa, na misaada ya kibinadamu. Mandhari ya mwaka huu yataufanyia majaribio mwingiliano wa kushughulikia changamoto za kikanda katika nyanja za anga, ardhi, bahari na mtandao.

Na Amerika, katika mkakati wake wa kisiasa, ni kuzuia hatari zinazotishia ushindani wowote nayo kama nchi ya kwanza duniani. Inazishughulisha nchi za ulimwengu katika vita vya kikanda kama vile vita vya Ukraine na kuichokoza China, na inashirikiana na nguvu zinazozunguka duara la maslahi yake, lakini katika nchi za Kiislamu inashikilia uwezo na majeshi ya Waislamu kwa dhurufu zozote za mustakbali zinazotaka ushirikishi na makabiliano ili kufikia maslahi yake, ili watoto wa Waislamu wawe vinara wake. Baada ya kushindwa na kupoteza maisha ya watu na zana zake nchini Afghanistan na Iraq, na haswa katika vita vyake dhidi ya Uislamu na mradi wa mwamko wa Umma kwa kurudi kwa Dola ya Khilafah Rashida, ambayo ndiyo tishio pekee duniani kote kuiondoa na kukomesha ukatili na kiburi chake kwa walimwengu, na kwa ajili hiyo haitafuti hata kidogo kutatua matatizo ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na kile kinachoitwa suluhu ya nchi mbili ili kutatua kadhia ya Palestina, ambayo udanganyifu wake utawala na ujenzi wa makaazi unaning'inia kikamilifu, ili ikamate nyuzi za udhibiti wa kimataifa ambao unadumisha utawala wake juu ya ulimwengu, maadamu tu utabaki mbali na tishio lake la moja kwa moja.

Enyi Waislamu, enyi watu wetu wa Jordan:

Haijuzu, kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, au kwa vipimo vyovyote vyengine kwa ajili ya manufaa ya Ummah huu uliotolewa kwa ajili ya watu, kwa kafiri mkoloni Amerika kuchezea usalama wetu na kuwadhihaki watoto wetu na majeshi yetu; Majeshi ya Waislamu yapo katika kuhudumia maslahi yao ya kikoloni, na wao ndio maadui ambao wamekuwa wakiwaua na kuwaangamiza Waislamu katika nchi zote za Kiislamu. Majeshi haya ni kwa ajili ya kuwahami Waislamu na kulinda nchi zao na hayakuwekwa kuwatumikia maadui zao na kulinda tawala za vibaraka, badala ya kujishughulisha na maandalizi ya kupigana katika njia ya Mwenyezi Mungu na kukomboa matukufu yao na kumfurusha mkoloni Kafiri kutoka humo katika miundo na maumbo yake yote. Mwenyezi Mungu (swt) asema:

[وَأَعِدُّوا لَهُم مَّا اسْتَطَعْتُم مِّن قُوَّةٍ وَمِن رِّبَاطِ الْخَيْلِ تُرْهِبُونَ بِهِ عَدُوَّ اللَّهِ وَعَدُوَّكُمْ]

Basi waandalieni nguvu kama muwezavyo, na kwa farasi walio fungwa tayari-tayari, ili kuwatishia maadui wa Mwenyezi Mungu na maadui zenu [Al-Anfal:60].

Wajibu halali unayataka majeshi ya Kiislamu yajizuie kushirikiana na majeshi ya kikoloni na adui ya Marekani, Uingereza, Ufaransa na adui katika mafunzo ya ‘Simba mwenye hamu’, na yaungane kuwa kiini cha majeshi ya Dola ya Khilafah Rashida yenye kuregesha fahari na adhama ya Umma wa Kiislamu, kumuondoa mvamizi kutoka katika nchi yake, na kuregesha uadilifu na rehema kwa walimwengu wote na sio kwa Waislamu pekee.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ تُلْقُونَ إِلَيْهِم بِالْمَوَدَّةِ وَقَدْ كَفَرُوا بِمَا جَاءَكُم مِّنَ الْحَقِّ]

Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki mkiwapa mapenzi, na hali wao wamekwisha ikataa haki iliyo kujieni.” [Al-Mumtahina:1].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu