Jumamosi, 21 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/23
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Afisi ya Habari
Wilayah Jordan

H.  9 Safar 1444 Na: 1444 / 04
M.  Jumatatu, 05 Septemba 2022

 Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi

مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ

وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً

“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.[Al-Ahzab: 23]

Kwa imani na kujisalimisha kwa qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt), Hizb ut Tahrir/Wilaya ya Jordan inaomboleza kwa Waislamu kwa jumla, na watu wa Jordan haswa, na kwa Amir wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah, mmoja wa mashababu wake wanyofu, wavumilivu, na mashuhuri, na mwenye misimamo thabiti inayomridhisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake (saw), na wala hatumtakasi yeyote mbele ya Mwenyezi Mungu:

Mwanachuoni wa fiqhi na mwanafikra wa kisiasa kutoka kizazi cha kwanza cha mashababu wa Hizb ut Tahrir

Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan)

Ambaye amekwenda kwa rafiki yake aliyeko juu (swt), leo Jumatatu, tarehe 5/9/2022 M, baada ya maisha aliyoishi katika utiifu kwa Mwenyezi Mungu (swt), akibeba ulinganizi wa haki na kheri pamoja na Hizb ut-Tahrir tangu kuasisiwa kwake, akifanya kazi ya kuregesha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah kwa njia ya Utume, akiwa mvumilivu kwa aliyokutana nayo kwa ajili ya hili, ikiwemo kuteswa, kukamatwa na kufungwa gerezani, kwa hayo akitarajia mema kwa Mwenyezi Mungu, akiwa na thiqa na nusra yake (swt), na yeye Mwenyezi Mungu amrehemu akabakia thabiti juu ya haki ambayo aliibeba, akisafiri kwa ukakamavu, asiyeyumba na asiyeteteleka katika azimio lake, aliyejaa imani kwa ahadi yake (swt) kwa Umma wa Kiislamu kwa nusra na tamkini.

Twamuomba Mwenyezi Mungu amfinike marehemu wetu, marehemu wa umma, kwa rehema zake, na amjaaliye kwa mapokezi mema, na amjaalie makaazi yake katika Pepo ya juu kabisa ya Firdaus pamoja na mitume, wakweli, mashahidi, na wema na hao ndio marafiki wema, na kumlipa kwa niaba yetu na kwa niaba ya Uislamu na Waislamu malipo bora zaidi, kama ambavyo twamuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwa ajili yetu na familia yake subira na faraja njema.

إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴿

“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqara: 156]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

katika Wilayah Jordan

- Kalima ya Ustadh Bilal Al-Qasrawi katika mazishi ya mwanafiqhi, mwanafikra wa kisiasa Muhammad Hussein Abdullah, Mwenyezi Mungu amrehemu -

- Kalima ya Ustadh Marwan Obeid katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi na mwanafikra wa kisiasa Muhammad Hussein Abdullah, Mwenyezi Mungu amrehemu -

- Kalima ya Ustadh Majid Al-Aned katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi na mwanafikra wa kisiasa Muhammad Hussein Abdullah, Mwenyezi Mungu amrehemu -

- Kalima ya Ustadh Ali Telfah katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan) -

- Kalima ya Dkt Muhammad Malkawy katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan) -

- Kalima ya Sheikh Abu Salim Al-Sakhri katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan) -

- Kalima ya Dkt Hassan Abu Abed katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan) -

- Kalima ya Ustadh Sufyan Muhammad Abdullah katika kikao cha kutoa rambirambi kwa mwanafiqhi Muhammad Hussein Abdullah (Abu Sufyan) -

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
Address & Website
Tel: 
http://www.hizb-jordan.org/
E-Mail: info@hizb-jordan.org

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu