Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Serikali ya Mpito Imeweka Mfano wa Aibu kwa Kumkamata Imtiaz Salim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Bangladesh

Katika majira ya mapema Oktoba 4, 2024, serikali ya mpito, kwa desturi ya serikali ya kidikteta ya Hasina aliyeondolewa madarakani, ilimkamata Imtiaz Salim, mwanachama wa Hizb ut Tahrir/Wilayah Bangladesh. Kwa mujibu wao, kosa lake ni kwamba alishiriki katika shughuli za kisiasa za Hizb ut Tahrir.

Soma zaidi...

Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi: Sheikh Alim Ahmad Al-Hussein Muhammad Ahmad Mudawi

Mmoja wa Mashababu aliyebeba Dawah ya kurudisha maisha kamili ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, akistahamili madhara ya madhalimu jeuri mpaka yakini ilipomjia jana, Alhamisi, tarehe 30 Rabi ' al-Awwal 1446 H, sawia na 3/10/2024, kwenye Kisiwa cha Tuti jijini Khartoum.

Soma zaidi...

Msimamo Dhaifu wa Watawala wa Pakistan kwa Kashmir Inayokaliwa Kimabavu Wampa Ujasiri Mvamizi India

Msimamo dhaifu wa watawala wa Pakistan ni kwa sababu ya ubaraka wao kwa Amerika. Hata kabla ya kuisalimisha Kashmir kwa India mnamo Agosti 2019, watawala wa Pakistan hawakuwa makini kuhusu ukombozi wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu. Watawala wa Pakistan walifuata tu sera ya Amerika ya kutoa shinikizo kwa India, ili iingie kwenye kambi ya Amerika. Baada ya India kuingia katika kambi ya Marekani kupitia kundi tawala la Hindutva, watawala wa Pakistan waliachana na Kashmir Inayokaliwa kimabavu ili kuifurahisha Amerika.

Soma zaidi...

Umbile la Kiyahudi Lawaua Waislamu nchini Lebanon na Palestina Kwa Sababu ya Mwaka Mzima wa Kutochukua Hatua kwa Watawala wa Waislamu na Makamanda wao wa Jeshi

Imepita mwaka mmoja tangu jeshi la watu waoga zaidi katika uso wa dunia kuanza mauaji ya halaiki huko Gaza. Mnawezaje bado kukubali kudhalilishwa, vifo na uharibifu kama huu uliowekwa juu ya watu wenu, mbele ya macho yenu? Vipi bado mnaweza kubaki tuli, ilhali ni kwa kupitia nguvu za mikono yenu ndipo Ummah unatafuta ulinzi wake? Je, mwanajeshi anaweza kukubali ukuu wa kijeshi wa adui yake, bila kufyatua risasi hata moja? Je, askari anawezaje kukataa kupigana na adui yake, na kudumisha Dini yake, heshima na uanaume wake imara?

Soma zaidi...

India Inafanya Kazi Kutishia Ugavi Wetu wa Maji, Huku Watawala wa Pakistan Wakifanya Kazi Kusawazisha Mahusiano na Mchokozi

Licha ya kupita siku nyingi, watawala wa Pakistan bado hawajajibu ipasavyo hatua hatari ya India kuhusiana na Mkataba wa Maji wa Indus (IWT), makubaliano ya kugawanya maji yaliyosimamiwa na Benki ya Dunia mnamo 1960. Mnamo 18 Septemba 2024, India ilituma notisi rasmi kwa Pakistan, ikitaja masuala mbalimbali, ikiwemo mabadiliko ya idadi ya watu, changamoto za kimazingira, na mambo mengine, ikiomba kutathminiwa upya kwa mkataba huo. India imeripotiwa kutuma barua nne tangu Januari 2023, ikitaka uhakiki.

Soma zaidi...

Wapambe wa Utawala wa Tunisia Waruhusu Huduma za Kijasusi za Mossad na za Kigeni Kuenea Nchini humu na Kuwatesa Wanawake wa Tunisia Kwa Sababu ya Kuiunga Mkono kwao Gaza!

Katika hali inayojitokeza mara kwa mara katika matembezi mengi yanayoandaliwa na Hizb, Mashababu huhangaishwa na usalama, hasa ufuatiliaji wa wale wanaotoa hotuba wanapokuwa njiani wakirudi, ima kwa kuwaita kwenye vituo vya usalama au kuwaitisha vitambulisho vyao kana kwamba wanashukiwa kufanya vitendo vya uhalifu!

Soma zaidi...

Hakika tutaridhika na Ushindi wa Kweli Siku ya Kusimamisha Khilafah!

Sherehe zilienea katika miji mingi nchini Sudan jana, Jumamosi, 28/9/2024, mjini Shendi, Atbara, Port Sudan, na kwengineko. Sherehe hizo hata zilivuka mipaka ya Sudan hadi Misri kwa furaha kwa ushindi wa jeshi na kuingia kwake katika kiwanda cha kusafisha mafuta cha Al Jaili kaskazini mwa Khartoum, ingawa habari hiyo haijathibitishwa hadi taarifa hii kwa vyombo vya habari ilipoandikwa.

Soma zaidi...

Kuinusuru Gaza si kupitia Hotuba na Sherehe, Enyi Wanazuoni!

Mnamo siku ya Alhamisi, tarehe 26 Septemba, shughuli za Wanazuoni wa Mpango wa Umma wa Kukinusuru Kimbunga zilizinduliwa kwa mnasaba wa mwaka wa kwanza wa Hijri tangu kutekelezwa kwa Kimbunga cha Al-Aqsa katika tamasha kubwa la umma katika mji wa Istanbul. Tamasha hilo lilishuhudia ushiriki wa idadi kubwa ya wanazuoni wa Kiislamu ana kwa ana au kupitia hotuba zilizorekodiwa, pamoja na mamia ya Waturuki na wanachama wa jumuiya za Kiarabu wanaoishi Istanbul.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu