Mswada wa Marekebisho ya 26 ya Katiba: Chini ya Khilafah, Madaraka na Mamlaka Vinaamuliwa na Qur'an Tukufu na Sunnah, Wakati Kuna Mivutano ya Kuendelea ya Madaraka Chini ya Demokrasia
- Imepeperushwa katika Pakistan
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Chini ya mfumo tawala wa Demokrasia, mzizi halisi wa ufisadi ni uwezo wa walio wengi waliochaguliwa kubadili kila sheria, kila kifungu cha katiba, kila kanuni na kila agizo. Nguvu ya kutunga sheria inavipa vikundi tawala uwezo wa kubadilisha sheria kulingana na maslahi yao, sio tu kupitia mlango wa nyuma, lakini kupitia mlango wa mbele. Nguvu ya sheria ndiyo inayoliruhusu Bunge kuhalalisha wizi unaofanywa na waporaji na wafujaji kupitia Sheria ya Maridhiano ya Kitaifa, kukubali kunyang'anywa madaraka na madikteta kwa nguvu, kupitisha mipango kadhaa ya msamaha kwa mirengo inayotawala na kutoa kinga ya kikatiba ya kutoshtakiwa kwa wale wanaohusika na mambo muhimu zaidi ya nchi.