Afisi ya Habari
Malaysia
H. 24 Jumada II 1446 | Na: HTM 1446 / 15 |
M. Alhamisi, 26 Disemba 2024 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi
[مِنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُوا مَا عَاهَدُوا اللهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُمْ مَنْ قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُمْ مَنْ يَنْتَظِرُ وَمَا بَدَّلُوا تَبْدِيلاً]
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab (33): 23]
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Malaysia inatoa rambirambi zake kubwa na inasalimu amri kwa Qadhaa ya Mwenyezi Mungu (swt) kwa kuondokewa na mmoja wa wanachama wake waheshimika
USTAZ SYAHRIL BIN NOHONG (ABU QAIM BI AMRILLAH)
aliye regea kwa Mwenyezi Mungu (swt) siku ya Jumatano, 23 Jumada al-Akhar 1446 H, sawia na tarehe 25 Disemba 2024 M, huko Sandakan, Sabah, akiwa na umri wa miaka 46. Alifariki dunia kwa amani usingizini, akimuacha nyuma mjane aliyejitolea na watoto saba.
Ustadh Syahril alikuwa miongoni mwa wanachama wa mwanzo kabisa wa Hizb ut Tahrir huko Sandakan, Sabah, na alijulikana sana kwa uchamungu wake (Zuhud), tabia ya kupendeza, kujitolea kusikoyumba, na ikhlasi katika juhudi zake za kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu. Baada ya kuutambua ukweli, aliukubali bila kusita na akajitolea maisha yake kwa moyo wote katika kujifunza, kufundisha, na kujitahidi kwa ajili ya Uislamu na kusimamisha tena Khilafah. Licha ya kuvumilia magumu mengi, hakuyumba yumba katika azma yake, wala hakulalamika. Alikuwa mwenza mpole na mpendwa kwa wote waliomfahamu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) amsamehe madhambi yake yote, azikubali amali zake, ampanulie na ampambie mahala pake pa kupumzikia, na amjaalie daraja za juu kabisa Peponi pamoja na Mitume, Wakweli, Mashahidi na watu wema. Mwenyezi Mungu (swt) awape subira na nguvu familia yake iliyofiwa. Huku tukiwa tunaomboleza sana kufariki kwake, tunabaki imara katika kusema tu yale yanayomridhisha Mola wetu Mlezi:
[إِنَّا لِلَّهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ]
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Al-Baqarah (2): 156].
Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Malaysia |
Address & Website Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor Tel: 03-8920 1614 www.mykhilafah.com |
Fax: 03-8920 1614 E-Mail: htm@mykhilafah.com |