Ni kweli kwamba dola kubwa hazizaliwi ghafla mara moja, lakini hakuna shaka kwamba zinajengwa juu ya itikadi ambayo kwayo mfumo huchipuka. Wakati wa kuzaliwa kwake, fikra yake ilijumuishwa katika kundi ambalo lilijitolea mhanga mali zake za thamani zaidi na kuiunga mkono kivitendo ndani yake. Hili lilizaa dola yake, ambayo ilijizatiti kujitengenezea njia kuelekea uongozi wa kimataifa kwa msingi wa itikadi yake, kufikia haki na rehema kulingana na viwango vya asili ya kimungu katika miongo michache tu. Ni lazima kwa Ummah ambao kwa hakika unataka kurudisha nafasi yake ya hadhi miongoni mwa mataifa, si tu duniani kote, kuregea kubeba ujumbe wake kwa ulimwengu na kulazimisha uongozi wake wa kifikra na utawala wake juu ya fikra za dhulma, ubabe, na utumwa, na kufikia ukombozi wa kifikra na wa kimada. Umma huu lazima uvuke hisia, mambo ya kijuujuu, na lugha ya maneno hadi vitendo.