Gazeti la Al-Raya: Vichwa Vikuu vya Toleo 545
- Imepeperushwa katika Al-Rayah
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hizb ut Tahrir/Wilayat Tunisia ilifanya kongamano lake la kila mwaka la Khilafah mnamo siku ya Jumamosi, 26 Aprili 2025, katika ukumbi wa mikutano kwenye makao makuu ya Hizb katika makutano ya barabara ya Sakra katika mji mkuu, Tunis, chini ya kichwa: “Kufeli kwa Serikali ya Kisasa na Kutoepukika kwa Dola ya Khilafah” Kumbi mbili zilizotengwa kwa ajili ya wageni zilijaa idadi kubwa ya wanaume na wanawake waliofika kwenye kongamano hilo kutoka pande zote za ardhi ya kijani ya Tunisia.
Baada ya kukutana na Makamu wa Rais wa Trump, J.D. Vance, Modi alisitisha Mkataba wa Maji wa Indus mnamo 23 Aprili 2025, akitishia usambazaji wa maji kwa Pakistan. Enyi, simba wa jeshi la Pakistan! Hakuna njia ila kukabiliana na mashambulizi ya pande mbili za Trump dhidi ya Umma. Nayo ni kwa kupitia muungano wa Umma wa Kiislamu chini ya Khilafah Rashida ya pili. Je, jeshi kubwa zaidi la Kiislamu lingewezaje kuacha heshima hii kwa jeshi jengine lolote?!
Video ya afisa mmoja kijana wa jeshi wa Pakistan akitaka kwenda Gaza imesambaa, na wakati huo huo, video nyingine ya afisa sawia wa Misri imesambaa. Enyi maafisa wa majeshi ya Waislamu! Ikiwa hamuwezi kuleta tama la maji au tembe ya tende mjini Gaza, mutawezaje kumleta afisa aliyebeba bunduki?!
Mnamo tarehe 11 Aprili 2025, Mufti Muhammad Taqi Usmani, jaji wa zamani wa Mahakama ya Shirikisho la Sharia, alisema kwamba jihad dhidi ya “Israel” ni faradhi kwa serikali zote za Waislamu. Hata hivyo, licha ya kutangaza kuwa ni wajibu, uongozi wa kijeshi haukukusanya vikosi vya kijeshi kuinusuru Gaza.
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi na kujeruhiwa kwa zaidi ya wanaume na wanawake wa Kiislamu 180,000 hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Sweden iliandaa kisimamo mbele ya ubalozi wa Marekani katika mji mkuu, Stockholm, chenye kichwa “Risala kwa Majeshi ya Waislamu!”
Kwa kuzingatia mauaji ya kikatili (mauaji ya halaiki) ambayo yamekuwa yakiendelea kwa zaidi ya miezi 18, yanayofanywa na umbile halifu la Kiyahudi dhidi ya Waislamu wasio na ulinzi katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ambayo yamesababisha kuuawa shahidi, kujeruhiwa na kupotezwa zaidi ya wanaume na wanawake 170,000 wa Kiislamu hadi sasa, Hizb ut Tahrir / Wilaya ya Pakistan inaandaa msururu wa amali kwa kichwa: “Majeshi na Yaelekee Al-Aqsa”