بسم الله الرحمن الرحيم
Enyi Majeshi: [ما لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ]
“Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache.” [At-Tawbah: 38]
(Imetafsiriwa)
Mayahudi wameanza tena kampeni yao kali ya anga, bahari na nchi kavu dhidi ya Gaza kuanzia tarehe 18/3/2025, na hadi leo. Uvamizi wao umeenea hadi kwa watu, miti na mawe, na kuua zaidi ya wanawake 400, watoto na wazee. Hii ilikuwa baada ya takriban miezi miwili ya kile walichodai kuwa ni usitishaji vita, lakini waliuvunja. Mayahudi ni watu makhaini ambao wanazuilika tu kwa yale aliyoyataja Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz (Mwenye nguvu) katika aya hii:
[فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ لَعَلَّهُمْ يَذَّكَّرُونَ]
“Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Al-Anfal: 57]. Hakuna kitakachowazuia isipokuwa "Khandaq (Vita vya Handaki)" mpya inayoondoa mizizi yao, na Khaybar anayorudisha kuwapiga kama ilivyowapiga Thamud. Vyenginevyo, wamezoea kuvunja maagano, na hawa hapa wanafanya hivyo.
[‘Israel’ ilianzisha tena vita vyake katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza kwa msururu wa mashambulizi makali yaliyoua mashahidi 412 na kujeruhi mamia. (Al Jazeera,18/3/2025)].
[Afisi ya Waziri Mkuu wa ‘Israel’ Benjamin Netanyahu ilitangaza, mapema Jumanne asubuhi, kwamba maeneo shahaba ya Hamas yalishambuliwa kote katika Ukanda wa Gaza. Taarifa hiyo iliongeza: "Israel, kuanzia sasa na kuendelea, itachukua hatua dhidi ya Hamas kwa kuongeza nguvu za kijeshi." (Sky News Arabia, 18/3/2025)].
[Waziri wa Habari wa Ikulu ya White House Karoline Leavitt alisema kuwa 'Israel' ilishauriana na utawala wa Rais wa Marekani Donald Trump kuhusu uvamizi wake huko Gaza mnamo siku ya Jumanne. (Al Hurra, 18/3/2025)].
Mauaji na uvamizi wote huo wa kinyama ulifanyika mbele ya macho ya majeshi ya nchi za Waislamu hususan zile zinazoizunguka Palestina kama vile Misri, Jordan, Saudi Arabia, Uturuki na Iran, bila kusahau zile nchi zilizojishughulisha na udhalilishaji wao wenyewe, kama vile Lebanon, Iraq na Syria! Licha ya hayo yote, watawala wanaiomba Marekani na jumuiya ya kimataifa kuwatia shinikizo Mayahudi, katika wakati ambapo Marekani ndiyo inayowaunga mkono. Ama watawala wenyewe, wametosheka tu na kulaani pekee, kana kwamba kulaani huku kutaregesha uhai kwa shahidi, kuleta uponyaji kwa aliyejeruhiwa, au kukomboa hata shubiri moja ya Ukanda wa Gaza! Mwenyezi Mungu awaangamize, wamedanganyika kiasi gani.
Misri, ambayo iliwafurusha Makruseda na Watatari, inaridhika na kuwalaani kwa taarifa tupu zisizo na maana! (Wizara ya Mambo ya Nje ya Misri ililaani uvamizi wa ‘Israel’ kwenye Ukanda wa Gaza katika taarifa yake mnamo siku ya Jumanne, ikiuita kama "ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya usitishaji vita na ongezeko la hatari ambalo linatishia matokeo mabaya kwa utulivu wa eneo hilo." Imetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa "kuingilia mara moja ili kukomesha uvamizi wa 'Israel' kwenye eneo la ukanda wa Gaza ili kuzuia kutokea tena kwa ghasia na kupambana na ghasia." (Sky News,18/3/2025).
Na Jordan, ardhi ya Yarmouk, vita vikuu vilivyoondoa mamlaka ya Kirumi kutoka Ash-Sham, pia ililaani! (Kwa upande wake, Waziri Mkuu wa Jordan, Jaafar Hassan alisisitiza mnamo Jumanne kwamba vita vinavyoanzishwa na Israel huko Gaza "ni vita dhidi ya ubinadamu." Shirika la habari la Jordan la Petra lilimnukuu Hassan akisema wakati wa kikao cha baraza la mawaziri kilichofanyika leo: “Jumuiya nzima ya kimataifa lazima ihusike na kukomesha ukatili huu ambao umelenga watoto, wanawake na wasio na ulinzi, na leo hii unawakilishwa na njaa kwa madhumuni ya uhamishaji.” (Sky News, 18/3/2025).
Ama kuhusu Uturuki, nchi ya mkombozi aliyekomesha Himaya ya Kirumi, pia inalaani kwa maneno bila vitendo (Uturuki inalaani mashambulizi mabaya ya ‘Israel’ huko Gaza, ikizingatiwa kuwa ni “awamu mpya ya sera ya mauaji ya halaiki” inayotekelezwa na taifa la Kiebrania katika ukanda huo wa Palestina. (Sky News, 18/3/202). Vilevile, jirani yake Iran, ilisema (katika taarifa ya mnamo Jumanne, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje, Esmail Baghaei alidokeza kuwa mashambulizi ya ‘Israel’ dhidi ya Gaza, alfajiri ya kuamkia leo, yalisababisha vifo vya mamia ya watu, wakiwemo wanawake na watoto... Msemaji huyo wa Iran alizingatia kwamba Marekani “inahusika moja kwa moja na mashambulizi haya.” (Anadolu Agency,18/3/2025).
Kwa upande wa Saudi Arabia, imeanza kuegemea upande wa Marekani ya Trump, ikisema anachosema, bila kupinga uungaji mkono wake kwa Mayahudi. Badala yake, haiendi zaidi ya kulaani kwa maneno, kama wenzao: (Saudi Arabia ililaani kwa maneno makali mnamo Jumanne ‘Israel’ kuzidisha mauaji ya halaiki dhidi ya Wapalestina katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi yake ya moja kwa moja katika maeneo yenye raia bila kuzingatia hata kidogo sheria za kimataifa za kibinadamu. (Anadolu Agency,18/3/2025)).
Kwa hivyo, nchi zinazoizunguka Palestina zililaani hujuma za Kiyahudi na jinai zao zinazoendelea katika Ukanda wa Gaza! Kwa hili, bila kuhamasisha jeshi au kuinua mkuki!
Enyi Majeshi katika ardhi za Waislamu, hasa zile zinazoizunguka Palestina:
Je, kuna udhuru wowote uliobaki kwa wanaoomba msamaha? Je, kuna hoja yoyote iliyobaki kwa wanaolaani? Vipi mnaweza kuona na kusikia uvamizi na mauaji ya Mayahudi hali mmekaa katika sehemu zenu, bila kutikisika, badala ya kuelekea katika ardhi ya Al-Ribat, Palestine Ardhi Iliyobarikiwa, ili kurudisha uvamizi wa Mayahudi na kuliondoa umbile lao? Mnawezaje kukubali kukaa ilhali mnasoma maneno ya Al-Qawi Al-Aziz,
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا مَا لَكُمْ إِذَا قِيلَ لَكُمُ انْفِرُوا فِي سَبِيلِ اللهِ اثَّاقَلْتُمْ إِلَى الْأَرْضِ أَرَضِيتُمْ بِالْحَيَاةِ الدُّنْيَا مِنَ الْآخِرَةِ فَمَا مَتَاعُ الْحَيَاةِ الدُّنْيَا فِي الْآخِرَةِ إِلَّا قَلِيلٌ * إِلَّا تَنْفِرُوا يُعَذِّبْكُمْ عَذَاباً أَلِيماً وَيَسْتَبْدِلْ قَوْماً غَيْرَكُمْ وَلَا تَضُرُّوهُ شَيْئاً وَاللهُ عَلَى كُلِّ شَيْءٍ قَدِيرٌ]
“Enyi mlio amini! Mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya Akhera ni chache * Kama hamwendi atakuadhibuni adhabu chungu, na atawaleta watu wengine, wala nyinyi hamtamdhuru chochote. Na Mwenyezi Mungu ni Muweza wa kila kitu.” [At-Tawbah: 38-9]?!
Je, mnawatii watawala wanaofuata nyayo za makafiri wakoloni, hatua kwa hatua na kutupilia mbali utiifu kwa Mwenyezi Mungu na Mtume wake nyuma ya migongo yao? Hawataki kupigana na Mayahudi, kana kwamba hawaegemei upande wowote, bali wako karibu zaidi na upande wa Mayahudi. Watawala hawa wanalinda migongo ya Mayahudi wakati wanafanya mauaji huko Palestina. Utiifu wenu kwao hautakuepusheni na aibu ya dunia hii au adhabu ya Akhera, na mutajuta, lakini mutakuwa mumechelewa.
[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]
“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao * Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqarah: 166-7].
Kuwatii watawala katika kumuasi Mwenyezi Mungu ni kosa kubwa.
[يَوْمَ تُقَلَّبُ وُجُوهُهُمْ فِي النَّارِ يَقُولُونَ يَا لَيْتَنَا أَطَعْنَا اللهَ وَأَطَعْنَا الرَّسُولَا * وَقَالُوا رَبَّنَا إِنَّا أَطَعْنَا سَادَتَنَا وَكُبَرَاءَنَا فَأَضَلُّونَا السَّبِيلَا]
“Siku ambayo nyuso zao zitapinduliwa pinduliwa katika Moto. Watasema: Laiti tungeli mt'ii Mwenyezi Mungu, na tungeli mt'ii Mtume! Na watasema: Mola wetu Mlezi! Hakika sisi tuliwat'ii bwana zetu na wakubwa wetu; nao ndio walio tupoteza njia.” [Al-Ahzab: 66-67]
Enyi Majeshi... Je, hakuna miongoni mwenu mwenye hekima wa kuliongoza jeshi na kutupa ushindi wa kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu Al-Qawi Al-Aziz?
[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]
“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao” [An-Nur: 55]. Je, hakuna miongoni mwenu mwenye hekima atakayeliongoza jeshi na kutunusuru katika kusimamisha Khilafah baada ya utawala huu dhalimu ambao tunaishi ndani yake ili kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw)?
«ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ ثُمَّ سَكَتَ»
“Kisha utakuwepo utawala wa kidhalimu (ملكًا جبرية), na utadumu kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu, kisha atauondoa akipenda kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa njia ya Utume.” Kisha (saw) akanyamaza.”
Je, hakuna mwenye hekima miongoni mwenu ambaye ataliongoza jeshi na kuvunja minyororo iliyotengenezwa na watawala wa Ruwaibidha (wasio na maana, wajinga) ya kutopigana na Mayahudi? Kisha askari wa Uislamu watoke na askari hawa wanali yale aliyotufahamisha Mkweli, Mwaminifu: Al-Bukhari amepokea katika Sahih yake:
«تُقَاتِلُكُمْ الْيَهُودُ فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ.. » “Mayahudi watapigana nanyi, nanyi mtawashinda...” na Muslim amepokea katika Sahih yake: «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ.. » “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawauwa…” Na kisha mutaling’oa umbile la Kiyahudi kutoka katika Ardhi iliyobarikiwa, na kisha Ardhi Iliyobarikiwa itarudi kwenye Makaazi ya Uislamu (Dar ul-Islam), kama Umar alivyoifungua, Salah ud-Din akaikomboa, na Abdul Hamid akaihifadhi!
[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]
“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5].
H. 19 Ramadan 1446
M. : Jumatano, 19 Machi 2025
Hizb-ut-Tahrir