Jumamosi, 23 Sha'aban 1446 | 2025/02/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Trump na Mfuasi wako Netanyahu: Macho Yako Yamepofushwa

[وَغَرَّكُمْ بِاللهِ الْغَرُورُ]

“Na mdanganyifu akakudanganyeni msimfuate Mwenyezi Mungu.” [Surat Al-Hadid:14]
Umesahau hatima ya watangulizi wako miongoni mwa Warumi na Wafursi, pamoja na washirika wako duni, Mayahudi!
(Imetafsiriwa)

Trump na wapambe wake wanaendelea kurudia madai yao kwamba atainunua Gaza na kuimiliki.

[كَبُرَتْ كَلِمَةً تَخْرُجُ مِنْ أَفْوَاهِهِمْ إِنْ يَقُولُونَ إِلَّا كَذِباً]

Ni neno kuu hilo litokalo vinywani mwao. Hawasemi ila uwongo tu.” [Surat Al-Kahf:5]

“Mapema leo, Rais Trump wa Marekani alithibitisha mpango wake wa Marekani kuchukua udhibiti wa Gaza na kuwafukuza Wapalestina, akisema kwamba amejitolea kuinunua na kuimiliki Gaza. Kauli hii ilitolewa na Trump mnamo Jumapili jioni ndani ya ndege ya Air Force One alipokuwa akielekea New Orleans kuhudhuria Super Bowl." (BBC, 10/2/2025) Baadaye, wakati wa mkutano wake na Mfalme wa Jordan, alisema: "Wapalestina wataishi kwa usalama mahali pengine, nje ya Gaza, na ninaelewa kwamba tuna uwezo wa kufikia suluhisho," kulingana na maneno yake. Trump aliongeza, "Tutaisimamia Gaza vizuri sana, lakini hatutainunua," kama ilivyoripotiwa na Reuters. Alipoulizwa kuhusu 'Israel' kunyakua Ukingo wa Magharibi, Trump alisema, "Itafanya kazi," kulingana na taarifa yake. (Reuters - Erem News, 11/2/2025) Hapo awali, alikuwa amesema kwamba "'Israel' itaikabidhi Gaza kwa Marekani baada ya mapigano kumalizika," akitarajia Marekani kuwa na "umiliki wa muda mrefu" wa eneo la Palestina. (Al Jazeera, 6/2/2025)

Dhalimu huyu, aliyepagawishwa na kiburi chake mwenyewe, haelewi anachokisema. Anafikiri kwamba Gaza ni milki yake au ya mwanachini wake, Netanyahu, inayoweza kununuliwa, kuuzwa, au kukabidhiwa! Kiburi chake kimemtia upofu na kumnyima busara. Amesahau au amechagua kupuuza hatima ya wale waliokuja kabla yake.Alitanguliwa katika udhalimu wake na wafalme wa Fursi na Rumi. Khosrow alipopata habari za ujio wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kiburi chake kilimtawala, hivyo akamtuma mmoja wa watumishi wake kumwambia: Nenda Bara Arabu ukaniletee kichwa chake.” Haya ndiyo aliyoyasema kutokana na upotovu wake! (Ibn Hisham amesema katika Serah yake: Khosrow alimwandikiwa Badhan: “Imenifikia habari kwamba mtu miongoni mwa Maquraysh amezuka mjini Makka, anadai kuwa ni Nabii. Nenda kwake na umfanye ajisalimishe. Ikiwa atattubu, muwacha; vyenginevyo, nitumie kichwa chake.” Hatima yake ilikuwa kuanguka kwa ufalme wake, na utawala wa Khosrow ukasalia kuwa kumbukumbu tu chini ya mashambulizi ya jeshi la Waislamu. Fursi hatimaye ikakombolewa, na nuru ya Uislamu ikaangaza ndani yake. Ama mfalme wa Rumi, alikusanya jeshi ili kuwamaliza Waislamu katika eneo la Yarmouk, lakini hatima yake ilikuwa kushindwa. Akakimbia Sham, akiiambia: “Kwaheri, ewe Sham, kwa kwaheri isiyo na kurudi tena!” Aliondoka kwenda mahali alipozaliwa, Konstantinopoli, mpaka ilipotekwa na kuwa nchi ya Uislamu. Ama kuhusu Mfalme wa Kirumi, alitayarisha jeshi la kuwaangamiza Waislamu huko Yarmouk, lakini mwisho wake ulikuwa kushindwa kabisa. Alikimbia Sham, akisema, * "Kwaheri, Sham, kwaheri isiyo na kurudi tena," * akirudi kwenye eneo lake la kuzaliwa huko Konstantinopoli - hadi hapo, pia, ilipotekwa na kuwa sehemu ya ardhi ya Uislamu.

Ama Mayahudi wanabaki kuwa duni, wamedhalilishwa popote waendako.

[ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِنَ اللهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ]

Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge.” [Surat Aal-i-Imran:112]. Walikata fungamano lao na Mwenyezi Mungu kwa kuwaasi Mitume Wake, na tegemeo lao pekee lililobaki ni juu ya msaada wa watu—msaada ambao bila shaka utakatiliwa mbali na Amri ya Mwenyezi Mungu, kwa wakati uliopangwa, kwa mikono ya wanajeshi wa Uislamu, wakiongozwa na Imam wao. Watapigana nyuma yake na watalindwa kwaye, kama Mtume (saw) alivyosema:

«إِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ»

Kamanda (wa Waislamu) ni ngao kwao. Wanapigana nyuma yake na wanalindwa na (yeye kutokana na madhalimu na wavamizi).”

Enyi Waislamu…Trump na mfuasi wake Netanyahu wanasahau historia ya watu wao na fedheha yao ya zamani mbele ya ulimwengu. Wanasahau udhalilifu wao na utukufu wa Uislamu juu yao wakati Khilafah ilipoasisiwa. Katika siku hizo, sio mababu wa Trump wala Netanyahu wangesubutu kusema hata neno moja kuhusu kununua hata shubiri moja ya ardhi ya Kiislamu, achilia mbali Gaza, ardhi ya Hashim. Badala yake, wangeinamisha vichwa vyao kwa kutajwa tu futi moja ya ardhi ya Kiislamu.

Ndio, wanawaona Waislamu leo ​​bila Khilafah kwa zaidi ya miaka mia moja. Wanaona ardhi za Waislamu zikiwa zimegawanyika, zikitawaliwa na mawakala wao—watawala vibaraka wanaowatumikia. Hivyo, Trump anatangaza wazi mpango wake wa kuwafukuza watu wa Gaza, kuinunua na kuimiliki. Wakati huo huo, watawala wa ardhi za Waislamu hawafanyi lolote kuyakusanya majeshi yao kuikomboa Gaza na kumshambulia Trump na mfuasi wake kwenye nyuso zao. Badala yake, Trump anasema kwa ujasiri kwamba watawala hawa hatimaye watakubaliana na mpango wa uhamishaji na kila kitu anachotaka. Alipoulizwa kwa nini viongozi hao wanadai hadharani kukataa mpango huo, alijibu: "Watakubali. Wanasubiri tu kukutana nami." Anatamka hili waziwazi, lakini bado wangali wanakimbilia kukutana naye bila aibu!

Enyi Waislamu…Khilafah itaregea, na kuhitimisha utawala wa vibaraka hawa wa fedheha katika ardhi za Waislamu. Itaregea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, hii ni yakini, kwa sababu Mwenyezi Mungu ameahidi:

[وَعَدَ اللهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ]

Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walio amini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya makhalifa katika ardhi kama alivyo wafanya makhalifa wa kabla yao [Surat An-Nur:55]. Mtume (saw) pia alitabiri kuregea kwa Khilafah baada ya kipindi hiki cha utawala dhalimu:

«...ثُمَّ تَكُونُ مُلْكاً جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللهُ أَنْ تَكُونَ، ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا، ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ. ثُمَّ سَكَتَ»

 “Kisha kutakuwa na kipindi cha utawala wa kidhalimu, ambao utadumu kwa kadri Mwenyezi Mungu atakavyo. Kisha atauondoa apendapo kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah na kwa njia ya Utume.” (Ahmad)

Hata hivyo, kama tunavyosema mara kwa mara, na kama watu wenye hekima wanavyoelewa, amri ya Mwenyezi Mungu ni kwamba Malaika hawatashuka kutoka mbinguni ili kutusimamishia Khilafah tukiwa tumekaa bila kufanya kazi. Bali nusra yake na bishara zake zinawajia walio muamini, na kuwazidishia uongofu, na kuwaweka imara katika vita, mpaka awape ushindi:

[نَصْرٌ مِنَ اللهِ وَفَتْحٌ قَرِيبٌ وَبَشِّرِ الْمُؤْمِنِينَ]

nusura itokayo kwa Mwenyezi Mungu, na ushindi ulio karibu! Na wabashirieni Waumini! [Surat As-Saff:13].

Na sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu, kwa kuwa dalili zinazoashiria kuregea kwa Khilafah zinaonyesha ukaribu wake. Ummah wa Kiislamu ni Ummah hai, changamfu, unaosonga mbele kwa shauku kuelekea kusimamisha Khilafah na kuunga mkono juhudi hii mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu. Baada ya hapo, utaungana kuilinda na kushikamana nayo…Hakika Umma unaregea kwa haraka kwenye njia yake ya asili, ambayo kwayo Mwenyezi Mungu aliuleta. Kama Mwenyezi Mungu Mtukufu anavyosema:

[كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللهِ]

Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.[Surat Aal-i-Imran:110].

Ndani ya Ummah huu, kuna kundi lenye ikhlasi lililojitolea kwa Mwenyezi Mungu, lenye uaminifu kwa Mtume Wake (saw). Wanasonga mbele, mchana na usiku, mpaka itimie ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume mikononi mwao. Hawaogopi kulaumiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, na azma yao haitayumba kwa idhini yake mpaka itimie amri yake. Ni kama Mtume (saw) alivyosema katika hadith iliyopokewa na Muslim:

«لَا تَزَالُ طَائِفَةٌ مِنْ أُمَّتِي ظَاهِرِينَ عَلَى الْحَقِّ لَا يَضُرُّهُمْ مَنْ خَذَلَهُمْ حَتَّى يَأْتِيَ أَمْرُ اللهِ وَهُمْ كَذَلِكَ...»

“Kundi la watu kutoka kwa Umma wangu daima watabaki kuwa ni wenye kudhihirisha haki. Anayejitenga nao hataweza kuwadhuru. Watabaki katika njia hii mpaka amri ya Mwenyezi Mungu ije na ilhali wako katika njia hii.”

Hivyo, Khilafah itaregea, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, kupitia juhudi za watu wake baada ya kipindi hiki cha utawala dhalimu. Kisha, umbile la Kiyahudi litatokomezwa, na Palestina itaregeshwa kikamilifu kama sehemu ya ardhi ya Uislamu. Muslim pia anasimulia kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume (saw) amesema:

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يُقَاتِلَ الْمُسْلِمُونَ الْيَهُودَ فَيَقْتُلُهُمْ الْمُسْلِمُونَ..»

 “Kiyama hakitasimama mpaka Waislamu wapigane na Mayahudi, na Waislamu watawaua...” Fauka ya hayo, hata Rumi itakombolewa na mikono ya Waislamu, kama vile Constantinople ilivyokombolewa. Ahmad amepokea kwamba Abdullah bin Amr bin al-As amesema: “Tulipokuwa tukiandika karibu na Mtume wa Mwenyezi Mungu (ﷺ), mtu mmoja alimuuliza: ‘Ni upi kati ya miji miwili itakaokombolewa kwanza, Konstantinopoli au Roma?’ Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akajibu:

«مَدِينَةُ هِرَقْلَ تُفْتَحُ أَوَّلاً يَعْنِي قُسْطَنْطِينِيَّةَ»

“Mji wa Heraclius utakombolewa kwanza, ikimaanisha Konstantinopoli.”

Enyi Waislamu…Ni miongoni mwa fedheha kubwa zaidi kwamba dola katika ardhi za Uislamu zinalizunguka umbile la Kiyahudi mithili ya bangili kwenye kifundo cha mkono, na bado hazikusanyi majeshi yao kupigana na kuitakasa ardhi iliyobarikiwa kutokana na uchafu wake. Ni miongoni mwa fedheha kubwa zaidi kwamba Trump anatangaza waziwazi kuwahamisha watu wa Gaza bila ya kujali watawala wa Waislamu wanaoizunguka. Na alipoulizwa kuhusu viongozi wa Kiarabu na Waislamu kukataa kuhamishwa kwa watu wa Gaza, anajibu kwa kujiamini kwamba hatimaye watakubali, hivyo kuwadhalilisha, lakini hawaoni haya. Ni miongoni mwa fedheha kubwa kwamba hawasubutu hata kuisusia Marekani au kukataa kukutana na Trump, licha ya kauli zake kuwafichua. Badala yake, wanampongeza, na anapowaita, wanakubali, wanamtembelea na kusikiliza kwa unyenyekevu.

Ni miongoni mwa fedheha kubwa kwamba majeshi ya Waislamu yanabaki yametulia tuli huku yakishuhudia uvamizi katili wa Kiyahudi, maangamivu ya maisha ya watu, miti na mawe, wakijidanganya nafsi zao kwamba utiifu kwa watawala wao kwa kujiepusha na kupigana na Wayahudi utawaokoa. Badala yake,

[يُرِيهِمُ اللهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ]

Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao.” [Surat Al-Baqara:167] na watasema wakati wakati majuto hayatawanufaisha kitu!

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Surat Qaf:37]

H. 14 Sha'aban 1446
M. : Alhamisi, 13 Februari 2025

Hizb-ut-Tahrir

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu