Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Ni nini Sababu ya Ziara Isiyokuwa ya Kawaida na Dharura ya Netanyahu kwenda London?

 (Imetafsiriwa)

Swali:

Netanyahu alizuru Moscow mnamo 12/9/2019 wakati wa kipindi muhimu cha uchaguzi wiki mbili kabla uchaguzi wa umbile la Kiyahudi. Kabla hapo mnamo 5/9/2019 kwa haraka alizuru Uingereza na kukutana na Waziri Mkuu ambaye alikuwa amebanwa kwa mzigo wa Brexit; wakati ambapo Johnson alipata mapigo ya kushindwa mtawalia katika Bunge la Uingereza kuhusiana na Uingereza kuondoka katika Muungano wa Ulaya pasina na makubaliano. Ni wazi kutokana na ziara hizi inaonekana kama ambaye Netanyahu yuko katika haraka! Ni kipi kilicho nyuma ya ziara hizi zisizokuwa za kawaida na dharura? Je ni kwa ajili ya sababu za kiuchaguzi au kwa malengo mengine?

Jibu:

Mazingira ambayo ziara hizo zilifanyika zinaashiria kwamba lengo sio kwa ajili ya uchaguzi licha ya kwamba ziara za kimataiga zinamnufaisha Netanyahu katika uchaguzi, lakini sio lengo lililokuwa limelengwa kwa mujibu mazingira ya ziara hiyo kieneo na kimataifa. Ili kupata picha kamili, tunatathmini yafuatayo:

Kwanza: maelezo ya ziara hizi zisizokuwa za kawaida na dharura, hususan ziara yake ya London ni maelezo sahihi. Waziri Mkuu wa umbile la Kiyaudi alikutana na Waziri Mkuu Johnson ambaye amezungukwa na vikwazo vya bunge kuhusiana na utekelezwaji wa ahadi zake za kuiondosha Uingereza kutoka katika Muungano wa Ulaya kufikia 31/10/2019 ikiwa na makubaliano au la. Hawezi kuwa makini kuhusiana na masuala ya kimataifa nje ya Brexit na baadhi ya Wabunge kutoka chama chake wanampinga na huku Bunge linapiga kura kuhusu kukubaliana na Brussels na kutaka kucheleweshwa kwa miezi mingine mitatu. Bunge la Mabwana la Uingereza limepitisha kwa haraka maamuzi ya Bunge la chini na ipo miito ya yeye kujiuzulu. Ziara yake katika mazingira hayo magumu ya Uingereza kwa uhakika ni jambo lisilo la kawaida na dharura. Labda iwe ni kwa ajili ya jambo la dharura na muhimu au isingeweza kufanyika.

Linalochanganya kuhusiana na ziara hii ni suala jingine. Ni mkutano wake na maafisa wa Amerika mjini London. Ziara ya Makamu wa Rais wa Amerika, Pence ilikuwa imepangwa kuwa Uingereza tangu White House ilipoitangaza mnamo 14/8/2019 ili kujadili masuala yanayohusiana na mustakbali wa mahusiano ya Amerika na Uingereza baada ya Brexit na kujadili "tishio la athari ya Uchina" kupitia mawasiliano ya simu ya mtandao wa 5G unaotarajiwa kujengwa ndani ya Uingereza na kampuni ya Kichina ya "Huawei." Haikupangiliwa wakati huo kwamba Waziri wa Ulinzi wa Amerika ataambatana na Makamu wa Rais katika ziara hiyo na pia halikupangiliwa kukutana na maafisa wa umbile la Kiyahudi ndani ya Uingereza, kwa mujibu wa Gazeti la Al-Watan mnamo 14/8/2019 katika taarifa iliyotolewa na White House. Netanyahu alikutana na mawaziri wa ulinzi wa Amerika na Uingereza kama ilivyoripotiwa na BBC mnamo 6/9/2019. Licha ya ripoti za habari ya mkutano wa Netanyahu pamoja na Waziri wa Ulinzi wa Amerika lakini mkutano wake na Makamu wa Rais haukutajwa na chanzo chochote hata kama wote walikuweko mjini London, ambayo inaashiria kwamba walikutana kisiri! Inaonekana kama ambaye mikutano ya makamu wa rais ilikuwa siri ili kuwaonya pande zote ili zisije zikacheza nje ya sera ya Amerika!

Pili, ziara hizi za ghafla kwa muktadha wa matukio yanayohusiana:

1- Amerika imetelekeza ulinzi aina yoyote kwa vyombo vya nchi nyingine. Rais Trump ametamka (kutofurahishwa kwake na kile alichokiita "ulinzi wa Amerika kwa njia za bahari kwa miaka pasina udhibiti" katika Chaneli ya Hormuz na kuitaka dunia hususan Uchina na Japani "kulinda vyombo vyao wenyewe." TRT Arabi 29/7/2019). Waziri wa Kigeni wa Amerika Mike Pompeo naye pia akasema kwamba Uingereza "inalo jukumu la kuzilinda meli zake, Anadol agency 22/7/2019), ambayo inamaanisha kuipunguzia shinikizo Amerika juu ya Iran ili kuziteka meli nyingine. 

2- Licha ya mazingira yasiyokuwa na uhakika kuhusiana na sera ya Uingereza tangu kwa watu wake walipopigia kura Brexit mnamo 2016 na kueneza hali ya wasiwasi kuhusiana na utekelezwaji wake, wanasiasa ndani ya Uingereza mara kwa mara huzijaribu sera ambazo zinalenga kujitoa katika vikwazo vya Muungano wa Ulaya na kuionyesha nguvu ya muungano wa Kiinegreza na hivyo ndivyo Uingereza ilivyoupatiliza mzozo wa mahusiano ya Amerika na Iran na kujitoa kwake katika makubaliano ya kinuklia na mawimbi ya ulipuzi wa meli ndani ya Ghuba, kwa hivyo Uingereza kinyume na muongozo wa Muungano wa Ulaya ikaishika meli ya mafuta ya Iran ndani ya Gibraltar mnamo 4/7/2019; ilhali nchi za Ulaya zinajaribu kupunguza mzozo na Iran na kuionyesha kwamba haitumiki katika sera ya Amerika ya kufutilia mbali makubaliano ya nuklia na majaribio yake ya kupata chombo cha Ulaya cha kubadilishana kibiashara na kifedha na Iran, katika mazingira haya Uingereza ilivunja mchoro huo na kuharibu mazingira na Iran. Inawezekana kwamba Uingereza ilikuwa inaisukuma Amerika katika matatizo ya vita na Iran hususan baada ya mzozo wa Uingereza na Iran ulipozidi kutokana na Uingereza kuiwachilia meli ya Iran Grace 1 mnamo 15/8/2019 ambayo ilikuwa imeshikwa, na baada ya Iran kutoadhamana kwamba meli hiyo haitokwenda Syria ambayo iko chini ya vikwazo kutoka kwa Muungano wa Ulaya. Baada ya wimbi refu la visingizio vya kwenda Ugiriki na kisha Uturuki, meli ya Iran kwa jina Adrian Daria-1 ikawasili Syria, kwa mujibu wa ART 6/9/2019 ambayo ilinukuu tovuti ya Middle East Eye ndani ya London. Kwa kwenda Syria kinyume na udhamini wa Iran iliyotoa kwa Uingereza, Uingereza ilikuwa imepigwa kofi usoni. Mpaka sasa bado Iran inaishikilia meli ya mafuta ya Uingereza ya Stilo Ambro na haijaiwachilia! Nalo hili ni pigo la pili kwa Uingereza. Jeshi la Maji la Uingereza "HMS Montrose" limekuwa mjadala kuhusiana na mzozo wa jeshi la Iranian Revolutionary Guards. Kwa mujibu wa Will King, kamanda wa meli ya kivita, ("meli ilijipata inahangaishwa karibu kila siku na Walinzi wa Kiiran katika maji ya Ghuba" (Independent Arabia 3/9/2019).

3- Umbile la Kiyahudi kuilipua sehemu za Iran hususan ndani ya Syria na Iraq:

a- Katika kipindi cha mapinduzi ya ash-Sham, umbile la Kiyahudi lilikuwa likilipua sehemu za Kiiran ndani ya Syria pasina na kupokea majibu kutoka kwa 'muungano wa upinzani.' Umbile la Kiyahudi lilizidisha mashambulizi yake na kuwalenga viongozi wa chama cha Kiiran na Kilibanon ndani ya Syria. Iran ilikataa kwamba mashambulizi haya ndani ya Syria yaliwalenga wao kama ambaye mauaji ya Wasyria au wanachama wa chama chake ndani ya Lebanon kutoka kwa umbile la Kiyahudi haiwahusu; na kwamba kilichomuhimu kwao ni kukataa kuwepo kwa majeruhi wa Kiiran moja kwa moja na hatimaye umbile la Kiyahudi kutangaza shambulizi kubwa dhidi ya Iran ndani ya Syria  [msemaji wa Jeshi la Israel alisema kwamba ndege ya kivita ya Israel iliyalipua majeshi ya Kiiran mnamo Jumamosi Agosti 24, 2019 karibu na Damascus ambayo yalikuwa yanapanga kurusha droni kuelekea maeneo ya Israel. Jeshi likasema katika taarifa: "Shambulizi lililenga Kikosi cha Al-Quds ((Failaq Al-Quds) na wanamgambo wa kishia wanaopangilia kuboresha mipango ya kuzindua mashambulizi yanayolenga maeneo ya Israel kutoka ndani ya Syria katika siku za hivi karibuni." Msemaji wa kijeshi aliwaambia wanahabari kuwa wanajeshi wanajiandaa kuzindua "droni za kivita" ndani ya Israel. (Deutsche Welle 24/8/2019)]. Hii iliwakilisha uhangaisho wa moja kwa moja wa kijeshi na changamoto kutoka kwa umbile la Kiyahudi ndani ya Iran, ambayo ilifungua mlango mpana kwa uwezekano wa vita baina yao lau Iran ingelijibu. Licha ya vifo vya Wairan kutokana na shambulizi la umbile la Kiyahudi [Syrian Observatory ilithibitisha mnamo Jumapili kifo cha wapiganaji wa Hezbollah na Muiran mmoja kutokana na shambulizi la "Israel" karibu na Damascus. (Al-Arabiya net 25/8/2019)]. Lakini kwa sababu Amerika haitaki Iran kuingia vitani na umbile la Kiyahudi ambayo itaipelekea nayo kuhusishwa, Iran imekanusha kuwepo kwa majeruhi katika shambulizi hilo.

b- Ndani ya Iraq mwanzoni mwa Agosti 2019, umbile la Kiyahudi limekuwa likilenga sehemu za kuhifadhi silaha zinazomilikiwa na Iran na wajuzi wa Iran ndani ya Kambi Maarufu za Ukusanyaji (Al-Hasd Ash-Sha’bi). Hili litakuwa ni kukuwa kwa umbile la Kiyahudi dhidi ya Iran, kama vile shambulizi katika kambi ya Saq" ya Ukusanyaji Maarufu wa Iraq kusini mwa Baghdad mnamo 12/8/2019. Lilikuwa shambulizi la tatu ndani mawiki na ulipuaji wa kambi ya Shuhada katika Salah ud-Din. Pia ilikuwa inamilikiwa na Ukusanyaji Maarufu. Umbile la Kiyahudi lililenga moja kwa moja sehemu za kuhifadhi silaha za Wairan na wajuzi [AFP ilimnukuu afisaa wa polisi kutoka Salah ud-Din akisema, baada ya kuchunguza eneo lililolipuliwa, kwamba waliokufa kutoka katika Ukusanyaji wa Kikabila na wawili walijeruhiwa ni "Wairan wawili wahandisi wakijeshi" ambao walikuwemo kambini. (Arab 48, 12/8/2019)], kisha shambulizi la 25/8/2019 karibu na mji wa Iraq wa Qaim katika kambi nyingine na magari yaliyokuwa yanatembea; ili kupunguza mzozo, Iraq iliripoti idadi ndogo ya majeruhina na Iran nayo haikutangaza majeruhi wake lakini ilikuwa wazi kwamba umbile la Kiyahudi linaipa changamoto Iran na uwepo wake wa moja kwa moja ndani ya Iraq pamoja na Syria.

Tatu, kwa kuzingatia hayo hapo juu, tunatamatisha na yafuatayo:

1- Muingereza ambaye ametukanwa na Iran kupitia kuhangaishwa kwa meli zake katika Ghuba na kuendelea kwa kushikiliwa kwa meli yake; yote haya yaliisukuma kuweza kuanza vita dhidi ya Iran ambavyo vingeliihusisha Amerika na bila shaka Uingereza ingeshiriki ili kulipiza kisasi kutoka kwa Iran. Hivyo ndiyo sababu haiko makini kupunguza lugha ya vurugu dhidi ya Iran; na ndiyo sababu ilikataa taarifa ya Kiamerika ya matumaini iliyotolewa na Waziri wa Ulinzi wa Amerika: "Inaonekana kama ambaye Iran polepole inakaribia hali ambayo tunaweza kuwa na mazungumzo na tunamatumaini itaendelea hivi," Waziri wa Ulinzi wa Amerika Esper aliiambia Taasisi ya Huduma za Muungano wa Ufalme ndani ya London.

Alipoulizwa katika kongamano la wahabari baadaye kuhusiana na matamshi yake, Esper alisema yalikuwa "yanazingatia baadhi ya maoni yaliyotolewa na Wairan katika kongamano la G7." [Reuters 6/9/2019). Uingereza imedumu katika kupinga sauti hiyo hata kama imeashiria (Waziri wa Ulinzi wa Uingereza alisema mnamo Ijumaa katika kongamano la wanahabari akiwa na Esper, kwamba Uingereza daima itaisaidia Amerika katika njia ya mazungumzo na Iran lau makubaliano yanaweza kupatikana, lakini alisisitiza haja ya kuihukumu Iran kupitia vitendo badala ya maneno (Reuters 6/9/2019)]. Hivyo basi Uingereza imekuwa ndio moyo wa mzozo mkubwa unaohusiana na Iran. Hatimaye, Uingereza inavyovigezo vya kuanzisha vita dhidi ya Iran na inakutana na serikali ya Kiyahudi kwa lengo hilo. Hata mashambulizi ya umbile la Kiyahudi yamezidishwa ndani ya Syria 24/8/2019, Iraq na Lebanon mnamo 25/ 8/2019 baada ya Iran kuiteka meli ya mafuta ya Uingereza ndani ya Ghuba mnamo 22/7/2019 katika hali ambayo ni sawa kwa Uingereza. Hivyo basi hakunatabu kusema kwamba Uingereza inalisukuma umbile la Kiyahudi vitani na Iran na mikono yake ndani ya eneo na kwamba inasajili nguvu ili kuihusisha katika vita hivi.

2- Dola ya Kiyahudi kwa uhakika inahofia nguvu za Iran na inataka kuchochoea vita dhidi yake na kuihusisha Amerika ndani yake. Imegundua huruma ya Amerika kwa Iran na kwamba haitaki kwenda vitani dhidi yake bali ni sawa na vitendo vya kisiasa vilivyofunikwa na vitisho vya kijeshi na mzozo katika Ghuba kwa malengo mawili: ili kuisumbua Ulaya kwa kuzishtua meli zake na kisha kuifedhehesha mbele ya Iran, hususan Uingereza ili kufuatana na Amerika katika sera yake na kisha kuzihonga nchi za Ghuba kifedha chini ya kisingizio cha kuilinda kutokana na hatari ya Iran! Mzozo katika Ghuba hailengwi kuwa ni vita dhidi ya Amerika na hili linathibitishwa na vitendo vya Amerika kwa Iran; Iran ilidengua droni ya Amerika mnamo 20/6/2019 na Amerika ikashughulikia suala hilo kimya kimya, pamoja na taarifa za kujirudia kuhusu kutokwenda vitani na Iran na sio kupindua utawala. Kwa kuongezea, mzozo ulipozidi uliidhinisha mazungumzo na Iran! Ama tulichokiona katika taarifa hizo hapo juu za Waziri wa Ulinzi wa Amerika kwa Taasisi ya Huduma za Muungano wa Ufalme "Inaonekana kama ambaye Iran polepole inakaribia hali ambayo tunaweza kuwa na mazungumzo na tunamatumaini itaendelea hivi." (Reuters 6/9/2019),   

Hili likawa wazi zaidi baada ya vyombo vya habari kuripoti kwamba mkutano baina ya Trump na Rouhani ulitarajiwa pembezoni kwa Baraza Kuu katika mkutano ndani ya New York kuhusiana na vikwazo na mahusiano. Hata imeripotiwa na magazeti baadhi kama makubaliano! Uwezekano wa makubaliano baina ya Amerika na Iran inamlazimisha Netanyahu kuzuru Moscow. Vyanzo viliashiria kwamba Netanyahu ana wasiwasi wa makubaliano baina ya Amerika na Iran ambayo yataipa usalama Jamhuri ya Kiislamu ili kuchangamkia mpango wake wa nuklia na kuiondoshea vikwazo iliyowekewa. Ripoti zilisema kwamba waziri mkuu wa Israel alikuwa na wasiwasi kuhusiana na mustakbali wa uwepo wa Iran ndani ya Syria kwa kuzingatia makubaliano hayo… (Arabs: 09/09/2019)]. Hili pia ndilo lililomfanya Netanyahu kuzuru Sochi ili kwenda kujua msimamo wa Urusi lau mzozo utatokea hususan Urusi kwa kuwa ina makubaliano na Iran: [Netanyahu alisema kabla kuondoka kuelekea Sochi kukutana na Putin: Hii ni ziara muhimu tena wakati huu, tunaofanya kazi katika maeneo mengi katika mzunguko wa 360 ili kuhakikisha usalama wa Israel na dhidi ya majaribio ya Iran kutushambulia sisi, tunafanyakazi dhidi yao… (Middle East 12/9/2019)].

3- Amerika imetambua hatari ya sera ya Uingereza ya kulisukuma umbile la Kiyahudi kupigana dhidi ya Iran na mikono yake ndani ya eneo. Vita hivi sio tu vina madhara kwa Iran bali pia kwa mikono yake lakini pia italidhuru umbile la Kiyahudi na Amerika haiwezi kubakia mtizamaji ilhali umbile la Kiyahudi linapigana vita. Kwa hiyo Amerika ikaliona hilo ni jambo la dharura baada ya matukio ya mnamo 25/8/2019 ndani ya Lebanon na Iraq na siku kabla ndani ya Syria. Kinachojitokeza wazi ni kwamba Amerika inafanyakazi kuyazima majaribio hayo wakati ambapo Amerika iligundua ziara ya Waziri Mkuu wa umbile la Kiyahudi kwenda Uingereza ambayo ilifanyika kwa mpangilio wa kijeshi, (Netanyahu alifuatana na Waziri wa Baraza la Usalama la Kitaifa Meir Ben Shabat na kamanda wa Jeshi la Maji Amikam Nurkin na Mkuu wa Oparesheni katika Jeshi la Ulinzi la Israel Meja Jenerali Aharon Halewa).

Mpangilio wa Kijeshi na Uingereza inamaanisha kuwa umbile la Kiyahudi kutumia zana za Uingereza kama vile kambi za kijeshi za Akrotiri na Diklia ndani ya Cyprus au kushiriki kwa ndege za kivita za Uingereza na jeshi la maji katika kambi zake mbili katika vita kisiri na hili linawezekana kwa kuzingatia makofi ya Iran yaliyoelekezwa kwa Uingereza kama ilivyotajwa hapo juu. Amerika ilipogundua hili, ikaizima ziara hiyo kwa kumtuma Waziri wake wa Ulinzi kwenda London ili kukutana na Netanyahu, kutathmini mahitaji ya kiusalama ya umbile la Kiyahudi na kukubali kusikiliza wasiwasi wake wa kiusalama kuhusiana na Iran na kulihakikishia umbile la Kiyahudi kuwa italihifadhia usalama wake na kuilinda dhidi ya vitisho vyovyote bali pia kulikataza kutoanza vita na kutoshirikiana na Uingereza.

Nne: Hivyo basi, ni wazi kwamba lengo kuu la ziara ya Netanyahu kwenda Uingereza ilikuwa ni kuzingatia hatua za kuzidisha mzozo wa kijeshi dhidi ya Iran katika hali ambayo haitotoa mwanya kwa Amerika kushirikiana nayo. Uingereza inatarajiwa kuendelea na mtazamo wake wa kulichochea umbile la Kiyahudi kwenda vitani na kuipa msaada wa kijeshi kwa kutumia kambi zake za kijeshi zilizoko Cyprus au nyingenezo na kuipa zana muhimu ndani ya nchi inazozidhibiti hususan kama Jordan na UAE. Kwa upande wake, Amerika itaendelea kuisukuma Iran na mikono yake kujibu kwa wepesi pasina majibu mazito na huu ndio umekuwa mtizamo wake kwa "muungano wa upinzani" kwa miongo: "Majibu kwa eneo na wakati muafaka" au kujibu ili kuziba sura pasina na athari ya kiuhakika. Hii ni kuongezea na kazi ya Amerika ndani ya umbile la Kiyahudi ili kuzuia vita kupitia ushawishi wa Amerika ndani ya jeshi la umbile hilo. Hali iko kama ilivyokuwa mnamo 2012 kwa mujibu wa vyanzo vya Kiyahudi kwamba umbile la Kiyahudi lilikuwa linaifanyia ujasusi Iran ili kuilipua.

Amerika inaifanyia ujasusi umbile la Kiyahudi ili kujua mipango yake dhidi ya Iran na kuizua. Hii ndiyo hali ilivyo hii leo. Licha ya upande wa Amerika dhidi ya vita utafaulu ukilinganishwa na Uingereza wa kuchochea vita, bali hali itabakia kuwa ya mshikemshike baina ya umbile la Kiyahudi linalochochewa na Uinfereza na zana zake na msaada wake kwa upande mmoja na Iran na mikono yake upande mwingine. Na huku Amerika ikiziongoza safu zote mpaka pale ambapo itatatua masuala ya upande mmoja!

Lengo la ziara ya kwenda Urusu ni tofauti na lengo la kuzuru Uingereza; ziara ya kwanza ilikuwa ni juhudi za kiushirikiano baina ya Netanyahu na Uingereza kuhusiana na harakati za matukio moto ili kuikabili Iran na kuiabisha Amerika kwa kushiriki ndani yake. Ziara ya Urusi ilikuwa kwa ajili ya kujua msimamo wa Urusi juu ya Iran na uwepo wa makombora yake ndani ya Syria na lau Urusi inaweza kutumia shinikizo zake "nyepesi" ili kuiondoa Iran ndani ya Syria au hata kuitenga kango kutokana na eneo lililovamiwa la Palestina ili kuyaweka mbali makombora yake kutolihami umbile la Kiyahudi na sio kushirikiana katika kukabiliana na Iran; Urusi ina makubaliano nayo. Kwa hiyo ushirikiano wa kukabiliana dhidi ya Iran hakutarajiwi kutokea baina ya Urusi na umbile la Kiyahudi

Tano: na mwisho kabisa watawala Ruwaibida (wajinga) ndani ya nchi za Waislamu wanawaruhusu Makafiri wakoloni hata pasina idhini wala ridhaa zao! Makafiri wakoloni wanaingilia kati masuala ya Waislamu na kuweka suluhisho na mipango yao ili kufikia maslahi yao na kuyaharibu maslahi ya Waislamu. Lakini lau kundi au chama cha Waislamu kitasimama ndani ya nchi za Waislamu ambacho kinalingania ukweli na kuonyesha suluhisho sahihi la Kiislamu kwa matatizo yetu kwa kurudisha tena maisha ya Kiislamu na kusimamisha Khilafah, kundi hili litazingatiwa kuwa limekiuka sheria na litashtakiwa, litateswa na kufungwa gerezani…n.k. Hii ni dhuluma na ukweli utadhihiri na utaangamiza urongo.

(وَسَيَعْلَمُ الَّذِينَ ظَلَمُوا أَيَّ مُنْقَلَبٍ يَنْقَلِبُونَ)

“Na wanao dhulumu watakuja jua mgeuko gani watakao geuka” [Ash-Shu’ara: 227].

(إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ)

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia” [Qaf: 37]

14 Muharram 1441 H

Ijumaa, 13/9/2019 M

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 02 Aprili 2020 20:38

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu