Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Jibu la Swali

Mvutano kati ya Marekani na China juu ya Taiwan

(Imetafsiriwa)

Swali:

Ni nini kinachosababisha mvutano kati ya Marekani na China kuhusu Taiwan? Je, nia gani zinazosababisha mvutano huu? Kwa nini Marekani iliichokoza China kwa ziara ya Spika wa Baraza la Wawakilishi na wajumbe wengine wa Congress nchini Taiwan? Ni nini umuhimu wa kisiwa hicho kwa China na Amerika? Je, mambo yanaelekea kwenye vita au kwa utulivu?

Jibu:

Ili kufafanua uhalisia wa mvutano huu unaokua juu ya Taiwan, nia yake, na uchockozi, ni muhimu kukumbuka ukweli fulani muhimu:

Kwanza: Amerika inaichukulia China kuwa mshindani wake nambari moja kimataifa. Uchumi wa China ni mkubwa sana na unakua kwa kasi zaidi kuliko ukuaji wa uchumi wa Marekani. Amerika inatishiwa na China kuwa nambari 1 katika uchumi duniani katika miaka michache. Nguvu hii ya kiuchumi nchini China inageuka kuwa nguvu ya kijeshi; Matumizi ya kijeshi ya China yanaongezeka mwaka baada ya mwaka, ambayo uwezo wa kijadi na nyuklia wa jeshi la China hukua, na kwa hayo, malengo ya kisiasa ya China yanakua, ukiwemo mradi wa Njia ya Hariri, unaoipa China ushawishi wa kisiasa na kiuchumi katika nchi kadhaa, hasa katika Asia. Haya yote hayaipendezi Marekani, ambayo ilitangaza vita vya kibiashara dhidi ya China, na kuanza kujenga ushirikiano wa kijeshi huko Asia ili kuipinga na kuzuia kuongezeka kwake.

Pili: Kwa upande wa Taiwan, ni kisiwa kikubwa chenye eneo la kilomita 36,000  mraba na wakaazi milioni 24. Ina uchumi uliotangulia ambao unaifanya kuwa "dola" ya 26 ya kiuchumi zaidi duniani na inajulikana kwa sekta yake ya kisikoloni (chip) za elektroniki. Kwa hivyo, ni nchi kamili kulingana na viwango vya nchi leo. Hata hivyo, historia yake na ukweli kwamba wakaazi wake ni Wachina, na kwa sababu iko umbali wa kilomita 140 tu kutoka bara la China, hufanya China ichukulie Taiwan kuwa eneo la waasi. Historia yake ya kisiasa inaufanya uhusiano wake na China kuwa mada motomoto, kwa sababu baada ya Chama cha Kikomunisti kushika hatamu za uongozi wa China Bara mwaka wa 1949, watawala walioshindwa wa China (Chama cha Kitaifa cha China- Kuomintang) walikuwa wamehamia Taiwan na kuwa washirika kwa utawala wao wakati huo. Wachina milioni mbili kutoka kwa wapinzani wa Chama cha Kikomunisti walihama nacho na kuanzisha mji mkuu wa Taipei, na hivyo watawala wa zamani wa China (kabla ya Wakomunisti kuchukua utawala) walikuwa wamekiweka kisiwa cha Taiwan chini ya utawala wao na kusaidiwa katika hilo na mwavuli wa jeshi la Amerika lililopanuliwa kwao. Marekani ilitia saini makubaliano ya pamoja ya ulinzi na Taiwan mwaka 1955 kama "Jamhuri ya China" kwa sababu Marekani haikuitambua Jamhuri ya China wakati huo, ambayo inatawaliwa na Chama cha Kikomunisti cha China. Marekani imeingilia kati mara kwa mara kuitetea Taiwan na kuipa  kiti cha kudumu cha China katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tatu: Hata hivyo, Marekani, baada ya maelewano yake na Beijing, imekubali kuhamisha kiti cha China katika Umoja wa Mataifa hadi Beijing, yaani, kwa Chama cha Kikomunisti cha China, na kuifukuza Taiwan kutoka Umoja wa Mataifa, na tangu wakati huo ilitangaza kwamba inaunga mkono sera ya China Moja, ikimaanisha kwamba haitambui uhuru wa Taiwan, lakini imeweka makubaliano yake ya ulinzi kuwa salama ili kuzuia China kuiteka. Haya yote yameifanya Amerika kuwa kipengele hai katika suala la Taiwan kwa zaidi ya miaka sabiini. Leo hii inaichukulia kama nchi huru bila kutambua rasmi uhuru wake, na inaanzisha uhusiano wa kisiasa, kibiashara, kiuchumi na kijeshi nayo, pamoja na ulinzi wa meli za Marekani kwa ajili yake, na ina afisi inayofanya kazi ya Ubalozi halisi huko Taipei, ingawa haujatajwa rasmi ubalozi huo.

Nne: Hii ilikuwa wakati wa historia ya kuzaliwa kwa Taiwan kama chombo cha kisiasa kilichojitenga na chombo cha Kichina. Leo, nguvu ya China imeongezeka sana, na imekuwa nchi maarufu katika anga ya kimataifa, na imepata ushawishi mkubwa katika Asia, hasa ushawishi wa kiuchumi, lakini kutokuwa na uwezo wa kutatua suala la Taiwan, kama eneo asi, inawakilisha udhaifu mkubwa kwa ajili yake, na kama China katika siku za nyuma na bado haiogopi nguvu za kijeshi za Taiwan na kwa hakika inaamini uwezo wake wa kurejesha kisiwa kwa kukumbatia kwa nguvu, ilikuwa na bado inaogopa vita na Marekani kwa sababu ya Taiwan. Hili linadhihirika katika mgogoro wa sasa ambapo Marekani inaonyesha uthabiti dhidi ya China, kwa sababu China kimataifa imeridhishwa na nchi za dunia kutotambua uhuru wa Taiwan, sera hiyo inayojulikana na iliyokubaliwa na Marekani yenye jina la "China Moja". Haya yote licha ya ukweli kwamba nchi hizo, zikiongozwa na Amerika, zinaichukulia Taiwan kama nchi huru. Kwa ujumla, China haikusababisha migogoro mikubwa karibu na Taiwan ambayo ingezuia uhusiano wa kibiashara wa China na ulimwengu.

Tano: Amerika imeichukulia Taiwan kama uwanja wa kuichokoza na kuitusi China na kuonyesha udhaifu wake ikiwa itakubali uchochezi wa Marekani, na ikiwa China itakataa uchochezi huo wa Marekani na kuanza kujitetea, basi Taiwan inakuwa shimo kamili ambalo China inahusishwa nayo. Maana, kuweka China kati ya hiari mbili, bora kati yazo ambayo ni chungu, na hii ndiyo inayofanyika leo kwenye mgogoro wa Taiwan. Bila sababu yoyote halali, Marekani ilitangaza nia ya Mbunge wa Marekani, spika wa Baraza la Wawakilishi, Nancy Pelosi kuzuru Taiwan, na tarehe iliyotarajiwa ilikuwa 3/8/2022. China ilikasirika na kuionya Amerika kwamba ingelipia gharama endapo Pelosi angezuru Taiwan: (Beijing ilionya, kwamba ndege zinazokiuka marufuku ya kusafiri katika anga ya Taiwan zinaweza kuangushwa." (Tovuti ya Gazeti la Al-Shorouk, 2/8/2022), lakini Amerika ilizidisha uchochezi wake, kwa hiyo Pelosi alitekeleza ziara hiyo akiwa ndani ya ndege ya kijeshi ya Marekani na kusindikizwa na ndege nyingine 13 za kijeshi zilizopaa kutoka kambi yake ya kijeshi huko Japan, na kukaidi majibu ya vitisho kutoka kwa China.

Sita: China ilitangaza kuanza kwa mazoezi makubwa ya kijeshi katika Mlango wa bahari wa Taiwan, ikiwa ni pamoja na kurusha makombora, na kuitaka Marekani kutii sera ya China Moja, iliyokubaliwa kati ya pande hizo mbili tangu mwaka 1971. Ukurasa wa ziara ya Pelosi ungegeuzwa karibu lau siyo nia ya Marekani kwa uchochezi zaidi. Uchochezi ambao ulionekana katika ziara ya baadaye ya wajumbe wengine wa bunge la Congress la Marekani kuonyesha dhamira ya Marekani ya kuikaidi China, (wawakilishi wa Bunge la Marekani waliwasili Taiwan, Jumapili, Agosti 14), kulingana na kile kilichotangazwa na taasisi inayohudumu kama Ubalozi wa Washington jijini Taipei, siku chache baada ya China kufanya mazoezi ya kijeshi karibu na kisiwa hicho kujibu ziara ya Spika wa Bunge la Marekani Nancy Pelosi. (The Independent Arabia, 14/8/2022). China ilijibu kwa kuanzisha mazoezi mapya ya kijeshi kwenye mlango huo wa bahari na Marekani ikatangaza kuwa jeshi lake la wanamaji na anga limefanya operesheni ya kupita katika Mlango-Bahari wa Taiwan ili kuthibitisha uhuru wa urambazaji humo. Taiwan ilianza kuonyesha meno na pia kufanya mazoezi ya kijeshi kuiga shambulizi la Wachina juu yao. Kwa hivyo, mzozo wa Taiwan ulizuka kati ya Amerika na China, na unaweza kufupishwa kama ifuatavyo:

1- China ina hasira na inajitayarisha kwa uwezekano wa vita. (Wizara ya Ulinzi ya China ilisema katika taarifa tofauti kwamba ziara ya wawakilishi wa Marekani ni ukiukaji wa ubwana na ukamilifu wa ardhi ya China, na "inafichua kikamilifu sura ya kweli ya Marekani kama mharibifu wa amani na utulivu katika Mlango Bahari wa Taiwan.” Aliongeza kuwa, "Jeshi la Ukombozi la Watu wa China linaendelea kutoa mafunzo na kujiandaa kwa vita, linatetea kwa uthabiti uhuru wa kitaifa na ukamilifu wa eneo, na litaondoa kwa uthabiti aina yoyote ya 'uhuru wa Taiwan'  kujitenga na uingiliaji wa kigeni." (The Independent Arabia,16/8/2022).

2- Kuhusu Amerika, inaendelea kuchochea, kuhamasisha miungano na karibu uchochezi moto dhidi ya China, (Makamu wa Admiral wa Seventh Fleet ya Marekani, Karl Thomas alisisitiza mnamo Jumanne, Agosti 16, wakati wa mkutano huko Singapore, kwamba uamuzi wa China wa kurusha makombora Taiwan lazima igombezwe kama "isiyowajibika," (The Independent Arabia, 16/8/2022) na alichochea nchi za Asia dhidi ya China, akisema kulingana na chanzo hicho hicho: ("Ikiwa huipingi, shida ni kwamba itakuwa ndio desturi... Watu wanakubali tu. Na kisha ghafla, watu wanaweza kutoa madai kama vile Bahari ya Kusini ya China ni eneo lao la bahari"). Kabla ya hapo, Rais wa Marekani alikuwa amejibu wazi kwamba Marekani itapigana pamoja na Taiwan ikiwa China itavamia (Rais wa Marekani Joe Biden alionya kwamba China "inacheza na moto" katika suala la Taiwan, na kuahidi kuingilia kijeshi ili kulinda kisiwa hicho ikiwa kitashambuliwa..., Alipoulizwa moja kwa moja iwapo Marekani ingeilinda kijeshi Taiwan endapo China itaivamia, wakati haikufanya hivyo nchini Ukraine, Biden alijibu: “Ndiyo...ni ahadi tuliyoiweka.” (BBC, 23/5/2022) Kwa kiwango hiki cha juu cha uchochezi wa Marekani kwa China nchini Taiwan na China kuonyesha uwezo wake wa kijeshi kuzunguka Taiwan, na vitisho vinavyo andamana na Marekani kuleta manuari zake na ndege katika mlango bahari huo huo, na changamoto kwa China mlangoni mwake, mgogoro huu  unachukuliwa kuwa hatari sana kwa sababu Amerika ndiyo inayoisukuma kwa kero zaidi. Imekuwa ikikusanya majeshi yake kwa miaka mingi huko Asia kwa uwezekano wa makabiliano ya kijeshi na China, hivyo Amerika iliharakisha hatua zake za kujenga ushirikiano mpya wa kijeshi dhidi ya China, kama vile muungano wa Aukus na Australia na Uingereza, na kuimarisha zilizopo, kama vile muungano wa mataifa ya Quad na Japan, India na Australia, yaani, Amerika inafanya majaribio ya tishio la kijeshi pamoja na tishio la kiuchumi, la kwanza ni la ufanisi zaidi kuliko la pili.

3- Inaonekana China imefahamu kwamba mipango hii inahusiana na sera kuu ya Marekani ya kuibana China na sio suala la Taiwan, hivyo inaona inaonyesha uwezo wake wa kijeshi. Taarifa iliyotolewa na Kamandi ya Mashariki ya Jeshi la China ilisema kwamba ("Jeshi la Ukombozi la Watu wa China lilipanga doria mnamo Agosti 15 kujiandaa kwa vita vya nguvu nyingi za silaha, na mazoezi ya vita baharini na anga karibu na Taiwan." Independent Arabia, 14/8/2022). Pia, (jeshi la China limesema leo kwamba lilifanya mazoezi karibu na Taiwan kuunda kile ilichoelezea kama kizuizi kikubwa kwa Washington na Taipei, "ambayo inaendelea kufanya hila za kisiasa na kudhoofisha amani na utulivu katika Mlango bahari mzima wa Taiwan." Kamandi ya mashariki ya jeshi la China ilisema Jeshi la Ukombozi la Watu limeandaa mazoezi

ya mapigano hai kwenye bahari na anga karibu na Taiwan. Katika muktadha huo huo, Wizara ya Ulinzi ya China ilisema vikosi vyake vinaendelea kutoa mafunzo, kujiandaa kwa vita na kutetea kwa uthabiti mamlaka ya kitaifa, na kukandamiza aina yoyote ya uhuru wa Taiwan na majaribio ya kuingiliwa kwa mataifa ya kigeni. Wizara ilionya Marekani na chama tawala cha maendeleo cha kidemokrasia huko Taipei kwamba kuitumia Taiwan kudhibiti China kunaelekea kushindwa. (Al-Jazeera Net, 15/8/2022). Pia, tarehe 17/8/2022, China ilituma baadhi ya vikosi vyake nchini Urusi kufanya mazoezi ya pamoja na jeshi la Urusi, kana kwamba ilikuwa inatishia Marekani na kumaanisha kwamba Urusi inaunga mkono China katika mgogoro wa Taiwan.

Saba: Hivi ndivyo vipimo vya mzozo wa Taiwan ambao Amerika inaunda na kupitia kwayo inataka kuikomesha China. Ni muhimu kuzingatia masuala manne yanayohusiana:

1- Wakati Marekani imekuwa na hofu ya vita vya kiuchumi na China kwa sababu ya nguvu ya uchumi wa China, tofauti kubwa ya nguvu za kijeshi kati ya Marekani na China inafanya Marekani isiogope makabiliano ya kijeshi na China, hivyo kero ya Marekani katika suala la Taiwan lazima  ionekane kama sera za wazi na kali zaidi za Marekani za kuhamisha uwanja wa migogoro na China kutoka kwa uchumi hadi uwanja wa nguvu za kijeshi ambapo Amerika inakaribia kuwa bora kuliko China. Na pengine kujishughulisha kwa Urusi na vita vya Ukraine kunatoa uwezekano wowote wa msaada wa kijeshi wa Urusi kwa China katika tukio la vita dhidi ya Taiwan, vita ambavyo ni mbali na uwezekano wowote wa nyuklia.

2- Iwapo Marekani itafanikiwa kuihusisha China katika vita nchini Taiwan, na kisha, pamoja na washirika wake, kuiwekea vikwazo vya kiuchumi, sawa na vile ilivyowekewa Urusi, basi ukuu wa China unaowakilishwa katika uchumi utakuwa chini ya tishio kubwa sana ambalo linaweza kufikia matarajio ya Amerika ya kudhibiti nguvu ya China. Vikwazo hivi vinavyotarajiwa dhidi ya China, katika tukio ambalo ilikimbilia kuivamia Taiwan, inaonekana kwa Amerika kuwa na ushawishi mkubwa na itakuwa chungu sana kwa tabaka la watu tajiri zaidi nchini China, ambao ni wanachama waandamizi wa Chama tawala cha Kikomunisti. Na tabaka hili lenye ushawishi mkubwa, endapo maslahi yake yataharibiwa kwa kiwango kikubwa sana, itafanya kazi kama safu ya tano kutoka ndani ya Chama cha Kikomunisti cha China kuelekea maelewano na Amerika!

3- Pamoja na yote yaliyotajwa, ni wazi kwamba ushadidi juu ya Taiwan unatokana na Amerika na unasonga kuelekea juu. Ni wazi pia kwamba kujishughulisha kwa Amerika na vita huko Ukraine hakuzuii kuongeza ushadidi kwa China. Ili kudhihirisha hili zaidi, Amerika iliitikia Poland ilipojitolea kuipatia Ukraine MiG zilizotengenezwa na Sovieti, Poland ilidai wakati huo kwamba hii iwe kama malipo kwa Marekani kuipatia Poland F-16. Marekani ilisema kuwa viwanda vya ndege vya Marekani vilikuwa vinafanya kazi ya kuipatia Taiwan ndege za kivita, ikimaanisha kuwa vita vya Ukraine havikuifanya Marekani kuipuuza China. Huu ndio mzozo wa sasa wa Taiwan na hiyo ndiyo ilikuwa nia yake.

4- Ama iwapo mgogoro huu utasababisha vita au mapatano, kuna uwezekano mkubwa unakusudiwa kuishughulisha China na mzozo ulio mlangoni mwake, ambao unaizuia kuiunga mkono Urusi katika vita vyake dhidi ya Ukraine, na kwa hivyo Amerika inaunda mzozo kwa Urusi huko Ukraine na mgogoro kwa China nchini Taiwan, na pwani itakuwa wazi kwa Marekani katika kudhoofisha pande zote mbili, kwamba ni kama Urusi na China hawatambui jinsi kinamasi ni hatari ambayo Marekani imewaandalia katika kupasha joto juu ya migogoro nchini Ukraine na Taiwan! Tunasema hili linawezekana zaidi kwa sababu uwezekano wa vita, au angalau mapigano ya kijeshi, ni jambo linalowezekana, kwa sababu kosa lolote lisiloweza kudhaniwa katika suala hili kutoka kwa muungano wa majeshi na kuongezeka kwa uchochezi hufanya hili kuwa jambo linalowezekana.

Nane: Hitimisho ni kwamba dunia hii siku hizi inatawaliwa na nchi (kubwa) zisizothamini haki na wema, bali zimegubikwa na dhulma na uovu kuanzia juu ya vichwa vyao hadi nyayo za miguu yao. Hizi ni nchi ambazo maslahi yao yakihitaji uharibifu wa ardhi na watu, watafanya hivyo, na ikiwa matamanio yao yanahitaji, rushwa, ufisadi na umwagaji wa damu, itamwaga. Ni kana kwamba uhalisia wa kale ulikuwa umerudi pamoja na Fursi na Rumi yake zile “dola kuu” za wakati ule, na kama vile zilivyoondolewa kwa mikono ya waumini, ndivyo dola kubwa zitakavyo toweka leo kwa mikono ya waumini, na Khilafah Rashida itang’ara tena kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu akipenda, na kueneza kheri kote duniani.

[وَيَقُولُونَ مَتَى هُوَ قُلْ عَسَى أَنْ يَكُونَ قَرِيباً]

Na watasema: Lini hayo? Sema: A'saa yakawa karibu!”  [Al-Isra: 51]

25 Muharram 1444 H

23/8/2022 M

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu