Jumanne, 22 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/24
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Vichwa vya Habari 15/05/2020

Vichwa vya Habari:

  • Virusi vya Korona Vinaweza Kuugharimu Uchumi wa Ulimwengu Dolari Trilioni 8.8 Imesema ADB
  • Virusi vya Korona: Amerika Yaishutumu China kwa Kujaribu Kuiba Chanjo ya Virusi Vya Korona
  • Pakistan Yaizawadia China Kandarasi ya Ujenzi wa Bwawa Bila Kujali Upinzani kutoka India

Maelezo:

Virusi vya Korona Vinaweza Kuugharimu Uchumi wa Ulimwengu Dola Trilioni 8.8 Imesema ADB

Janga la virusi yya Korona huenda likaugharimu uchumi wa ulimwengu kati ya dolari Trilioni 5.8 na dolari trilioni 8.8 (euro trilioni 4.7 hadi euro trilioni7.1), kulingana na Benki ya Maendeleo ya Asia (ADB). Matarajio haya ni mara mbili zaidi ukilinganisha na miezi iliyopita ikiwa ni sawa na asilimia 6.4 hadi 9.7 ya uchumi wa dunia. Inakuja kama kipimo cha kupunguza kusambaa kwa Virusi vya Korona vinavyo endelea kupooza na kudumaza shughuli za kiuchumi dunia nzima. Kiulimwengu mataifa yamechukua hatua tofauti tofauti kwa ajili ya kuzuia athari kuendelea. "Uchambuzi huu mpya unaweka picha wazi ya namna uchumi ulivyo athiriwa na virusi vya Korona," mwanauchumi mkuu wa Benki ya ADB Yasuyuki Sawada alisema. "pia inaonyesha umuhimu wa uingizaji mpya wa sera mbadala zitakazo saidia kupunguza madhara na uharibifu katika uchumi ," aliongezea. ADB ilisema mwisho kabisa wa jambo hili umeegemea katika dhana kwamba vizuizi vya kuendelea na shughuli za kibiashara vitabakia kwa miezi sita, wakati ambao kilele cha mwisho kinaonyesha vizuizi vitabaka kama vilivyo kwa miezi mitatu. Benki kuu zote duniani zimeamua kupunguza viwango vya riba na kufanya kila juhudi kuzuia athari ya tatizo ambalo limekumba soko la fedha na kuzusha taharuki ya muanguko mkubwa wa uchumi ulimwenguni. Jana takwimu mpya zimeonyesha athari kubwa za virusi vya Korona katika uchumi mkubwa dunia ikiwa ni pamoja na idadi kubwa ya watu wa Amerika wasiokuwa na ajira waliokuwa wakitafuta pozo za malipo kufika milioni 3 wiki iliyopita. Karibu robo ya nguvu kazi ya watu wa Amerika hivi sasa ikidai aina ya malipo kama hayo. Mapema wiki hii mwenyekiti wa Shirikisho la Akiba la Amerika alionya kwamba uchumi wa Amerika utaregea katika hali yake kwa taratibu mno kuliko ilivyo tarajiwa. Jerome Powell alitahadharisha kwamba Amerika itaregea katika hali yake taratibu sana pamoja na maumivu ya kiuchumi bila msaada wowote wa ziada kutoka serikalini. Muda huo huo inatarajiwa kwamba juhudi za serikali ya Uingereza ya kupambana na janga la virusi vya Korona imepelekea kupatikana kwa euro bilioni £123.2. Afisi inayohusika na Bajeti ilisema inataraji mkopo wa mwisho wa mwaka kufikia sawa na asilimia 15.2 ya uchumi wa Uingereza, ikiwa ni pamoja na ongezeko la  gharama la miradi midogo kuwa ni sababu msingi ya kuongezeka huko. [Chanzo: BBC]

Katika namna nyingine, takwimu mbaya za kiuchumi zinasababishwa na hatua zinazochukuliwa na serikali duniani kote kwa kuzuia shughuli zote za kiuchumi. Ingelitosha kuwazuia wagonjwa na watu hatarishi, na kisha kuendelea na shughuli za kawaida za kiuchumi, hilo lingesaidia kupunguza athari ya pato la uchumi wa kiulimwengu.

Virusi vya Korona: Amerika Inaishutumu China kwa Kujaribu Kuiba Chanjo ya Virusi vya Korona

Mnamo siku ya Jumatano mamlaka za Amerika zilionya kwamba wadukuzi mitandao wa China walijaribu kuiba taarifa muhimu kuhusu virusi vya Korona zinazohusu matibabu na chanjo, hilo limezidi kuchochea vita kati ya Washington na Beijing kuhusu janga la Korona. Shirika la ujasusi FBI na kikosi maalumu cha ulinzi wa mitandao na shirika la ulinzi la miundombinu (CISA) yalisema mashirika yanayojishughulisha na utafiti wa virusi vya Korona yalikuwa katika hatari ya "kulengwa na kupata mashambulizi ya kimtandao kutoka kwa Jamhuri ya Watu wa China." Walionya kwamba serikali ya China ilishirikiana na wadukuzi wa mitandaoni waliojaribu kupata "Taarifa muhimu za kisomi  na taarifa za afya ya umma zinazohusiana na chanjo, na majaribio kutoka katika mtandao na baadhi ya watu wanaojihusisha na utafiti wa virusi vya Korona ." "Juhudi za China zinazolenga vitengo hivi zinatishia juhudi za nchi yetu za kupambana na virusi vya Korona," walisema. Mashirika hayo mawili hayajatoa ushahidi wowote wala mfano unaothibitisha madai yao. Lakini onyo hilo limeongeza ukuaji wa vita kati ya Nchi kubwa Duniani kuhusu mlipuko wa maradhi ulioanzia China na kuua watu 293,000 dunia nzima, na zaidi ya 83,000 nchini Amerika. Rais Donald Trump ameishutumu China kuficha chanzo cha Virusi hivi na kutoshirikiana na Amerika na nchi nyingine katika utafiti na kupambana na ugonjwa huu. Mnamo siku ya Jumatatu Rais Trump aliulizwa kuhusu ripoti kwamba Amerika inaamini wadukuzi wa mtandaoni kutoka China walilenga tafiti za Amerika za chanjo ya Korona, Trump alijibu: "Ni kipi kipya kutoka China? Ni kipi kingine kipya? Niambie. Sina furaha na China." Onyo la Jumatano pia limeweka wazi kwamba Washington inaamini China inaendeleza juhudi pana za kupata siri za Amerika za kibiashara na teknolojia kwa kila njia, chini ya Raisi  Xi Jinping ambaye anafanya juhudi ili kuifanya nchi yake kuwa ni kinara wa teknolojia katika muongo huu. Mwezi wa pili Idara ya Haki ya Amerika iliwahukumu wanajeshi wanne wa China kwa kosa la udukuaji wa data za hali ya juu za Amerika, zilizowapa taarifa ya watu milioni 145 kutoka Amerika. Hivi sasa Amerika imeendelea kuwashtaki wasomi wengi kwa uhalifu unao husishwa na tukio hilo, nchi zote Amerika na China. Mnamo Jumatatu, Idara ya haki ilitangaza kuwashikilia Profesa na mhandisi kutoka chuo kikuu cha Arkansas Simon Saw-Teong Ang kwa kuficha kushirikiana na Serikali ya China na Chuo kukuu cha China wakati huo huo akifanya kazi na Shirika la anga la Amerika [NASA]. Upande wa mashtaka ulisema Ang alikuwa ni mshirika wa siri wa shughuli zaidi ya elfu moja zinazo dhaminiwa na Xi, ambazo Washington inasema China  imezitumia kwa ajili ya kukusanya data nje ya nchi. Pia siku ya Jumatatu Li Xiaojiang, profesa wa zamani wa chuo kikuu cha Atlanta, alikiri kukwepa kodi katika mapato yake ya siri kutoka China, pia akiwa ni mshirika katika mpango wa vipaji elfu moja. Beijing imerudia mara kwa mara kupinga shutuma hizo. "Tunaiongoza dunia katika kutibu virusi vya Korona na utafiti wa chanjo. Ni kinyume na maadili kuishutumu China kwa maneno ya kuzusha na kutengeneza tena bila ya ushahidi wowote," Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Zhao Lijian alisema mnamo siku ya Jumatatu. Onyo la FBI limekuja kufuatia mamia ya kampuni, taasisi na mataifa duniani kote yakishindana kutafuta chanjo ili kuzuia kusambaa kwa virusi vya Korona. Makundi mengi zaidi yanafanya utafiti wa tiba kwa wagonjwa walioathirika tayari. Mpaka muda huu hakuna mafanikio yaliothibitishwa. Chanjo madhubuti itawezesha nchi iliyo gundua kupata mamilioni ya dolari kwa uvumbuzi wake. Wataalamu wengi wanaona kwamba itachukua zaidi ya mwaka mmoja kupata chanjo iliyo thibitishwa, na itachukua muda mrefu zaidi kuzalisha chanjo itakayokidhi mahitaji ya kiulimwengu. Onyo kuhusu wadukuzi wa mtandao kutoka China limeongoza idadi ya shutuma na taarifa zinazo shutumu serikali kwa kusaidia shughuli za udukuzi katika nchi kama Iran, Korea kaskazini, Urusi, na China kuhusu shughuli zinazo husiana na janga la virusi vya Korona, kwa kusambaza habari za uongo zinazo walenga wafanyakazi na wanasayansi. [Chanzo: Khaleej Times]

Amerika inatumia virusi vya Korona kama sababu nyingine ya kuishinikiza zaidi Beijing kurudi katika mazungumzo kutokana na mazoezi ya kijeshi yanayo fanyika kusini mwa bahari ya China kwa lengo la kuzuia kampuni ya kiChina kusimika mtandao 5G, Amerika inaogopea ukuaji na ongezeko la nguvu za China katika ulimwengu.

Pakistan Imeipatia China Kandarasi ya Ujenzi wa Bwawa bila Kujali Upinzani Kutoka India

Mnamo siku ya Jumatano serikali ilitia saini mkataba wenye thamani ya Rupia bilioni 442 kwa kushirikiana na China Power na shirika la Frontier Works (FWO) kwa ajili ya ujenzi wa bwawa la Diamer-Bhasha. China itagharamia asilimia 70 pamoja na FWO, na jeshi la Pakistan, asilimia 30 ya hisa za mkataba huo. Mkataba huo umelenga mfumo wa utawanyaji, bwawa kuu, daraja na uzalishaji nishati ya nguvu za umeme kiasi cha megawati 21. Eneo lenye ukubwa wa ekari milioni nane (MAF) na mita urefu wa 272- kulifanya kuwa ndio bwawa refu zaidi Duniani. Iitakuwa na njia nyingi,  mageti 14  na sehemu tano za kutolea maji. Mfumo huo utajumuisha njia za chini mbili na mfereji vyote vitatu vitakuwa na jumla ya kilomita moja kwa kila kimoja. Daraja hilo litatengenezwa katika muundo wa gilda likijengwa kuelekea katika mkondo wa chini wa bwawa, wakati huo huo mtambo wa kuzalisha nguvu za megawati 21 za umeme zitatosheleza matumizi ya umeme katika eneo la mradi wakati mradi huo ukiwa unaendelea. Waziri Mkuu Imran Khan alidokezwa kuhusu maendeleo ya mradi huo siku kadhaa zilizopita. Kazi za ujenzi wa bwawa zitaanza wiki kadhaa zijazo. Akizungumzia maendeleo, Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Anurag Srivastava alisema kanda ya Gilgit-Baltistan ni sehemu ya mashariki ya Jammu na Kashmiri ambayo ilinyakuliwa kimabavu na Pakistan. “Msimamo wetu ni thabiti na wazi eneo lote la mpaka wa muungano wa Jammu na Kashmiri na Ladakh limekuwa, linakuwa, na litaendelea kuwa eneo muhimu la India,” alisema Srivastava. “Tumesha fikisha madai yetu na kuweka wazi jambo hili kwa nchi zote China na Pakistan kwamba eneo zima la mradi lipo katika mpaka wa India chini ya uvamizi haramu wa Pakistan,” alisema. Pia hapo nyuma, India ilipinga mradi shirikishi uliojumuisha  Pakistan na  China katika eneo la Kashmiri linalomilikiwa na Pakistan mradi ambao ulikuwa ni sehemu muhimu kiuchumi kati ya China na Pakistan. [Chanzo: The Dawn na magazeti mengine].

India itaendelea kupinga uhuru wa ndani wa kimaamuzi wa Pakistan hadi pale itakapoikomboa Kashmiri yote. Njia nzuri ya kufikia hapo, ni Waislamu wa Pakistan watakapo isimamisha tena dola ya Khilafah kwa njia ya Utume  na kumaliza kabisa mzozo na India.

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumamosi, 06 Juni 2020 11:12

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu