Afisi ya Habari
Wilayah Sudan
H. 7 Rabi' I 1447 | Na: HTS 1447 / 20 |
M. Jumamosi, 30 Agosti 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Wanachama wa Hizb ut Tahrir huko Abbasiya Taqli Watoa Wito Mkali kwa Waislamu Kutibua Mpango wa Marekani wa Kutenganisha Darfur
(Imetafsiriwa)
Kama sehemu ya kampeni iliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir/ Wilayah Sudan ya kukwamisha mpango wa kuisambaratisha Sudan kwa kutenganisha eneo la Darfur, na kuzingatia umoja wa Ummah kama suala nyeti, suala la uhai na kifo, wanachama wa Hizb ut Tahrir huko Abbasiya walifanya mkutano mnamo Ijumaa, 6 Rabi' al-Awwal 1447 H sawia na 29 Agosti 2025 M, baada ya swala ya Ijumaa katika Msikiti wa Sheikh Yahya kituo cha kuhifadhi Quran. Walitoa wito wa dhati kwa Waislamu wa matabaka yote, wakiwemo wanasiasa, wanahabari, wanazuoni, maafisa na askari na wengineo, wakiwahimiza kutimiza wajibu wao wa kidini ili kuzuia kujitenga kwa Darfur.
Wito huo ulisomwa na Ustadh Abdul Rahim Abdullah, mwanachama wa Hizb ut Tahrir, katikati ya umati mkubwa wa waumini. Waliosimama kuliani mwake na kushotoni walikuwa baadhi ya wanachama wa Hizb wakiwa wamebeba mabango yakitoa wito wa kukataa kujitenga na mengine yakitoa wito kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu.
Wahudhuriaji waliitikia wito huo kwa nguvu, wakiomba kwamba Mwenyezi Mungu Awalipe kheri wanachama wa Hizb na kubariki juhudi zao.
Ibrahim Othman (Abu Khalil)
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Sudan
Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Sudan |
Address & Website Tel: 0912240143- 0912377707 http://www.hizb-sudan.org/ |
E-Mail: Spokman_sd@dbzmail.com |