Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 21/09/2022

Vichwa vya Habari:

  • Urusi Yasonga Kuyaunganisha Rasmi Maeneo ya Ukraine
  • Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asema Ulimwengu Uko ‘Hatarini na Kulemwaza’ wakati Mkutano wa Kilele Ukifanyika
  • Ujerumani Yataifisha Mali za Urusi

Maelezo:

Urusi Yasonga Kuyaunganisha Rasmi Maeneo ya Ukraine

Viongozi wa mamlaka nne zinazojitangaza kuunga mkono uvamizi wa Urusi katika maeneo ya Luhansk, Donetsk, Zaporizhzhia na Kherson ya Ukraine walitangaza nia yao ya kufanya "kura za maoni" kuhusu maeneo yao yatakayojiunga na Shirikisho la Urusi kuanzia Septemba 23-27. Matangazo hayo yalikuja siku hiyo hiyo ambapo bunge la Duma la Urusi liliidhinisha marekebisho ya kanuni ya jinai iliyoanzisha fahamu za "uhamasishaji," "sheria ya kijeshi" na "wakati wa vita," na kuweka hadi miaka 15 jela kwa kutoroka na hadi miaka mitatu kwa wanajeshi wa kandarasi kukataa kwenda Ukraine. Putin amehitaji kujibu baada ya vikosi vya Urusi kupata hasara kubwa katika eneo la Kharkiv ambapo vifaa muhimu vya kijeshi vya Urusi vilitekwa na wanajeshi wa Ukraine. Kuna uwezekano tishio la kuanganishwa ni jaribio la kufufua mazungumzo na Magharibi kuhusu kuweka udhibiti wa usambazaji silaha kwa Ukraine, pamoja na matumizi ya Ukraine ya silaha hizi kushambulia eneo jipya la Urusi lililounganishwa. Ambayo yote yataonyesha kwamba lengo la awali la Urusi la kuichukua Ukraine linasonga kando zaidi na kufikiwa.

Mkuu wa Umoja wa Mataifa Asema Ulimwengu Uko ‘Hatarini na Kulemwaza’ wakati Mkutano wa Kilele Ukifanyika

Katika tathmini ya kutisha, mkuu wa Umoja wa Mataifa amewaonya viongozi wa dunia kwamba mataifa "yamekwama katika hali mbaya ya utendakazi duniani" na hayako tayari au hayana utashi wa kukabiliana na changamoto zinazotishia mustakbali wa binadamu. "Ulimwengu wetu uko hatarini - na umelemazwa," alisema. Mkutano wa 77 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UNGA) wa viongozi wa dunia unafanyika chini ya kivuli cha vita vya Urusi nchini Ukraine, ambavyo vimeibua mgogoro wa chakula duniani na kufungua mpasuko kati ya dola kubwa kwa njia ambayo haijaonekana tangu Vita Baridi. Akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa ngazi ya juu wa kila mwaka jijini New York, Katibu Mkuu Antonio Guterres alianza hotuba yake kwa kutoa sauti ya matumaini kwa meli iliyokodishwa na Umoja wa Mataifa inayobeba nafaka kutoka Ukraine. Historia ya Umoja wa Mataifa kwa muda mrefu imekuwa ya kuidhinisha mipango ya Magharibi kwa ulimwengu.

Ujerumani Yataifisha Mali za Urusi

Ujerumani imechukua udhibiti wa operesheni za Ujerumani za kampuni ya mafuta ya Urusi ya Rosneft ili kupata usambazaji wa kawi ambayo imetatizwa baada ya uvamizi kamili wa Moscow nchini Ukraine. Kampuni tanzu za Rosneft za Ujerumani, ambazo zinachukua takriban 12% ya uwezo wa kusafisha mafuta nchini, zimekamatwa na kutaifishwa. Rosneft ilijibu katika taarifa yake kwamba hatua hiyo ni kinyume cha sheria na kwamba inaweza kwenda mahakamani kupinga uamuzi huo wa Ujerumani. Kuchukuliwa huko kunajiri wakati ambapo Ujerumani inajitahidi kujiondoa kwenye utegemezi wake wa kawi ya Urusi. Moscow imesimamisha usafirishaji wa gesi asilia hadi Ujerumani kupitia bomba la Nord Stream 1. Ujerumani imeanza kujihusisha na Urusi na kuna uwezekano itaangalia biashara zake zote za pamoja na Urusi. Makabiliano kati ya Ujerumani na Urusi sasa yamepamba moto na kihistoria yamethibitika kuwa hatari kwa bara hilo.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu