Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Mpango wa Khalilzad sio Kuleta Amani bali ni Kuisalimisha Taliban!

Habari:

Mnamo 3 Februari 2020, katika kipindi cha mkutano uliofanyika na waandishi wa habari nchini Uzbekistan, Waziri wa Mambo ya Nje wa Amerika Mike Pompeo alitaka “athibitishiwe ushahidi” kutoka kwa Taliban kwamba itapunguza matukio ya uhalifu ndani ya Afghanistan kabla ya kutia saini makubaliano ambayo yatapelekea mazungumzo ya amani na kuondoa vikosi vya kijeshi vya Amerika kutoka Afghanistan. Pia aliongezea kwamba “Tunachokita kwa sasa ni ‘kuthibitishiwa ushahidi’ wa nia yao na uwezo wa kupunguza matukio ya kiuhalifu, hivyo basi mazungumzo ya Afghan na kuondoka kwa vikosi vya Amerika yatafanyika katika mazingira ya amani.” Pia Pompeo alisema kwamba, ‘‘Tunashughulikia mpango wa amani na uwiano. Mwanzoni kabla tulikuwa karibu kimakubaliano ya kutekeleza mpango huu kwa pande zote mbili lakini Taliban hawakuweza kuonyesha nia yao au uwezo wao au vyote kwa pamoja katika kufikia upunguzaji wa matukio ya kiuhalifu.” (Voice of America)

Maoni:

Amerika, kwa upande mmoja imekuwa ikisisitizia “upunguzaji wa matukio ya kiuhalifu” na kwa upande mwingine imekuwa ikiporomosha mabomu mazito kutoka angani hali ya kuwa mazungumzo ya amani yamekwisha anza. Katika wiki chache zilizopita, mashambulizi kutoka angani yalifanywa na Amerika yamesababisha vifo na mauaji ya mamia ya raia wasiokuwa na hatia kwa upande wa mashariki, kaskazini mashariki, kusini na katika miji mikuu ya Afghanistan. Mashambulizi kama hayo mara nyingi yamekuwa yakifanywa na vikosi vya Amerika sambamba na msaada wa vikosi vya Afghanistan vilivyo chini ya utawala wa sasa, hali hii imekuwa yenye kuchochea kwa jamii kuja juu na kuhamaki. 

Amerika haina makusudio ya kweli ya kutaka kuleta amani ndani ya Afghanistan kwa sababu inajaribu kuwasogeza Taliban katika michakato ya Kidemokrasia na Kimagharibi ndani ya Afghanistan yaani kama vile ilivyokuwa kwa Muungano wa Kaskazini na Chama cha Kiislamu cha Hekmatyar. Kwa upande mwingine vikosi vya kijeshi vya Amerika vimewapiga mabomu 7,423 watu wasio hatia wa Afghanistan mnamo 2019 pekee, kwa udanganyifu wa kwamba wanashambulia adui ili waweze kuisalimisha Taliban kukubaliana na matakwa ya Amerika. Idadi ya mabomu yaliyopigwa mnamo 2019 ni mara saba ya yale yaliyopigwa mwaka 2015. Kiukweli Amerika imepiga mabomu 947 katika mnamo 2015 na mabomu 7,362 na milipuko mnamo 2018 kwa watu wasio na hatia wa Afghanistan. Kiuhakika haya ni katika matukio machache yaliyotimizwa na Amerika ambayo imekuwa ikiyafanya kwa Waislamu wa Afghanistan kabla hata ya makubaliano yoyote ya amani kufanyika.

Amerika imeshirikisha wengi katika vibaraka wake katika eneo hili na ulimwengu wa kiarabu, ikijumuisha Pakistan, Uzbekistan, Qatar, United Arab Emirates, Saudia Arabia na hata Iran katika kuishinikiza Taliban kukubaliana na yale inayotaka Amerika katika mazungumzo yao ya amani. Katika wakati huo huo Serikali ya Aghanistan inaonekana kujitenga kimaksudi katika mazungumzo kwa maelekezo ya Amerika, pengine imesimama kupunguza misimamo ya Taliban pamoja na hali yao ya kutokuthamini misingi ya Kimagharibi ya kidemokrasia ili hatimaye waweze kufikia “miaka 19 ya mafanikio” ya kuona Taliban ikibadilika na kuachana na misimamo yake kidogo kidogo. Mfano wa wazi unaweza kuwa msimamo wa serikali ya Afghanistan katika kusitisha mapigano na Taliban katika kupunguza matukio ya kiuhalifu na Amerika kutokubaliana juu ya vipi kila mmoja atambulike. Zalmay Khalilzad akiwa kama mjumbe maalumu wa Amerika katika maswala ya upatanishi katika kipindi cha karibuni alichotembelea Kabul alisema kwamba “alikuwa na matumaini ya kufikia makubaliano na Taliban juu ya kusitisha mapigano au kupunguza matukio ya kiuhalifu.”

Mpaka kufikia sasa Karibia mikutano 10 imefanyika kati ya Wanadiplomasia wa Amerika na Wawakilishi wa Taliban, kwa kutumaini kwamba Amerika na Taliban wangeweza kufikia makubaliano katika vikao vya mwisho, lakini Zalmay Khalilzad katika safari yake ya karibuni aliyokwenda Kabul alizungumza vitu tofauti kabisa kwamba “kumekuwa hakuna mwelekeo mzuri unaoendelea katika majadiliano na Taliban, lakini tunamatumaini kufikia suluhusho.”

Mwishoni mwa mzunguko wa kikao cha tisa katika mazungumzo ya amani, Khalilzad aliandika kupitia mtandao wa Twitter “Tuko katika mchakato wa makubaliano ya kupunguza matukio ya kiuhalifu na kufungua mlango kwa Waafghanistan kukaa pamoja kujadili heshima na amani endelevu na umoja, kuifanya Afghanistan kuwa huru isiyoitishia Amerika, washirika wake au nchi yoyote nyingine.” Mtu anayeweza kuona waziwazi kutoka katika maelezo yaliyo nukuliwa hapo juu na kuongezeka kwa hofu juu ya Taliban kwamba mazungumzo ya amani lazima yacheleweshwe katka wakati huu na baadaye yaendelezwe haya yote ni kwa sababu tu ya Trump kutaka zoezi hili liende sambamba na tarehe za uchaguzi utakaofanyika nchini Amerika mnamo mwaka huu.

Inaonekana wazi kwa mujibu wa habari iliyo nukuliwa hapo juu pamoja na hofu waliyonayo kwamba huu mchakato kihakika ni ulaghai tu wa kisiasa, wenye lengo la kuivunja, kuidhoofisha na kuisalamisha Taliban, kwa upande mmoja, kumaliza vita virefu vya Amerika nchini Afghanistan, na kwa upande mwingine, kuirahisishia kazi Amerika kufikia malengo yake bila kutumia nguvu ambapo imekuwa vigumu kwake kufikia malengo hayo kwa miaka 19 sasa kupitia njia za kivita. Kwa kuongezea, chama kinachoongzwa na Trump kinalenga kutumia mazungumzo haya ya amani nchini Afghanistan kama mtaji wake wa kisiasa katika uchaguzi utakaofanyika 2020 katika kuibadilisha rai ya umma nchini Amerika na ulimwengu kuhusiana na kwamba Amerika kushindwa katika vita vya Afghanistan. Kiuhakika, Amerika haiko tayari kuiachilia Afghanistan, lakini inatafuta muonekano mwingine wa kuendelea kuwepo Afghanistan ili kuweza kuendelea kuitumia kijiiografia kama nukta ya kimikakati ya kudumu katika kupanua ushawishi wake dhidi ya Uchin, Urusi, Pakistan na Iran. Mitazamo ya kisiasa ya Amerika na Magharibi dhidi ya Afghanistan bado haujabadilika kwa sababu, kuongezea umuhimu wa kimikakati wa Afghanistan, ni migodi asilia yenye kushangaza na uzalishaji wa madawa kwa kiasi kikubwa imekuwa ikiwavutia wakoloni Wakimagharibi na kuwafanya kuwa makini katika kutupia jicho kindani dhidi ya maeneo ya asili ya hifadhi ya Afghanistan. Kwa hivyo, Amerika imekuwa ikirudia kusisitiza kuwepo kwa majasusi wake wengi na huku ikiendelea kudhihirisha nia ya kundoa vikosi vyake vyote kutoka Afghanistan.

Na kwa muda mfupi, lau Taliban ingeliweza kufaulisha maslahi ya Amerika ndani ya mchakato huu, ingelifahamika wazi kwamba makafiri hususan Amerika hawana tena uwezo wa kibinafsi kwa sababu serikali ya Amerika imejumuisha taasisi tofauti ambazo kwamba lau mchakato utafaulisha maslahi ya taasisi fulani itapongezwa na kinyume chake itadhoofika lau haitofaulisha maslahi ya mwingine. Kwa sababu sera ya kigeni ya Amerika inazunguka baina ya taasisi na vyama; hivyo basi, lau taasisi yoyote iliyopo na/au chama kitafikia kutia saini makubaliano na kundi na/au nchi; hakuna dhamana kwamba makubaliano hayo yatawekewa ahadi ya kutimizwa na taasisi na chama chengine kesho. Mtu anaweza kuurudia Mpango wa Nuklia wa Iran, Makubaliano ya Paris ya Tabia ya Nchi na mikataba na makubaliano mengi ili kuona kwamba ni rahisi kwa Amerika kujiondosha katika mpango.

Hatimaye, suluhisho msingi kwa tatizo hili hatari ni kusitisha mazungumzo ya amani na Amerika hivi leo na sio kesho, na kuendelea kupigana na Amerika mpaka izikwe katika Makaburi ya Ufalme ili kushindwa kwake nchini Afghanistan kutahisika duniani kote. Kiuhakika uongozi huu wa udanganyifu na ujanja lazima uvunjwe na kutoa nafasi ya kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume kutoka katika kizuizi kikubwa. Hii ni katika moja ya vitendo vikubwa ambavyo vitafika mwisho kupitia hatua zenu. Kisha kutapatikana ushindi kupitia kuwapindua wahalifu wakubwa na madhalimu wa zama hizi!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Saifullah Mustanir

Mkurugenzi wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Afghanistan

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:07

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu