- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Watu wa Bangladesh hawajamuondoa Hasina ili kukabidhi ‘biashara’ yao kwa Marekani
(Imetafsiriwa)
Habari:
Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na kiongozi wa mpito wa Bangladesh Muhammad Yunus pembezoni mwa mkutano wa kila mwaka wa Umoja wa Mataifa, katika kuonyesha uungaji mkono baada ya maasi kuiangusha serikali ya kiimla ya Hasina. Yunus, mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, baadaye alisifiwa sana na rais wa zamani Bill Clinton, ambaye alimwambia “Wewe ndiye mzee pekee ninayemjua ambaye aliwahi kuandikishwa kwa nafasi yake ya utukufu na vijana wa nchi yake,” Clinton alidhihaki kuhusu kuinuka kwa Yunus hadi kiongozi wa muda. “Hiyo ni kwa sababu amefanikiwa kufanya kile ambacho sisi sote lazima tufanye: sote tunapaswa kubaki katika biashara ya baadaye.” (The Daily Sun, 25 Septemba 2024)
Maoni:
Sababu ya watu wengi nchini Bangladesh kusimama kishujaa dhidi ya Hasina na kuuondoa utawala wake kwa kumwaga damu yao ilikuwa ni kukombolewa sio tu kutokana na udhalimu wake bali pia kutokana na ubeberu mamboleo wa Kimagharibi. Ingawa India ilimuunga mkono Hasina bila haya, lakini watu wa Bangladesh walijua kuwa Amerika pia ilimtumia Hasina kwa gharama ya ustawi wa watu kwa faida na manufaa yake ya kijiografia. Kwa hivyo, serikali ya mpito ya Bangladesh lazima isiwe na shaka yoyote kwamba kujitolea kwa watu, utashi na matarajio yao hayakuwa ya kukabidhi ardhi kutoka kwa mshiko wa India hadi kwa mabeberu wa Magharibi. Lakini kwa bahati mbaya, serikali ya mpito pia haichezi tofauti na watawala vibaraka wa kisekula. Watu wa Bangladesh hawaruhusiwi na watawala na wanasiasa hawa kutoka nje ya mchezo uliowekwa na Magharibi. Tunaona hamu ya Ummah ya mabadiliko ya kweli, hamu ya ukombozi kutoka kwa ubeberu wa Magharibi ikikabidhiwa kwa hila za nchi za Magharibi. Kama vile tulivyoshuhudia katika kipindi cha baada ya Mapinduzi ya Kiarabu, hapa pia tunaona hamu ya watu ya mabadiliko ikiendeshwa na kudhibitiwa na utawala wa magharibi. Vijana wetu wanawasilishwa katika majukwaa mbalimbali nchini Amerika kana kwamba hatuwezi kusimama kwa miguu yetu bila kutambuliwa na Amerika. Vijana wetu wanawasilishwa kama mashujaa kwa Amerika ya kibeberu ambao wamemruhusu Hasina kwa miaka mingi kuwa dhalimu wa kutisha. Ajenda kuu sio kuwaruhusu wavulana wetu kuiona Amerika kama adui yao. Kwa hakika Mkuu wa sasa wa Bangladesh (Dkt. Muhammad Yunus) aliziomba dola za kibeberu za kigeni: “Kwa hiyo, tafadhali wasaidieni, waungeni mkono. Ili ndoto zao zitimie. Na, hili ni jukumu tunalolichukua pamoja. Na, mtakuwa pamoja nasi,” alisema haya yote akiwa amemshika mkono Bill Clinton.
Ili kufikia ukombozi wa kweli, watu wa Bangladesh lazima wampe mamlaka yao mtawala (Khalifa) ambaye ataendesha mambo ya watu kwa kupambana na mfumo wa kilimwengu wa Kimagharibi. Mkataba wa utawala naye utaegemezwa juu ya sharti la uhuru kutokana na makafiri wa kibeberu na utekelezaji wa Hukmu za Shariah kwa ukamilifu wake. Isipokuwa ikiwa tutashindwa kurudisha Khilafah, usimamizi wa kweli wa Waislamu, utashi wa watu wa kuleta mabadiliko vitaambulia patupu kwa kila uasi mkubwa kama huo, na, cha kusikitisha, tutakuwa daima katika kitanzi cha maangamivu cha demokrasia ya kisekula ya Magharibi. Mwenyezi Mungu (swt) asema,
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا اسْتَجِيبُوا للهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُمْ لِمَا يُحْيِيكُمْ]
“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele.” [Surah Al-Anfal:24].
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Talha Hossain
Mjumbe wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Bangladesh