Ijumaa, 20 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Uswidi Katika Mapambano ya Uzazi: Mlima Umezaa Panya

(Imetafsiriwa)

Habari:

Nchini Uswidi, babu na bibi sasa wanapokea pesa kutoka kwa serikali kwa ajili ya kuwatunza wajukuu zao. Sheria inayohusiana na hili ilianza kutumika msimu huu wa joto. (ru.euronews)

Maoni:

Habari hii ni mfano mwengine tena wa majaribio yasiyofanikiwa ya nchi za Ulaya kutatua tatizo la kutoweka kwa idadi ya watu wao.

Hapa, kwanza kabisa, ningependa kudokeza baadhi ya nukuu kutoka kwa nususi za habari hii, ambayo hutumika kama alama fasaha za kufeli kwa thaqafa ya Kimagharibi katika kuinua kiwango cha uzazi miongoni mwa wafuasi wake.

Kwa hivyo, hadithi hii ya habari inazungumza juu ya Maria Karlsson, mama mmoja anayefanya kazi ambaye anamlea mtoto wa miaka mitatu. Mama yake mwenyewe amekuwa akimsaidia na hii ni tangu kuzaliwa kwa mtoto huyo, na kuanzia sasa atakuwa akifanya hivi kwa pesa kutoka kwa serikali ya Uswidi.

Kwa mujibu wa mwakilishi mmoja wa Shirika la Bima ya Kijamii la Uswidi, sheria hiyo mpya inalenga kukuza usawa wa kijinsia. Waziri wa Usalama wa Jamii Anna Tenje, ambaye alianzisha sheria hiyo, anatumai kuwa Uswidi itakuwa mfano kwa Ulaya nzima. Pia anaamini kuwa sheria hii itawahimiza vijana kupata watoto, lakini pia kubaki katika soko la ajira na kuishi maisha changamfu ya kufanya kazi.

Kwa kweli, hali iliyoelezwa hapo juu ni ya kawaida kwa idadi kubwa ya kina mama katika nchi za Ulaya.

Ni muhimu kwamba mama asiye na mwenza anayelea mtoto hawezi kuelewa kwamba yuko chini ya shinikizo kutoka kwa serikali yake, ambayo inaleta fahamu za usawa wa kijinsia na kuendelea kumfanyia kazi ili abaki katika soko la ajira na kuishi maisha ya ufanyaji kazi. Ni jambo kubwa jinsi Mwenyezi Mungu alivyowatia upofu watu hawa wanaoona furaha katika kumwacha mtoto wao, hata kwa bibi, na kwenda kufanya kazi kwa ajili ya kuendeleza taaluma na kutaka kujiimarisha mbele ya jamii nzima na hasa machoni pa baba wa mtoto (ambaye kuna uwezekano mkubwa aliwatelekeza).

Serikali hizi zimedunishwa kufikia hadi zinalazimika kulipa pesa kwa babu na bibi ili ili kuwashajiisha vijana kupata watoto.

Bila shaka, kuongeza kiwango cha uzazi huko Magharibi kunawezekana tu kwa kukataa masanamu ya ulimwengu wa kisasa wa kidemokrasia. Hizi ni fahamu kama vile usawa wa kijinsia, uhuru wa kibinafsi, na ukuzaji wa mtindo wa maisha wa watumiaji.

Ni fahamu hizi ndizo ambazo ni kikwazo kisichoweza kushindwa katika kutatua tatizo la kupungua kwa viwango vya uzazi. Baada ya yote, fahamu ya kindoto ya usawa wa kijinsia imewanyima wanawake na familia katika nchi za Magharibi hamu ya kimaumbile ya kuwa na watoto wenye afya, wengi. Uhuru wa kibinafsi na fikra ya utumiaji huharibu kizazi kipya na kukifanya kisiweze kuunda familia zenye nguvu, ambazo ndio msingi wa jamii yoyote.

Tofauti na ulimwengu wa Magharibi, katika ulimwengu wa Kiislamu hakuna tatizo la kile kinachoitwa umri wa kustaafu, kwani Sharia imeweka sheria imara zinazoendana na maumbile ya mwanadamu na kuhakikisha maendeleo endelevu.

Hivyo, Mtume (saw) ameshajiisha kuwa na watoto wengi. Na matokeo yake, hakuna tatizo na wastaafu. Kwa sababu nusu makumi ya watoto wa wazazi wowote wazee huwapa pesa kwa urahisi, aghlabu bila hata kuhitaji msaada kutoka kwa serikali.

Sharia ya Mwenyezi Mungu imeweka sheria zinazogawanya kwa uwazi majukumu kati ya mume na mke, hivyo kuhakikisha familia zenye nguvu ambazo kwazo talaka ni nadra mno.

Mwanamke wa Kiislamu, akiwa na haki ya kuajiriwa kwa mujibu wa Uislamu, hajawahi kuhisi haja ya kwenda kazini, kwa sababu wajibu wa kumpa matumizi yeye na watoto wake umewekwa na Uislamu wote kwa mume. Ikiwa atafanya kazi, basi mshahara wake ni mali yake, ambayo hailazimiki kugharamia familia na mume hawezi kumlazimisha kufanya hivyo. Ndiyo maana kiwango cha ajira kwa wanawake katika ulimwengu wa Kiislamu ni cha chini sana. Hili halihusiani kabisa na ukiukwaji wa haki za wanawake, kama wenye chuki na Uislamu wanavyojaribu kuwasilisha.

Ili kutatua tatizo la idadi ya watu, Ulaya ya kisasa inahitaji kitu chochote chini ya kuukaa ubepari, ambao ndiyo sababu halisi ya kutowezekana kutatua tatizo hili leo. Ni kukataliwa kwa mfumo wa kibepari ambako kutairuhusu Ulaya kuongeza kiwango cha uzazi, wakati idadi ya watoto katika familia za Ulaya ilifikia watoto 6-7, kama ilivyokuwa hadi hivi karibuni.

Kwa kushindwa kuachana na maadili yao potovu, serikali ya Uswidi, katika juhudi zake za kuongeza kiwango cha uzazi, ni kama mlima uliozaa panya.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Fazil Amzaev
Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Ukraine

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu