Jumapili, 20 Jumada al-thani 1446 | 2024/12/22
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Sintofahamu ya GISB: Nukta ya Mabadiliko ya Kushughulikia Upotofu na Kuregesha Khilafah

(Imetafsiriwa)

Habari:

Katika wiki za hivi karibuni, Global Ikhwan Sdn Bhd (GISB) imekabiliwa na uchunguzi mkali kutoka kwa mamlaka kufuatia wasiwasi wa muda mrefu juu ya desturi zake potovu. Ingawa ripoti zilikuwa zimewasilishwa dhidi ya GISB mapema zaidi, hatua za hivi majuzi za polisi zinaashiria hatua ya kwanza muhimu ya kupunguza shughuli za kundi hili. GISB, ambayo mizizi yake inatoka kwenye vuguvugu la Al-Arqam ambalo sasa limezimika, imevutia umakini wa watu wengi kwa kulingania vitendo vya upotofu vya Aurad Muhammadiyah na madai ya utovu wa nidhamu, hasa katika uendeshaji wa nyumba za misaada. Kwa hivyo mamlaka zimeona kuwa ni muhimu kusitisha shughuli za GISB kabisa, ikiwemo biashara zake na maduka ya kijamii, katika juhudi za kudhibiti kile wanachokiona kama tishio kubwa kwa utulivu wa kidini na kijamii.

Maoni:

Mtazamo wa sasa wa mkengeuko wa GISB unaangazia suala pana zaidi ambalo halipaswi kupuuzwa—kutolingana kati ya mifumo ya sasa ya kijamii na kanuni za Kiislamu. Ingawa mafundisho ya GISB yamekosolewa sana na watumiaji wa mitandao, serikali, na wengineo, swali halisi sio tu kuhusu makosa ya kiitikadi ya kundi hili. Ni lazima pia tuzingatie matatizo ya kinidhamu ndani ya serikali, miundo ya kiuchumi, na mifumo ya kisheria ambayo haiambatani na sheria ya Kiislamu. Kwa mfano, mifumo ya utawala inayofanya kazi bila kuzingatia maadili ya Kiislamu inaleta mtengano kati ya imani na shughuli za kijamii. Vile vile, mifumo ya kiuchumi iliyokita mizizi katika riba na kukosekana kwa usawa, pamoja na mifumo ya kisheria ambayo inatanguliza usekula badala ya Shariah, inaakisi mikengeuko ya ndani zaidi ya kijamii kutoka kwa Uislamu. Mikengeuko hii ina athari kubwa, inayoongoza sio tu kwa upotofu wa kiitikadi bali pia katika muozo wa kimaadili na kijamii ndani ya nchi. Kinachoakisiwa katika mgogoro huu, kwa kweli, kinapita zaidi ya upotofu wa kiitikadi. Wakati mamlaka zimechukua hatua haraka dhidi ya GISB, fikra nyengine na vitendo viovu ambavyo pia vinakiuka kanuni za Kiislamu zinaendelea kushamiri bila kudhibitiwa. Kufeli kimfumo kushughulikia mikengeuko hii mipana ya kijamii kunachangia mmomonyoko wa maadili ya Kiislamu katika maisha ya kila siku.

Kwa bahati mbaya, baadhi ya viongozi wa Waislamu wamejaribu kuzima harakati zozote zinazotaka kurudi kwenye Uislamu wa kweli, wakiziita juhudi hizo kuwa ni za itikadi kali au potofu. Hili linadhihirisha upinzani wa kimsingi kwa kusimamishwa tena kwa Uislamu, huku baadhi ya viongozi wakiwa tayari kukandamiza mipango inayotetea utekelezwaji kamili wa Shariah kwa hofu ya kuhusishwa na misimamo mikali.

Kwa kuhitimisha, ingawa kufichuliwa kwa upotovu wa itikadi  ya GISB ni muhimu, inapaswa kuonekana katika muktadha wa kushindwa kupana kwa jamii. Mzizi wa suala hilo haupo tu katika mkengeuko wa kiitikadi uliokithiri katika jamii bali pia katika mkengeuko wa kimfumo kutoka kwa utawala, uchumi na sheria unaozingatia Sharia, ambao kwa pamoja unachangia kuporomoka kwa maadili tunayoshuhudia leo. Tunatoa wito kwa jamii kutathmini upya mifumo tunayoishi chini yake na kujitahidi kurudisha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu chini ya Shariah, ambao unaweza kupatikana tu kupitia kusimamisha tena Khilafah. Pasi na mfumo huo wa kina wa utawala, juhudi za kurekebisha matukio ya upotofu zitasalia kuwa pungufu, na muundo wa maadili wa jamii utaendelea kumomonyoka.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Dkt. Mohammad – Malaysia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu