Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Marekani Yazunguka Afrika Kujaribu kuziba Aibu ya Kiulimwengu ya Urasilimali

(Imetafsiriwa)

Habari:

Mke wa rais wa Marekani Dkt Jill Biden Mnamo siku ya Jumapili Februari 26, 2023 alitamatisha ziara yake ya siku tano katika mataifa mawili barani Afrika. Hii ilikuwa ni ziara yake ya sita barani, na ni ya kwanza huko Namibia, ya sita nchini Kenya. Ziara ya Dkt Biden inaenda sambamba na maazimio ya mkutano wa hivi karibuni wa viongozi wa Kiafrika huko Washington ambapo rais wa Marekani Joe Biden aliahidi ushirikiano zaidi na Afrika. Jill, aidha aliangazia masuala ya kuwawezesha wanawake na vijana, juhudi za kukabiliana na ukosefu wa chakula na kushajiisha maadili ya pamoja ya Kidemokrasia.

Maoni:

Ziara hii imekuja miezi kadhaa baada ya rais wa Marekani Joe Biden kuwaalika viongozi 49 wa nchi za Afrika jijini Washington na akaahidi kwamba “Marekani iko tayari kujali mustakabali wa Afrika”. Katika mkutano huo wa siku tatu mwezi Disemba, Biden alitangaza kwamba ataelekea barani Afrika katika msimu huu wa joto na kwamba viongozi wakuu wa utawala wake akiwemo mkewe Jill Biden, makamu rais wake Harris watafanya ziara mwaka huu kuonesha dhamira kubwa katika kushirikiana na Afrika. Kama gazeti la Washington Post, ziara ya mke wa rais ni sehemu ya azma kubwa ya kusaidia mataifa ya Afrika hasa ikizingatiwa kwamba athari ya China barani Afrika inakua ambapo wamediriki majasusi wa Kiamerika kutaja kwamba China inaangalia suala la kuipa silaha Urusi hatua ambayo waziri wa mambo ya nje wa Marekani ameitaja kwamba huenda ikawa ni “tatizo kubwa”.

Ni dhahiri kwamba Marekani inaona China kama tishio dhidi ya maslahi yake barani Afrika. Maslahi ya Marekani yanahitaji kushinikiza Afrika kuchagua, na hii kama ilivyokuwa mwanzoni pale Marekani iliposhinikiza serikali za Kiafrika kupiga kura katika baraza la Umoja wa Mataifa China ikasita kupiga kura ya kushtumu uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. Kwa jumla diplomasia ya Marekani barani Afrika itakuwa yenye athari kubwa zaidi kama haitopangiliwa kirai ya “sisi ama wao” hasa dhidi ya China. Mapema, ndani ya utawala wa Biden Waziri wa Mambo ya nje Antony Blinken aliambia washirika wake kwamba Marekani haitowatarajia wao kuchagua baina utawala wa Washington na Beijing. Ni muhimu kuashiria kwamba tokea mwaka wa 2000 serikali ya China imekuwa ikifanya makongamano ya kibiashara baina yake na Afrika kila baada ya miaka mitatu kama mbinu ya kuimarisha mahusiano yake ya kidiplomasia na maslahi yake ya kibiashara. Kwa sasa China inatajwa kuwa ndio mshirika mkubwa wa Kibiashara wa bara la Afrika. Na taifa hili ndilo mwekezaji mkubwa katika uekezaji wa kigeni kwa Afrika ambao ni karibu mara mbili ya uekezaji wa Marekani.

Kuhusu uwezeshaji wa wanawake na vijana, ukosefu wa usalama wa chakula na Demokrasia, Dkt Jill aliweka wazi "Siku zote nimekuwa nikiamini kuwa kusaidia wanawake na vijana kote ulimwenguni ni muhimu kwa mustakabali wetu wa pamoja, pamoja na elimu, afya, na uwezeshaji katika moyo wa yote” Maoni haya yanaonyesha kejeli ya hali ya juu kwani wanajeshi wa Marekani wamekuwa wakifanya ukatili dhidi ya wanawake duniani kote kwa kibandiko cha kurejesha Demokrasia na 'vita dhidi ya ugaidi' kama ilivyo nchini Afghanistan na Somalia. Wanasiasa wa Kimagharibi akiwemo mke wa rais  lazima watambue kuwa mfumo wanaouamini na kuukumbatia wa Kirasilimali na kuupigania duniani kote umesababisha ukandamizaji wa wanawake sio tu barani Afrika bali duniani kwa jumla. Wanawake na vijana wameteseka sana kutokana na kutawaliwa na hadhara ya Kimagharibi inayotokana na itikadi ya kisekula.

Kenya na Namibia bali Afrika nzima imegubikwa na viwango vikubwa vya umaskini, njaa na magonjwa. Sera mbovu za biashara zinazotetewa na Marekani na Ulaya kama vile soko huria zimesababisha maafa ya kiuchumi yanayoshuhudiwa katika bara hilo tajiri. Muhimu kutambua kwamba, sera ya Biden kwa Afrika ni mwendelezo tu wa juhudi za kibeberu kukoloni na kunyonya nchi za Kiafrika. Mipango ya Marekani, Ulaya na China inalenga kuficha aibu ya itikadi ya ubepari na si kupendelea Afrika iliyo bora zaidi. Safari hizi si nyingine bali ni mipango ya kikoloni iliyokusudiwa kuficha aibu ya Ubepari. Kwa hiyo si kweli kwamba Marekani, Ulaya na China zinaitakia mema Afrika badala yake wana ajenda ile ile ya kuisababishia madhara zaidi. Amerika na itikadi yake ya kibepari ndio chanzo pekee cha matatizo yote duniani. Wafuasi wake wanazunguka dunia nzima wakijaribu kwa siri kuficha aibu yao wenyewe, na maafa, kushindwa na mapungufu ya itikadi yao. Uislamu ndio mfumo pekee unaohitajika duniani ili kudhamini utu na hadhi ya wanawake na vijana.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari wa Hizb ut-Tahrir Kenya

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu