Jumanne, 03 Jumada al-awwal 1446 | 2024/11/05
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Je, Kizuizi cha Nyuklia cha Pakistan ndio Mstari Mwekundu Unaofuata, wa Kuvukwa?

(Imetafsiriwa)

Habari:

“Pakistani na IAEA zitaongeza ushirikiano katika matumizi ya amani ya sayansi na teknolojia ya nyuklia, hasa katika kilimo na matibabu, kwa manufaa ya nchi hiyo na majirani zake. Hayo yalikuwa ndiyo matokeo ya safari ya siku mbili ya Mkurugenzi Mkuu Rafael Mariano Grossi nchini Pakistan wiki hii, ambapo alikutana na uongozi wa nchi hiyo - akiwemo Waziri Wakuu na Waziri wake wa Mambo ya Nje - na kutembelea vituo vingi vya nyuklia kote nchini, baadhi yake alivizindua yeye. ” (Chanzo tovuti ya IAEA)

Maoni:

Ratiba ya kina na makadirio ya ziara ya Mkurugenzi Mkuu wa IAEA nchini Pakistan mnamo Februari 2023, inasikitisha. Ni kana kwamba watawala wa Pakistan walikuwa wanatafuta idhini ya IAEA ya mpango wetu wa nyuklia. Ni wazi kwamba watawala wetu wamejitolea kwa itikadi ya Bajwa, ya kuipa India hali ya usalama, kupitia kubadilisha ujumbe wa kujizuia, kwa simulizi ya matumizi ya amani ya teknolojia ya nyuklia. Kufuatia mtindo wa Musharraf wa kuvuka mistari mekundu, huku akitumia mstari mwekundu unaofuata, mabaya zaidi yanatarajiwa. Urejeshaji wa simulizi ya kujizuia inaweza kufuatiwa na upokonywaji wa silaha za nyuklia endapo Khilafah haitasimamishwa hivi karibuni.

Hebu natuzingatie mistari mekundu ambayo imevukwa. Baada ya 9/11, wakati marehemu Jenerali Pervez Musharraf alipovuka mstari mwekundu kuhusiana na Afghanistan. Alifinika usaliti wake kwa hoja kwamba mali za nyuklia, Kashmir na uchumi vitaokolewa. Kisha akavuka mstari mwingine mwekundu, kwa kuwakandamiza mujahidina huko Kashmir, kwa ombi kwamba mali za nyuklia na uchumi vitaokolewa.

Mistari mekundu inaendelea kuvukwa. Wasiwasi uliongezeka wakati wakoloni walipoiweka Pakistan katika orodha ya kijivu ya FATF, na tishio la kuigeuza kuiweka kwenye orodha nyeusi. Wakikabiliwa na shinikizo, watawala wa Pakistan walizima msaada wowote kwa Waislamu wa Kashmir Inayokaliwa kimabavu, kutoka Pakistan. Walifanya hivyo kwa gharama ya kuisalimisha Kashmir kwa Dola ya Kibaniani, wakati Modi alipoiunganisha kwa nguvu mnamo Agosti 2019. Ni ukweli ambao umekubaliwa hata na duru tawala. Baada ya kuvuka mstari huu mwekundu, watawala walisema kwamba uchumi utakuwa salama.

Sasa ni uchumi wa Pakistan ndio unaoporomoka kutokana na watawala kujiingiza katika maagizo ya kiuchumi ya wakoloni, ikiwemo kushuka kwa thamani ya sarafu, malipo ya riba, kupanda kwa bei ya mafuta na nishati na ongezeko la kodi. Baada ya mstari huu mwekundu pia kuvukwa, watu sasa wanajadili mstari mwekundu unaofuata, ambao ni mali za nyuklia.

Ilikuwa katika hali hii ambapo IAEA ilizuru Pakistan. Wapakistan walishtushwa na kiwango cha ziara hiyo, pamoja na wakati wake. Ilikuja baada ya Rais Joe Biden Biden, alipokuwa akihutubia harambee ya kuchangisha fedha kwa Wabunge wa Democrat mnamo Oktoba 2022, kusema kwamba Pakistan "inaweza kuwa moja ya mataifa hatari zaidi ulimwenguni" kwa kumiliki "silaha za nyuklia bila mshikamano wowote."

Watu wa wenye nguvu lazima wasongee sasa ili kuzuia mstari mwekundu unaofuata usivukwe. Hakuna chochote chengine kitakachozuia hilo ila kwa kusimamisha kwao Khilafah kwa Njia ya Utume. Khilafah itabadilisha itikadi ya uzuiaji wa chini, kwa utawala kamili. Haitanyenyekea kwa mfumo wa kiulimwengu wa Kimagharibi kwa ajili ya uhalali wa kimataifa wa mpango wetu wa nyuklia. Badala yake itatia hofu nyoyoni mwao.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Mhandisi Shahzad Shaikh
Naibu Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu